JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
BURUNDI: KIONGOZI WA ‘IMBONERAKURE’ APEWA UONGOZI SHIRIKA LA HABARI LA TAIFA

> Imbonerakure ni kikundi cha vijana cha chama tawala, CNDD-FDD wanaotuhumiwa kwa mauaji, ubakaji kwa Wapinzani hususani mwaka 2015 wakati wa jaribio la mapinduzi

Soma https://jamii.app/NshimirimanaHeadRTNB
#JFLeo
HALIMA MDEE AKAMATWA NA JESHI LA POLISI AKIWA BUKOBA

- Jeshi la Polisi limezingira ukumbi wa kikao cha Semina ya kuwajengea Uwezo BAWACHA, na kumkamata Mbunge wa Kawe

- Aidha, jana akiwa Simiyu, Jeshi la Polisi lilizuia kikao chao cha ndani

Soma https://jamii.app/MdeeAkamatwaBukoba
#AFCON2019: Dakika 90 za Mchezo wa nusu fainali kati ya #Senegal 🇸🇳 na #Tusinia 🇹🇳 zimemalizika kwa timu hizo kutoshana nguvu kwa kutofungana

- Mchezo huo unaenda katika dakika 30 za nyongeza na timu hizo zikitoka suluhu tena, mshindi atapatikana kwa penati
TENNIS: NOVAK DJOKOVIC ASHINDA TAJI LA WIMBLEDON DHIDI YA ROGER FEDERER

- Amefanikiwa kutetea taji hilo kwa kumfunga Federer seti 7-6, 1-6, 7-6, 4-6, 7-6 katika fainali iliyoweka historia ya kuchezwa kwa muda mrefu

- Hili ni taji lake la 5 la Wimbledon
#AFCON2019: Timu ya Taifa ya #Senegal 🇸🇳 imefanikiwa kutinga fainali ya michuano hiyo baada ya kuifunga timu ya Taifa ya #Tunisia 🇹🇳 goli 1-0

- Senegal inasubiri kucheza fainali na mshindi wa mechi kati ya #Algeria 🇩🇿 na #Nigeria 🇳🇬 itakayoaanza saa nne usiku huu
#AFCON2019: Timu ya Taifa ya #Algeria🇩🇿 imefanikiwa kufuzu kucheza fainali ya michuano hiyo baada ya kuifunga timu ya Taifa ya #Nigeria🇳🇬 goli 2-1 katika mchezo wa nusu fainali

- Algeria itakutana na #Senegal🇸🇳 katika fainali ya michuano hiyo mnamo Julai 19, 2019

#JFLeo #ALGNGA
SAKATA LA MUSIBA: WAZEE NDANI YA CCM WACHEFUKWA

> Mzee Makamba, Kinana waandika waraka mzito kwa niaba ya Wazee

> Wakerwa na tabia yake kuwachafua watu bila kuchukuliwa hatua

> Wadai anatumiwa na watu wenye uwezo wa kumlinda

Soma zaidi > https://jamii.app/WarakaWazeeCCM
KAHAMA: KAKA AMUUA DADA YAKE BAADA YA KUMKUTA NA MPENZI NYUMBANI KWAO

Daudi Bundala amemuua Suzana Bundala (21) kwa kumpiga na kitu kizito kichwani baada ya kumkuta amelala na mpenzi wake nyumbani kwao

> Mtuhumiwa baada ya kutekeleza mauaji hayo alikimbia na juhudi za kumtafuta na kumkamata zinaendelea

Soma - https://jamii.app/KakaAuaDadaMpnz
GEITA: RAIS MAGUFULI KUZINDUA NYUMBA ZAIDI YA 114 ZA POLISI

> Tukio litafanyika leo ktk nyumba za makazi zilizopo eneo la Magugu mkoani humo

> Rais Magufuli atazindua zaidi ya nyumba 114 zilizokwishakamilika huku matarajio ya mradi huo ni kuwa na nyumba takribani 400 kwa nchi nzima

Soma - https://jamii.app/UzinduziNyumbaPolisi
BEI YA PAMBA NYUZI SOKO LA DUNIA YAPOROMOKA, WANUNUZI WAOGOPA HASARA

> Bei ya pamba nyuzi katika soko la dunia kwa sasa ni dola 0.63 ambayo ni Tsh. 1,449 hivyo endapo watanunua pamba mbegu kwa Tsh. 1,200 watapata hasara

> Wanunuzi wameomba bei ya mkulima ishuke sokoni au Serikali iwape kinga (guarantee) ya kuwafidia hasara itakayopatikana

Soma - https://jamii.app/KushukaBeiPamba
SERIKALI: TUNAENDELEA KUTAFUTA MASOKO YA TUMBAKU

- Imesema inaendelea kutafuta masoko ili kuwawezesha Wakulima kuzalisha kwa wingi na kuinua kipato

- Imebainisha kuwa imeshafanya mazungumzo na nchi mbalimbali zikiwemo Vietnam na Misri

Zaidi, soma https://jamii.app/SokoTumbakuLatafutwa
KENYA: POLISI AJIUA AKIDAIWA ALIKUWA NA UGOMVI NA MKEWE

- Polisi wa Kituo cha Kizurini huko Kaloleni, Kaunti ya Kilifi, Kelvin Kipkemoi amejiua jana kwa kujipiga risasi

- Amejiua majira ya saa 11 alfajiri baada ya kutoka lindoni

Zaidi, soma https://jamii.app/PolisiAjiuaKilifi
MAREKANI YAZINDUA KAMPENI YA UKAGUZI WA WAHAMIAJI HOLELA

> Idara ya forodha na uhamiaji ya Marekani imezindua ukaguzi wa kushtukiza unaowalenga wahamiaji 2,000 wasio na vibali nchini humo

> Operesheni hiyo itakayofanyika katika miji mikubwa ikiwemo Los Angeles, New York, Chicago na Houston

Soma - https://jamii.app/USMigrantsInspection
KAGERA: POLISI YAENDELEA KUMNG’ANG’ANIA HALIMA MDEE

- Amenyimwa dhamana huku Mbunge wa Viti Maalumu, Conchesta Rwamulaza akisema haijaeleweka anashikiliwa kwa sababu gani

- Aidha, CHADEMA imedai Polisi wamedai wanasubiri maelekezo ya RPC

Zaidi, soma https://jamii.app/MdeeAkamatwaBukoba
AFGHANISTAN: KITUO CHA REDIO CHAFUNGWA KIKIDAI KUTISHWA NA TALIBAN

- Kituo cha redio cha Samaa kimedai kutishwa na Kamanda wa Taliban akipinga uwepo wa Watangazaji wa Kike

- Kimedai kusitisha matangazo kufuatia vitisho vya maandishi na maneno

Zaidi, soma https://jamii.app/AfghanRadioShutsDownTalibanThreats
RUKWA: TANI 2 ZA SAMAKI WENYE SUMU ZATEKETEZWA
-
> Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi na Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania wameteketeza samaki hao waliohifadhiwa kwa kutumia sumu ya kuoshea mifugo aina ya DIP ili wasiharibike

> Sumu hiyo hutumika kuulia kupe kwenye mifugo

Soma - https://jamii.app/SamakiDawaKupe
KIKOSI CHA TAIFA STARS KWA AJILI YA KUFUZU CHAN, CHATANGAZWA

- Kaimu Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Etiene Ndairagije ametaja kikosi cha Wachezaji 26 kitakachojiandaa na mchezo dhidi ya Kenya

- Stars itapambana na Kenya Julai 28, 2019 na itaingia Kambini Julai 21, 2019
KAGERA: HALIMA MDEE AACHIWA KWA DHAMANA

- Jeshi la Polisi limemuachia Mbunge huyo wa Kawe aliyeshikiliwa tangu jana baada ya kudhaminiwa na Watu wawili

- Ametakiwa kuripoti Kituoni hapo baada ya mwezi mmoja au muda wowote atakapohitajika

Zaidi, soma https://jamii.app/MdeeAkamatwaBukoba
BURUNDI: WANANCHI WAFUNGUA KESI DHIDI YA SERIKALI

> Raia 19 wamefungua kesi katika Mahakama ya Afrika Mashariki dhidi ya Serikali yao kupinga vitendo vya unyanyasaji wa haki za binadamu unaoendelea Nchini humo

> Ni baada ya Serikali yao kutaifisha Ardhi na Nyumba zao zimetaifishwa walipopinga Rais Pierre Nkurunzinza kujiongezea muda wa madaraka mwaka jana

Soma - https://jamii.app/RaiakesiVsSerikali
MBEYA: MBARONI KWA KUKUTWA NA LAINI 141 ZA SIMU

- Ally Mwakila (32), amekutwa na laini za Halotel 13, laini za Tigo 29, laini moja ya TTCL, laini 78 za VodaCom na laini 20 za Airtel

- Pia, alikutwa na simu ya Itel (3), Oking (1) na Hotwave (1)

Zaidi, soma https://jamii.app/MbaroniLaini141Simu