JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MBEYA: DAKTARI FEKI ANASWA. AKUTWA NA WAGONJWA ZAIDI YA 100

- Ni Abdallah Bushiri(42) aliyejifanya daktari wa binadamu na kufanyia watu upasuaji wakati hana taaluma hiyo

- Wagonjwa zaidi ya 100 wamekutwa nyumbani kwake wakisubiri matibabu

Zaidi, soma https://jamii.app/DaktariFekiMbeya-Juni2019
AFCON2019: Nigeria imefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Guinea katika mchezo wa Kundi B na kuongoza kundi hilo ikiwa na alama 6

- Timu nyingine katika kundi hilo za Burundi na Madagascar zitakutana kesho saa kumi na moja na nusu jioni
MADEREVA BAJAJI WAGOMA KUNUNUA VITAMBULISHO VYA WAJASIRIAMALI

> Polisi Mkoani Rukwa wamefyatua mabomu ya machozi hewani ili kuwatawanya baadhi ya madereva wa bajaji wanaoendelea na mgomo wa kutoa huduma ya usafiri wakipinga kuuziwa vitambulisho vya ujasiriamali

> Wamesema wao vitambulisho haviwahusu kwani ni madereva kama walivyo madereva wengine na vyombo vyao vimesajiliwa

Soma - https://jamii.app/MgomoBajajiVitambulisho
#JFLeo
AFCON2019: Timu ya Taifa ya Uganda imetoka sare ya goli 1-1 na timu ya Taifa ya Zimbabwe katika mchezo wa kundi A

- Uganda imefikisha alama 4 ikiwa inaongoza kundi hilo huku Misri ikiwa nafasi ya pili ikiwa na alama 3 na michezo mmoja pungufu
MTUMISHI WA HIFADHI MATATANI BAADA YA KUKUTWA NA NYAMA YA NYUMBU

> Thomas Mugabo (56) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Wilaya ya Serengeti kwa kosa la kukutwa na nyama ya nyumbu vipande 231 sawa na nyumbu mzima mwenye thamani ya Tsh. 1,430,000

Soma - https://jamii.app/HujumaNyamaNyumbu
CHELSEA YAKUBALIANA NA REAL MADRID KUMNUNUA KOVACIC

- Chelsea imefikia makubaliano na Real Madrid kumsajili moja kwa moja Mchezaji wake, Mateo Kovacic

- Chelsea inatumikia kifungo cha kutosajili kwa madirisha ya usajili katika misimu miwili, ila inaweza kusajili Wachezaji walio kwa mkopo Klabuni hapo
HAI: DIWANI ADAIWA KUBAKA NA KUMPA MIMBA MWANAFUNZI

> Diwani wa Kata ya Masama Mashariki Mkoani Kilimanjaro, John Munisi(38), amefikishwa Mahakamani akidaiwa kumbaka na kumpa mimba mwanafunzi(17) kidato cha nne wa Shule ya Sekondari Marire

> Alikana mashtaka na yupo nje kwa dhamana baada ya kukidhi masharti

Soma - https://jamii.app/DiwaniUbakajiMimba
JAGUAR AFIKISHWA MAHAKAMANI, ANYIMWA DHAMANA

- Mbunge wa Starehe, Charles Njagua maarufu Jaguar amekosa dhamana huku Hakimu akisema atatoa hukumu Ijumaa

- Aidha, simu yake ya mkononi inashikiliwa na Wapelelezi ila bado haijafanyiwa uchunguzi

Zaidi, soma https://jamii.app/JaguarMahakamaniUchochezi
NGARA: WANAFAMILIA WAFARIKI BAADA YA NYUMBA KUTEKETEA KWA MOTO

> Ajali hiyo ilitokea jana na waliofariki ni Abubakary Ramadhan Sudi(41) ambaye ni Baba, Zamrat Abubakary(4), Maryam Abubakari(7) na Suzy Abubakari
(36) ambaye ni mama na alifariki akiwa anapewa matibabu hospitalini

Soma - https://jamii.app/FamiliaKifoMoto
#JFLeo
TATIZO JINGINE LAGUNDULIKA KATIKA NDEGE ZA BOEING 737 MAX

- Wakaguzi wa Marekani wamegundua tatizo linaloweza kuchelewesha ndege hiyo kurudi kutoa huduma

- Bila kutaja tatizo wamesema wakati wa majaribio wamegundua "inayowezekana kuwa hatari"

Zaidi, soma https://jamii.app/TatizoJipyaBoeingMax
NGARA, KAGERA: WALIOKUWA WAKISAFIRISHA MITIHANI WAFARIKI AJALINI

- Ni Watu 2 akiwemo Askari wa JWTZ waliokuwa wakisafirisha mitihani ya majaribio ya kidato cha 4

- Gari walimokuwemo lilipinduka katika mteremko mkali ulioko barabara ya Kumnazi

Zaidi, soma https://jamii.app/AjaliWawiliWafariki-KumnaziKGR
MAUAJI AFISA WA JESHI ETHIOPIA: WATU 39 MBARONI WAKIHUSISHWA

> Polisi nchini Ethiopia wamewakamata watu 39 kutoka chama cha Impala kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya maafisa watano wa Jeshi katika jaribio la kuipindua Serikali katika jimbo la Amhara

> Kati ya waliofariki yupo Mkuu wa majeshi na aliyekuwa Gavana wa jimbo la Amhara

Soma - https://jamii.app/Revolution39Arrested
AFCON2019: Madagascar imeibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi Burundi katika mchezo wa Kundi B

- Madagascar inafikisha alama 4 huku Kundi hilo likiongozwa na Nigeria yenye alama 6, Guinea ina alama 1 na Burundi ina alama 0 ambapo timu zote zimecheza michezo miwili
AFCON2019: Michezo inayofuata ni ya Kundi C ambapo Senegal inakutana na Algeria majira ya saa mbili kamili usiku huu

- Katika Kundi hilo hilo Kenya ‘HarambeeStars’ inakutana na Tanzania ‘TaifaStars’ majira ya saa tano kamili usiku
NIGERIA: FEDHA ZILIZOKUWA ZIMEFICHWA NA RAIS MSTAAFU ZATAIFISHWA

> Fedha hizo ni zaidi ya Dola milioni 267 (zaidi ya Tsh bilioni 600) ambazo zilifichwa na Rais San Abacha katika benki iliyopo kisiwa cha Jersey

> Zilipatikana kwa njia za rushwa wakati wa utawala wake kati ya mwaka 1993 hadi kifo chake mwaka 1998

Soma - https://jamii.app/TaifishoFedhaRais
URUSI: WAWILI WAFARIKI, SABA WAJERUHIWA KATIKA AJALI YA NDEGE

- Ni baada ya ndege kutua kwa dharura katika uwanja wa ndege katika eneo la Buryatia huko Siberia na kuwaka moto

- Waliofariki katika ndege hiyo iliyokuwa imebeba watu 48 ni rubani na fundi

Zaidi, soma https://jamii.app/TwoKilledPlaneAcc-Urusi
KOREA KASKAZINI YAITAKA KOREA KUSINI KUSITISHA MAZUNGUMZO NA MAREKANI

> Korea Kaskazini imeitaka Korea Kusini kusitisha juhudi zake za upatanishi katika mazungumzo yake na Marekani

> Rais Donald Trump atakutana tena na kiongozi wa Korea Kusini, Moon Jae In mjini Seoul Jumapili baada ya mkutano wa kilele wa G20 huko Osaka Japan

Soma - https://jamii.app/NorthKoreaVsUs
AFCON2019: Mchezo kati ya timu za Taifa za Tanzania ‘Taifa Stars’ na Kenya ‘Harambee Stars’ umeenda mapumziko huku Tanzania ikiwa inaongoza kwa goli 2-1

Magoli ya Tanzania yamefungwa na Simon Msuva katika dakika ya 6 na Mbwana Samatta katika dakika ya 40 huku goli la Kenya likifungwa na Michael Olunga katika dakika ya 39
AFCON2019: Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imepoteza mchezo wake wa pili katika hatua ya makundi baada ya kukubali kufungwa goli 3-2 na timu ya Taifa ya Kenya ‘Harambee Stars’
-
Kwa matokeo yao, Algeria inaongoza Kundi C ikiwa na alama 6 huku Kenya na Senegal wakiwa wanafuata wakiwa na alama 3 kila moja, Tanzania inashika nafasi ya mwisho ikiwa na alama 0
Bunge la Tanzania jana lilipitisha Muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (No.3) wa 2019

> Muswada unagusa Sheria za Takwimu, Makampuni, Asasi za Kiraia, Vikundi vya Kijamii, Uwakala wa Usafirishaji Majini, Filamu na Michezo ya Kuigiza

Zaidi, soma - https://jamii.app/PitishoSheriaAZAKI
#UhuruWetu