JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
TRUMP AMUWEKEA KIONGOZI WA DINI WA IRAN VIKWAZO

- Ameiwekea Iran vikwazo vipya vikali ikiwemo Ofisi ya Kiongozi Mkuu wa dini, Ali Khamenei

- Iran imesema Marekani haipendi diplomasia na kuushutumu utawala wa Trump kwa kuwa na kiu ya vita

Zaidi, soma https://jamii.app/VikwazoKiongoziDini-Iran
TABORA: MKUU WA MKOA AMSIMAMISHA KAZI MENEJA WA TRA, IGUNGA

- Aggrey Mwanri amemsimamisha kazi, John Mgeni ili kupisha uchunguzi wa tuhuma za rushwa zinazomkabili

- Inadaiwa alidai Mfanyabiashara mmoja rushwa ya Tsh. Milioni 2

Zaidi, soma https://jamii.app/MenejaTRAIgunga
UGANDA YAPINGA MAHAKAMA YA EAC KUAMUA KUHUSU UKOMO WA MIAKA YA URAIS

> Serikali ya Uganda imesema Mahakama ya Afrika Mashariki iliyoko Arusha, haina mamlaka ya kusikiliza kesi kuhusu kipengele cha umri wa Rais

> Kesi hiyo ilipelekwa na wanaharakati wakitaka ibatilishe uamuzi wa Mahakama ya Katiba iliyokubaliana na Bunge kuondolewa kwa ukomo wa umri wa mtu kuwania urais mwezi Aprili 2019

Soma - https://jamii.app/UGVsEACCourt
#JFInternational
HARRY MAGUIRE AGOMBANIWA NA MANCHESTER UNITED NA MANCHESTER CITY

- Inadaiwa beki huyo wa Leicester City yupo tayari kujiunga na Man. City na 'kuitosa' Man. Utd

- Inadaiwa United ipo tayari kulipa ada ya Tsh. 234,597,076,000 lakini yeye anataka kujiunga na Man. City
IRINGA: WATUMISHI 2 WA TARURA MKOANI SONGWE WAFARIKI AJALINI

- Wengine 3 wamejeruhi katika ajali hiyo iliyotokea maeneo ya Izazi katika barabara kuu ya Iringa-Dodoma

- Gari lao limegongana na lori lililohama upande baada ya kumshinda dereva

Zaidi, soma https://jamii.app/AjaliTARURASongwe-IRN
RAIS MAGUFULI ASISITIZA MATUMIZI YA GESI KWA WANANCHI

> Ametoa wito hasa wananchi wa Dar ambao kwa siku wanatumia magunia 40 elfu ya mkaa sawa na asilimia 90 ya mkaa wote nchini kuanza kubadilika na kutumia gesi

> Hayo ameyasema leo wakati akizindua Ghala na Mitambo ya Gesi ya LPG ya Taifa Gas Tanzania Limited katika eneo la Vijibweni Kigamboni

Soma - https://jamii.app/RaisGesiVsMkaa
RAIS MAGUFULI AIKINGIA KIFUA TAIFA STARS

- Amesema kufungwa goli 2 na timu inayoongoza Afrika ambayo Wachezaji wake wote wanacheza nje si mwanzo mbaya

- Amemruhusu RC Makonda kwenda Misri na kuwaambia Stars wasikate tamaa na wajitume zaidi

Zaidi, soma https://jamii.app/MagufuliStarsMakonda
KENYA: WAFANYABIASHARA RAIA WA KIGENI WAPEWA SAA 24 KUONDOKA

> Wafanyabiashara kutoka mataifa mengine wanaofanya biashara katika jimbo la Starehe wamepewa saa 24 kuondoka la sivyo watapigwa

> Taharadhi hiyo imetolewa na Mbunge wa jimbo la Starehe, Charles Njagua maarufu kwa jina la kisanii Jaguar

Soma - https://jamii.app/FukuzoWageniKE
BALOZI WA KENYA, TANZANIA: MANENO YA MBUNGE WA KENYA SI MSIMAMO WA SERIKALI YA KENYA

- Amesema ule ni mtazamo wake na Serikali yake itachukua hatua

- Waziri Mkuu, Majaliwa amewataka Watanzania kuwa watulivu kwani Kenya na Tanzania ni marafiki

Zaidi, soma https://jamii.app/KenyaYamrukaJaguar
BUNGENI, DODOMA: Bunge la Tanzania limepitisha mapendekezo ya makadirio ya mapato na matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2019/2020 ya Tsh trilioni 33.1

> Wabunge waliopiga kura ni 380; 83 walisema hapana na 297 walipiga kura za ndio

Soma - https://jamii.app/PitishoBajetiSerikali
#JFLeo
NDUGAI: TUNA VIONGOZI WA SERIKALI WANAODIRIKI KUMDANGANYA RAIS HADHARANI

- Amesema “Kiongozi wa Serikali unapoongea mbele ya Rais, ongea ukweli Mwenyezi Mungu anaoujua“

- Akaongeza “Bahati mbaya kijana wetu huyu hajitambui, hajielewi”

Zaidi, soma https://jamii.app/NdugaiKijanaSerikaliHajitambui
UFARANSA NA UJERUMANI ZAKUMBWA NA JOTO KALI

> Idara kuu ya hali ya hewa imesema kiwango cha joto kinatarajiwa kufikia nyuzi joto 38 na kinaweza kuvunja rekodi hadi kufikia nyuzi joto 40 kwenye baadhi ya maeneo ya Ujerumani kama vile sehemu zinazouzunguzuka mji wa Frankfurt

> Waathirika wakubwa ni watoto chini ya miaka 2 na wazee wenye matatizo ya afya kama vile ya figo na moyo

Soma - https://jamii.app/OngezekoJotoUJFRN
KAMISHNA MAMLAKA YA USIMAMIZI WA BIMA TANZANIA, ATEULIWA

- Rais Magufuli amemteua Dkt. Mussa C. Juma kuwa Kamishna wa Mamlaka hiyo(TIRA) kuanzia Jana Juni 25

- Anachukua nafasi ya Dkt. Baghayo Abdallah Saqware ambaye uteuzi wake umetenguliwa

Zaidi, soma https://jamii.app/MagufuliAtenguaKamshnaTIRA
WATUMISHI 6 WASIMAMISHWA KAZI KWA TUHUMA ZA UBADHIRIFU WA FEDHA

> Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro limewasimamisha kazi watumishi sita kupisha uchunguzi wa tuhuma za ubadhirifu wa fedha pamoja na kufanya manunuzi yanayotia shaka

> Baadhi ya miradi inayotiliwa shaka ni ujenzi wa hospitali ya Wilaya hiyo pamoja na kituo cha afya Mkuyuni na Duthumi

Soma - https://jamii.app/SitishoKaziWatumishi
#JFLeo
MAREKANI: MKUU WA USALAMA WA MIPAKANI AJIUZULU

> John Sanders ametangaza kuachia ngazi baada ya shirika la Haki za Binadamu 'Human Rights Watch' kuchapisha ripoti mbaya kuhusu hali ya watoto wahamiaji 250 wanaozuiliwa katika kituo cha Clint

Soma - https://jamii.app/UzuluUsalamaMipaka
#JFLeo
KENYA: MBUNGE JAGUAR AKAMATWA NA POLISI

- Mbunge wa Jimbo la Starehe, Charles Njagua maarufu 'Jaguar' amekamatwa baada ya kuwataka Wafanyabiashara wa kigeni Jimboni kwake kufunga biashara zao na kuondoka la sivyo wataondolewa kwa nguvu

Zaidi, soma https://jamii.app/JaguarMbaroniKenya
MFANYABIASHARA KUTOKA KENYA ADAIWA KUTEKWA, JIJINI DAR

- Raphael O. Ongangi anadaiwa kutekwa Juni 24, 2019 na watu wenye silaha akielekea nyumbani kwake maeneo ya Masaki

- Alikuwa mshauri wa karibu wa Zitto Kabwe kabla ya Uchaguzi Mkuu 2015

Zaidi, soma https://jamii.app/MfanyabiasharaOngangiAtekwa-Dar
IDADI YA WARAIBU WA DAWA ZA KULEVYA YAPUNGUA

> Tanzania leo Juni 26, imeungana na mataifa mengine duniani kuadhimisha siku ya Kimataifa ya kupambana na matumizi na biashara ya dawa za kulevya

> Idadi ya waathirika katika vituo vya tiba imeongezeka kutoka wagonjwa 2,400 mwaka 2015 hadi wagonjwa 7000 mwaka 2018 na kufanya waraibu wa dawa za kulevya wanaojidunga kupungua kutoka 35% mwaka 2015 hadi 18.5% mwaka 2018

Soma - https://jamii.app/SikuDawaKulevya
#JFLeo
SERIKALI YATOA MAPENDEKEZO YA KUBADILI SHERIA KATI YA TBS NA TFDA

> Imependekeza marekebisho ya sheria ya viwango ili kuhamisha usimamizi wa masuala ya chakula na vipodozi kwa Shirika la Viwango Tanzania kutoka Mamlaka ya Chakula na Dawa

Soma - https://jamii.app/SheriaTBSnTFDA
#JFLeo
MBEYA: DAKTARI FEKI ANASWA. AKUTWA NA WAGONJWA ZAIDI YA 100

- Ni Abdallah Bushiri(42) aliyejifanya daktari wa binadamu na kufanyia watu upasuaji wakati hana taaluma hiyo

- Wagonjwa zaidi ya 100 wamekutwa nyumbani kwake wakisubiri matibabu

Zaidi, soma https://jamii.app/DaktariFekiMbeya-Juni2019