JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
TMDA YAONYA JUU YA UWEPO WA DAWA BANDIA SOKONI

- Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) imegundua uwepo wa dawa bandia aina ya ‘Gentrisone 10g cream’

- Inafanana na dawa halisi ila dawa halisi haijawahi kuwa na namba ya toleo GNTRO X030 kama ilivyo kwenye dawa hiyo bandia

Zaidi, soma https://jamii.app/GentrisoneBandiaTZ
KENYA: MUME AMNYOFOA MDOMO MKE WAKE

> Jackline Kerubo (39) mkazi wa Tanga Kona anauguza majeraha baaada ya mume wake kumnyofoa mdomo na sikio kwa kumtafuna kwa meno kufuatia ugomvi baina yao

> Jackline alitaka kwenda kuchuma mboga katika shamba la jirani yake lakini mume wake alimkataza na ndipo ulipozuka ugomvi kati yao

Soma - https://jamii.app/MeAtoaMdomoKe
GUINEA YAWA YA 6 KUMTIMUA KOCHA BAADA YA AFCON

- Kocha Paul Put amefukuzwa kufuatia timu ya Taifa ya Guinea kufanya vibaya katika michuano ya Mataifa ya Afrika

- Nchi nyingine zilizofukuza Makocha baada ya kutoka #AFCON2019 ni Namibia, Tanzania, Misri, Uganda na Cameroon
IRENE UWOYA NA STEVE NYERERE HAWAJASAJILIWA BASATA KUFANYA SANAA

- Kaimu Katibu wa BASATA, Onesmo Kayanda ameeleza baada ya kumalizika kikao kati yao na wasanii hao

- Aidha, amesema wanakemea vikali kitendo cha Uwoya kurushia fedha Wanahabari

Zaidi, soma https://jamii.app/UwoyaSteveHawajasajiliwaBasata
WALIMU WABAKA MWANAFUNZI NA KUMPA UJAUZITO

> Polisi Mkoani Katavi inawashikilia walimu wawili wa Shule ya Msingi Kambuzi kwa tuhuma za kumbaka kwa nyakati tofauti mwanafunzi wa darasa la saba na kumsababishia ujauzito

> Watuhumiwa ni Ambukile Mwakapala na John Ndenje

Soma - https://jamii.app/MchAbakaMtotoMimba
SUDAN: Viongozi wa waandamanaji na Jeshi wametia saini tamko la kisiasa la kugawana madaraka
-
Hata hivyo mazungumzo bado yatafanyika katika siku zijazo kuhusu mambo mengine yanayoendelea kuzua mgongano kwenye makubaliano yaliyofikiwa Julai 5 kati ya pande hizo mbili
MICHEZO: Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limeamua kuwepo kwa mchezo mmoja tu wa fainali ktk mashindano yake mawili ya ngazi ya klabu Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho Afrika

> Uamuzi huo umefikiwa leo kwenye kikao cha Kamati ya Utendaji ya CAF

#JFMichezo
MAREKANI: El CHAPO AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA

- Joaquin ‘El Chapo’ Guzman (62), amehukumiwa kifungo cha maisha gerezani baada ya kupatikana na hatia katika makosa 10 yakiwemo ya kusambaza #DawaZaKulevya na utakatishaji fedha

Zaidi, soma https://jamii.app/ElChapoLifeInPrison
DAR: AMPIGA NA KUMUUA MKE WAKE KABLA YA KUUCHOMA MWILI MOTO

- Polisi inamshikilia Khamis Luwongo(38) kwa tuhuma za kumuua na kumchoma moto mke wake, Naomi Marijani(36)

- Baada ya mauaji aliwataarifu ndugu wa Naomi kuwa mke haonekani nyumbani na hivyo kwenda Polisi kuripoti

Zaidi, soma https://jamii.app/AmuuaMkeAmchoma-Dar
BEKI WA TOTTENHAM, KIERAN TRIPPIER AJIUNGA ATLETICO MADRID

- Amejiunga na kikosi cha Diego Simeone kwa kandarasi ya miaka mitatu kwa ada ya Paundi Milioni 20 (Tsh. 57,233,000,000)

- Anakuwa mchezaji wa kwanza raia wa England kuchezea Atletico ndani ya miaka 95 iliyopita
MWANZA: POLISI WALIOSINDIKIZA DHAHABU WAFUTIWA MASHTAKA

> Mkurugenzi wa Mashtaka nchini amewafutia kesi askari Polisi 8 waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi

> Pia amefuta kesi nyingine 322 wakiwemo wafungwa 70 kutoka gereza la Butimba ambako Rais Magufuli alifanya ziara juzi

Soma - https://jamii.app/DPPAfutaMashtaka
BASHE: WALICHOFANYA KINANA NA MAKAMBA KINAKIUKA KATIBA YA CCM

- Mbunge Hussein Bashe(CCM) amesema barua ya Wazee hao kuhusu Musiba ina lengo la kumchafua Rais Magufuli na kuigawa CCM

- Amesema Musiba si mwanaCCM huwezi kumshtaki ndani ya CCM

Zaidi, soma https://jamii.app/BasheVsKinanaMakamba
TABORA: KIZIMBANI KWA KUKUTWA NA KAKAKUONA

- Thadeo Shahibu amefikishwa Mahakamani jana Julai 17, akikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi

- Amekutwa anamiliki mnyama, Kakakuona kinyume na sheria namba 5 ya Uhifadhi Wanyamapori ya mwaka 2009

Zaidi, soma https://jamii.app/KizimbaniAkutwaKakakuona
Pongezi toka kwa Balozi wa Denmark nchini kwa Mkurugenzi wetu Maxence Melo kupata Tuzo ya Kimataifa ya Uhuru wa Habari
Gazeti la The Monitor la nchini Uganda lilivyoandika kufuatia Mkurugenzi wetu, Maxence Melo kutunukiwa Tuzo ya Kimataifa ya Uhuru wa Vyombo vya Habari
Salaam za Pongezi toka Ubalozi wa Marekani nchini kufuatia Mkurugenzi wetu, Maxence Melo kutunukiwa Tuzo ya Kimataifa ya Uhuru wa Vyombo vya Habari
UGONJWA WA EBOLA WATANGAZWA KUWA JANGA LA DHARURA DUNIANI

> Shirika la Afya Duniani limetangaza ugonjwa wa Ebola kuwa dharura ya kiafya duniani kutokana na ugonjwa huo kuua watu 1,668 katika nchi ya Kidemokrasia ya Congo tangu mwezi Agosti 2018

> Uamuzi huo umechukuliwa na jopo la wataalamu na shirika limezingatia vigezo kadhaa, ikiwemo hatari ya kusambaa kwa virusi vya Ebola duniani

Soma - https://jamii.app/EbolaGlobalEmergency
RASMI: MATTHIJS DE LIGT ASAJILIWA JUVENTUS

- Beki huyo raia wa Uholanzi mwenye miaka 19 amesajiliwa kwa ada ya Paundi Milioni 67.5 (Tsh.193,519,125,000) kutoka Ajax kwa mkataba wa miaka mitano

- Alikuwa akiwaniwa pia na vilabu vya Manchester United, Barcelona na PSG
Salaam za Pongezi toka kwa Balozi wa Sweden nchini kufuatia Mkurugenzi wetu, Maxence Melo kutunukiwa Tuzo ya Kimataifa ya Uhuru wa Vyombo vya Habari
POLISI KUKATWA MSHAHARA ILI KUMLIPA WALIYEMVUNJA MGUU KWA KIPIGO

> Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Alli Hapi ameliagiza Jeshi la polisi kuwakata mshahara kiasi cha Tsh. milioni 1 askari wake 10 waliohusika kumvunja mguu Maiman Mwakajenge

> Inaelezwa kuwa walimshambulia kwa kipigo wakidai kuwa amewatukana

Soma - https://jamii.app/MakatoMshaharaPolisi