JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
#AFCON2019: #Senegal inakuwa timu ya kwanza kufuzu kucheza hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo baada ya kuifunga #Benin goli 1-0 katika mchezo wa robo fainali

- Senegal sasa inasubiri kucheza nusu fainali na mshindi wa mechi kati ya #Madagascar na #Tunisia
WAZIRI KABUDI: AZORY GWANDA SIO MTU PEKEE ALIYEPOTEA NA KUFA

- Akiwa katika kipindi cha ‘Focus on Africa’ cha BBC, amesema kupotea kwa Azory ni moja ya mambo ya kuumiza sana ambayo Tanzania imepitia kwani katika eneo la Rufiji si Azory pekee aliyepotea na kufa

Zaidi, soma https://jamii.app/AzoryKabudiKupoteaKufa
LEO JULAI 11: MAADHIMISHO YA SIKU YA KUPINGA RUSHWA BARANI AFRIKA

> Umoja wa Afrika unaitumia siku hii kuzikumbusha nchi Wanachama, sekta binafsi na asasi za kiraia kutumia siku hii kutathmini juhudi za kupiga vita rushwa kwa ajili ya maendeleo endelevu

Soma > https://jamii.app/RushwaAfrika
ADDIS ABABA, ETHIOPIA: WAKOSOAJI WA SERIKALI WAKAMATWA KWA KUDAIWA KUHUSIKA NA MAUAJI

> Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed aliyesifiwa kwa kuwaachia huru wafungwa wa kisiasa, ahofiwa kuwa mbioni kuirudisha nchi hiyo katika utawala wa mabavu

Zaidi, soma => https://jamii.app/WapinzaniVsSerikali-Ethiopia
CCM YAPATA MGOMBEA WA KUWANIA UBUNGE JIMBO ALILOONDOLEWA LISSU

- DC wa Ikungi mkoani Singida, Miraji Mtaturu ataiwakilisha CCM katika kinyang’anyiro cha Ubunge Jimbo la Singida Mashariki

- Ameshinda kura za maoni 396 kati ya 634 sawa na 63%

Zaidi, soma https://jamii.app/MirajiMtaturuUbunge
MWAKYEMBE: KAMA TFF IMEMFUKUZA AMUNIKE KWA KUIGA MISRI, NAO WAJIUZULU

- Amesema hana tatizo na uamuzi wa TFF iwapo wataonesha mkakati wa kutupeleka mbele kisoka

- Amewataka TFF kama waliiga, waige kikamilifu kwani Viongozi wa soka Misri walijiuzulu

Zaidi, soma https://jamii.app/MwakyembeVsTFF
NECTA YATANGAZA MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2019. UFAULU WAONGEZEKA KWA 0.74%

- Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limetangaza matokeo ya kidato cha sita ya mwaka 2019 ambapo ufaulu umeongezeka kutoka 97.58% mwaka 2018 hadi 98.32% kwa mwaka huu 2019

Zaidi, soma https://jamii.app/MatokeoKidato6-2019
MAXENCE MELO KUHOJIWA KWA DCI JUU YA MADAI YA MUSIBA KUTAKA KUULIWA

- Ni kuhusiana na tuhuma za kupanga njama za kumuua Cyprian Musiba zilizoandikwa na magazeti ya Tanzanite na Fahari Yetu

- Magazeti hayo yamedai amepanga njama hizo kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi, TCRA, Balozi Emmanuel Nchimbi na Benard Membe

Zaidi, soma https://jamii.app/MaxMeloDCIMusiba
NAHODHA WA ARSENAL AGOMA KUSAFIRI NA TIMU

- Laurent Koscielny amegoma kwenda Marekani na timu hiyo kwenye maandalizi ya msimu mpya wa Soka wa mwaka 2019/20

- Anadaiwa analazimisha kuondoka klabuni hapo na tayari ana ofa kubwa kutoka vilabu vya Bordeaux, Lyon na Rennes
WAZIRI KABUDI AKANUSHA KUTHIBITISHA KIFO CHA AZORY GWANDA

- Amesema amepokea kwa masikitiko taarifa potofu zinazochapishwa kimakosa kuwa amethibitisha kifo cha Azory

- Amesema "Mpaka sasa hakuna uthibitisho kuwa Azory yuko hai au amefariki.”

Zaidi, soma https://jamii.app/KabudiAkanaKuthibitishaKifoAzory
ALGERIA: MBUNGE WA UPINZANI ACHAGULIWA KUWA SPIKA

> Aliyechaguliwa kuwa Spika ni Slimane Chenine kiongozi wa muungano wa vyama vitatu vidogo vya Kiislamu katika Bunge

> Hii ni Mara ya kwanza katika siasa za Algeria

Zaidi, soma => https://jamii.app/ChenineSpikaAlgeria
MBUNGE FRANK MWAKAJOKA (CHADEMA) MBARONI

- Mbunge huyo wa Tunduma amekamatwa na Polisi leo ikielezwa atafikishwa Mahakamani kujibu tuhuma za kumpiga Mtu mwaka 2018

- Inadaiwa amekamatwa kwa madai ya kumpiga Afisa Mtendaji, Deus Mwampashe

Zaidi, soma https://jamii.app/MwakajokaMbaroniTuhuma2018
AFCON2019: Timu ya Taifa ya Ivory Coast imetoshana nguvu na timu ya Taifa ya Algeria katika dakika 90 za mchezo wa robo fainali kwa kufungana goli 1-1

- Timu hizo zinaenda katika dakika 30 za nyongeza na zikitoka suluhu mshindi atatafutwa kwa mikwaju ya penati
DAR: WATU 7 WATUHUMIWA WA UJAMBAZI WAKAMATWA

- Walivunja maduka matatu na kuiba bidhaa mbalimbali, fedha na bajaji mbili huko Ukonga

- Polisi imesema Watuhumiwa hao walikuwa wakitumia gari aina ya Toyota Harrier nyeusi yenye namba T 666 DJG

Zaidi, soma https://jamii.app/Majambazi7Mbaroni-DarJul2019
AFCON2019: Algeria imefuzu kucheza nusu fainali baada ya kuiondosha Ivory Coast kwa penati 4-3

- Mchezo huo umeamuliwa kwa penati baada ya timu hizo kutoka sare ya goli 1-1 ndani ya dakika 120

- Algeria itakutana na Nigeria Julai 14, 2019 katika nusu fainali
TFF IMEMCHAGUA KOCHA WA AZAM KUKAIMU UKOCHA WA TAIFA STARS

- Ndayiragije Etienne anakaimu ukocha na ataiongoza Stars kufuzu CHAN

- Kocha wa Coastal Union, Juma Mgunda na Kocha Msaidizi wa Polisi Tanzania, Suleiman Matola wapo benchi la ufundi

Zaidi, soma https://jamii.app/NdiyaragijeKaimuStars
AFCON2019: Timu ya Taifa ya Tunisia 🇹🇳 imefanikiwa kufuzu kucheza hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo baada ya kuifunga timu ya Taifa ya Madagascar 🇲🇬 goli 3-0

- Tunisia itapambana na timu ya Taifa ya Senegal 🇸🇳 katika mchezo wa nusu fainali mnamo Julai 14, 2019
MAREKANI: R. KELLY AKAMATWA TENA KWA TUHUMA ZA UNYANYASAJI WA KINGONO

> Akamatwa na Idara ya Polisi ya New York kwa tuhuma za kuwasafirisha Wanawake kwa ajili ya kuwatumikisha kingono

> Ametiwa nguvuni wakati akiwa katika Jimbo la Chicago

Soma > https://jamii.app/RKellyArrested