JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
INDIA YAONGEZA USHURU KWA BIDHAA ZA MAREKANI

- Imesema imeamua kuongeza ushuru kwa bidhaa 28 zinazoagizwa kutoka Marekani kuanzia jana

- Ni kutokana na Marekani kuongeza ushuru wa bidhaa za chuma na aluminium zinazoingizwa nchini humo

Zaidi, soma https://jamii.app/IndiaMarekaniUshuru
MTU MWENYE DALILI KAMA ZA EBOLA AONEKANA KENYA, MAMLAKA ZA AFYA ZACHUKUA TAHADHARI

- Dalili zimeonekana kwa Mwanamke mmoja aliyetoka Mabala, mpakani mwa Kenya na Uganda

- Amelazwa katika hospitali ya rufaa ya Kaunti ya Kericho tangu jana

Zaidi, soma https://jamii.app/SuspectedEbolaCase-KE
DR CONGO MASHARIKI: ENEO LENYE UTAJIRI WA MITI INAYOZALISHA DAWA AINA YA QUININE

> Jimbo la Kivu(Kusini na Kaskazini) linahifadhi kubwa ya miti aina ya Cinchona inayotumika kutengeneza dawa hizo

> Hata hivyo DRC ni Taifa la pili Duniani kwa vifo vya Malaria

Soma > https://jamii.app/QuinineDRC
MTAMBO WA MAJI WA RUVU JUU KUZIMWA

- Uzalishaji wa maji katika mtambo wa Ruvu Juu umesimamishwa kwa muda ili kuruhusu mafundi wa TANESCO na DAWASA kufanya maboresho

- Baadhi ya maeneo ya Jiji la Dar na maeneo ya Mlandizi na Kibaha yatakosa maji

Zaidi, soma https://jamii.app/RuvuJuuKuzimwa-DAWASA
INDIA: MFANYAMAZINGAOMBWE APOTEA MTONI AKIJARIBU KUONESHA UJUZI

- Chanchal Lahiri aliyefungwa kwa minyororo na makufuli na kisha kutumbukizwa mtoni anaofiwa kufa hapo jana

- Alitakiwa kuibuka akiwa amejifungua minyororo hiyo lakini hakuibuka na hadi jana jioni alitafutwa bila mafanikio

Zaidi, soma https://jamii.app/MfanyamazingaombweAhofiwaKufa-IND
WEMA SEPETU KWENDA MAHABUSU KWA SIKU 7

- Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu imeamuru msanii huyo kukaa mahabusu akisubiri uamuzi wa dhamana baada ya kukiuka masharti

- Mara ya mwisho shauri hilo kusikilizwa, Mahakama iliamuru Wema akamatwe

Zaidi, soma https://jamii.app/WemaSepetuMahabusuSiku7
HUAWEI KUPATA HASARA YA DOLA BILIONI 30 KWA MIAKA 2 IJAYO

> CEO wa Huawei, Ren Zhengfei amesema kampuni hiyo anailaumu Marekani kwa kupinga biashara yake

> Amesema mauzo ya nje ya bidhaa za kampuni hiyo yameshuka kwa asilimia 40 kwa mwaka huu

Soma > https://jamii.app/HuaweiLoss
MWANAFUNZI CHUO KIKUU KIU AFARIKI BAADA YA KUSHAMBULIWA NA VIBAKA

> Aliyefariki ni Anifa Mgaya mwanafunzi wa Stashahada ya Maabara katika Chuo Kukuu cha Kampala tawi la Tanzania

> Alivamiwa na vibaka waliomjeruhi kwa kisu

Zaidi, soma https://jamii.app/RIPAnifaMgaya
NIGERIA: WATU 30 WAMEFARIKI KATIKA MASHAMBULIO MATATU YA BOMU

- Watu wengine 40 wamejeruhiwa katika milipuko hiyo iliyotokea nje ya ukumbi huko Konduga, Borno

- Katika ukumbi huo Mashabiki wa mpira walikuwa wakifuatilia mechi kupitia runinga

Zaidi, soma https://jamii.app/30WauawaNigeriabomu
KIRINYAGA, KENYA: AMCHOMA MKEWE KWA KUPIKA WALI BADALA YA KANDE

> Peter Ngugi(32) anashikiliwa na kwa kumjeruhi mkewe kwa kumwagia moto

> Alimuagiza Mkewe apike 'Githeri' (Kande) lakini Mkewe alipika wali

Zaidi, soma => https://jamii.app/AmchomaMkeweKE
TAASISI ZA KIDINI NA JUMUIYA ZA KIJAMII KUFUTIWA USAJILI ZISIPO HAKIKIWA

-Serikali inafanya uhakiki wa Jumuiya na Taasisi hizo nchi nzima ambapo awamu ya 2 itafanyika Dodoma, Morogoro, Singida na Manyara kuanzia Juni 23 hadi Julai 2 mwaka huu

Zaidi, soma https://jamii.app/TaasisiZisizohakikiwaKufutwa
RIPOTI: KIWANGO CHA SILAHA ZA NYUKLIA CHAPUNGUA DUNIANI

- Kituo cha Kimataifa cha Utafiti wa Amani kimesema kiwango kimepungua kwa silaha 800 katika nchi 9 katika kipindi cha mwaka mmoja ila Mataifa yanatengeneza silaha za kisasa zaidi

Zaidi, soma https://jamii.app/SilahaNyukliaZapungua
KENYA: MWANAMKE ALIYEONESHA DALILI ZA EBOLA, HANA UGONJWA HUO

- Matokeo ya vipimo ya mgonjwa aliyedhaniwa kuwa na Ebola yameonesha hana ugonjwa huo

- Amelazwa kwenye Hospitali ya Rufaa ya Kaunti ya Kericho akiwa ameonesha dalili kama za Ebola

Zaidi, soma https://jamii.app/SuspectedEbolaCase-KE
MWENYEKITI WA BODI YA WAKURUGENZI WA REA ATENGULIWA

- Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Wakala wa Nishati Vijijini(REA), Michael Pius Nyagoga

- Aidha, amemteua Wakili Julius B. Kalolo kushika nafasi hiyo kuanzia leo

Zaidi, soma https://jamii.app/MwenyekitiBodiREAAtenguliwa
MTANDAO WA 5G WAANZA KUPATIKANA KWENYE BAADHI YA MAJIMBO YA MAREKANI

> Kampuni ya Verizon imefunga miundombinu ya mtandao wa 5G katika Majiji yafuatayo, Houston, Indianapolis, Los Angeles, Sacramento, na California

> Siku za hivi karibuni Kampuni ya Huawei ya China ilijitapa kuwa na teknolojia hiyo

Soma => https://jamii.app/5GMarekani
TUKUKURU YAKANUSHA TAARIFA ZA UPOTOSHAJI ZENYE TUHUMA DHIDI YA MAAFISA WAKE

> Taarifa hizo zinazotajwa kuwa za upotoshaji zilichapishwa katika magazeti mawili ya Fahari Yetu na Tanzanite

> TAKUKURU yasema taarifa hizo zimelenga kuidhoofisha

Soma > https://jamii.app/TAKUKURUVsMagazeti
DODOMA: WATU 29 WAJERUHIWA KATIKA AJALI YA TRENI NA LORI

- Ajali hiyo imetokea usiku wa kuamkia leo ambapo pia mabehewa matatu ya treni yalianguka

- Treni hiyo iliyokuwa inatoka Tabora kwenda Dar ilipata ajali kabla ya kuingia stesheni

Zaidi, soma https://jamii.app/AjaliTreni29Wajeruhiwa-DOM
TANZANIA KINARA WA AMANI AFRIKA MASHARIKI

- Kwa mujibu wa ripoti ya Global Peace Index(GPI), Tanzania imeshika nafasi ya 7 kwa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara

- Kwa Afrika Mashariki, Rwanda inafuata, ikifuatiwa na Uganda na kisha Kenya

Zaidi, soma https://jamii.app/TZKinaraAmaniEA
CHINA: WATU 12 WAMEFARIKI NA 134 KUJERUHIWA KATIKA TETEMEKO LA ARDHI

- Uokoaji unaendelea huko Sichuani Kusini Magharibi mwa China baada ya kutokea tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa Kipimo cha Richa 6, jana usiku

Zaidi, soma https://jamii.app/EarthquakeKills12-China
MCHEZAJI WA FC BARCELONA FRENKIE DE JONG ATEMBELEA SERENGETI

> Amepost picha kupitia Instagram akionekana ndani mbuga hiyo

> Aidha, zipo taarifa pia za Mshambuliaji, wa Chelsea, Gonzalo Higuaín kuwepo nchini akitembelea vivutio mbalimbali

Soma > https://jamii.app/FrenkieDeJongTz