JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
SIKU 7 ZATOLEWA KATIKA UBORESHAJI WA DAFTARI LA WAPIGA KURA

> Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi amewataka wananchi wa Mikoa ya Kilimanjaro na Arusha, kutumia siku 7 ili kujiandikisha na wasitarajie muda zaidi kuongezwa

> Uboreshaji wa Daftari hilo utaanza Julai 18, 2019 katika mikoa hiyo na baadaye katika mikoa mingine

Soma - https://jamii.app/BoreshoDaftariKura
VIONGOZI WALIOMPIGA MSHIRIKI ‘U-MISS’ WAFUNGIWA

- BASATA imeisimamisha Kampuni ya Makumbusho Entertaintment na viongozi wake kujishughulisha na shughuli za sanaa na burudani

- Walimpiga mshiriki wa ‘Miss Shinyanga’ alipokuwa akidai nauli

Zaidi, soma https://jamii.app/KampuniYampigaMissYafungiwa
CAMEROON YAMFUKUZA KOCHA BAADA YA KUFANYA VIBAYA AFCON

- Kocha wa Cameroon, Clarence Seedorf na Msaidizi wake, Patrick Kluivert wamefutwa kazi baada ya timu hiyo kutolewa katika hatua ya 16 bora na kushindwa kutetea taji la michuano ya Africa Cup of Nations (#AFCON2019)
RAIS MAGUFULI ASISITIZA BEI ELEKEZI YA PAMBA NI TSH. 1,200

> Rais amesisitiza msimamo wa Serikali kuwa bei elekezi ya kununua zao la pamba ni Tsh. 1,200 kwa kilo na anayetaka kutoa bei tofauti na hiyo alipe bei ya juu zaidi lakini siyo chini ya bei elekezi iliyotangazwa na Serikali Mei 2, 2019

Soma - https://jamii.app/RaisBeiPamba
AKAMATWA KWA TUHUMA ZA KUBAKA NA KULAWITI WATOTO 5

> Jeshi la Polisi Kilimanjaro, linamshikilia Yahya Idd kwa tuhuma za kubaka na kulawiti watoto 5, wanaosoma darasa la tatu katika shule ya Msingi Chemchem

> Uchunguzi wa awali, umeonesha watoto hao kubakwa, huku mmoja akiwa amelawatiwa

Soma - https://jamii.app/AbakaKulawitiWatoto5
MALAYSIA: WABUNGE WAUNGA MKONO KUPUNGUZA UMRI WA KUPIGA KURA

- Bunge jana limeunga mkono kupunguza umri wa kupiga kura kutoka miaka 21 hadi 18

- Mabadiliko hayo yanabidi kupitishwa katika baraza la seneti la nchi hiyo kabla ya kuwa sheria

Zaidi, soma https://jamii.app/MalaysiaUmriKura
Kwa hisani ya Gazeti la The Citizen kuhusu tuzo ya Maxence Melo wa JamiiForums aliyotunikiwa na ‘The Committee to Protect Journalists (CPJ)’
Taasisi za Twaweza na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu za Tanzania; MLDI ya Uingereza na Mtandao wa Waandishi wa Habari za Uchunguzi Duniani (Global Investigative Journalism Network -
GIJN) walivyoandika kuhusiana na tuzo aliyopewa Mkurugenzi wetu, Maxence Melo
KIZIMBANI KWA KUJIFANYA MAAFISA WA TAKUKURU NA KUOMBA RUSHWA

- Ni Mkuu wa kitengo cha mauzo Hoteli ya Ramada, William Mgatta(36) na Mohammed Abdallah(25) na Daniel Ileme(35)

- Inadaiwa waliomba rushwa ya Tsh. Milioni 300 kwa Francis Matunda

Zaidi, soma https://jamii.app/RushwaKizimbaniTAKUKURU
URSULA VON DER LEYEN ACHAGULIWA KUWA KIONGOZI UMOJA WA ULAYA

> Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani amechaguliwa kuwa Rais wa Umoja wa Ulaya na Bunge la Ulaya limethibitisha uteuzi wake na hivyo kuwa mwanamke wa kwanza kuongoza taasisi hiyo kubwa

> Alipata kura 374 ambazo ni zaidi ya nusu ya wajumbe wa baraza la Umoja wa Ulaya

Soma - https://jamii.app/EUPresdElection
RAIA WA MISRI KIZIMBANI KWA KUSAFIRISHA ALMASI BILA KIBALI

> Hany Ahmed (27) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na shtaka la kutorosha madini aina ya Almasi yenye thamani ya zaidi ya Tsh. Milioni 12

> Alikamatwa Julai 10, katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere akisafirisha madini hayo bila ya kuwa na kibali

Soma - https://jamii.app/MisriUsafiriMadini
MCHUNGAJI ATUHUMIWA KUMBAKA MTOTO WAKE NA KUMPA UJAUZITO

> Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi limemtia mbaroni Mchungaji Boaz Yohane (56) wa Kanisa la FPCT kwa tuhuma za kumbaka mtoto wake (17) anayesoma kidato cha kwanza na kumpa mimba

Soma - https://jamii.app/MchAbakaMtotoMimba
DODOMA: AFISA ELIMU WA CHAMWINO ASIMAMISHWA KAZI KUPISHA UCHUNGIZI

- Mwalimu David Mwamalasa amesimamishwa kazi na Serikali kwa muda wa wiki mbili kupisha uchunguzi dhidi yake wa matumizi mabaya ya fedha kiasi cha Tsh. Milioni 259

Zaidi, soma https://jamii.app/AfisaElimuChamwinoAsimamishwa
Pongezi toka kwa Balozi wa Uingereza nchini, Sarah Cooke na Balozi wa Canada nchini, Pamela O’Donnell kwenda kwa Mkurugenzi wa JamiiForums, Maxence Melo kwa kutangazwa mshindi wa Tuzo toka The Committee to Protect Journalists
TMDA YAONYA JUU YA UWEPO WA DAWA BANDIA SOKONI

- Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) imegundua uwepo wa dawa bandia aina ya ‘Gentrisone 10g cream’

- Inafanana na dawa halisi ila dawa halisi haijawahi kuwa na namba ya toleo GNTRO X030 kama ilivyo kwenye dawa hiyo bandia

Zaidi, soma https://jamii.app/GentrisoneBandiaTZ
KENYA: MUME AMNYOFOA MDOMO MKE WAKE

> Jackline Kerubo (39) mkazi wa Tanga Kona anauguza majeraha baaada ya mume wake kumnyofoa mdomo na sikio kwa kumtafuna kwa meno kufuatia ugomvi baina yao

> Jackline alitaka kwenda kuchuma mboga katika shamba la jirani yake lakini mume wake alimkataza na ndipo ulipozuka ugomvi kati yao

Soma - https://jamii.app/MeAtoaMdomoKe