JamiiForums
52.9K subscribers
34.3K photos
2.43K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
SERIKALI YAKUSUDIA KUSHUSHA UMRI WA VIJANA KUPATA HUDUMA ZA UKIMWI

> Serikali inatarajia kupeleka Muswada wa sheria Bungeni wa kushusha umri wa kuridhia vijana kupata huduma za UKIMWI bila ridhaa ya wazazi kutoka miaka 18 hadi 15 ili kupunguza wimbi la maambukizi mapya ya Virusi Vya UKIMWI(VVU)

> Kwa siku, zaidi ya watu 200 hupata maambukizi mapya ya VVU huku kati yao 80 wakiwa ni vijana wenye umri wa miaka 15 hadi 24

Soma - https://jamii.app/UmriMaambukiziVVU
MOROGORO: VIONGOZI WATATU WA BAVICHA MBARONI

- Ni Mwenyekiti wa BAVICHA, Patrick Ole Sosopi pamoja na Daniel Ngogo na mwingine ambaye jina lake halijafahamika

- Wamewakamatwa wakiwa Ifakara wakituhumiwa kufanya kampeni za nyumba kwa nyumba

Zaidi, soma https://jamii.app/MwenyekitiBavichaMbaroni
SRI LANKA YAPITISHA SHERIA YA KUZUIA MATAMSHI YA CHUKI NA HABARI ZA UONGO

- Ni ili kuimarisha usalama wa Taifa, baada ya mashambulio ya bomu Sikukuu za Pasaka

- Watakaosambaza habari za uongo kufungwa hadi miaka 5 au faini ya Tsh. 13,041,567

Zaidi, soma https://jamii.app/SheriaHabariUongo-SLNK
UJERUMANI: AFUNGWA MAISHA KWA KUUA WAGONJWA 85

- Muuguzi wa zamani, Niels Högel(42) aliwaua Wagonjwa wengi kwa kuwapa dawa ya kusimamisha mapigo ya moyo na kisha kuwaokoa

- Alikuwa akifanya hivyo ili kupata sifa kwa Wafanyakazi wenzake

Zaidi, soma https://jamii.app/MuuguziAua85-UJR
SUDAN YASIMAMISHWA KUSHIRIKI SHUGHULI ZOTE ZA AU

> Umoja wa Afrika umeisimamisha Sudan kushiriki shughuli zote za Umoja huo kufuatia hatua ya Jeshi la nchi hiyo kuwashambulia waandamanaji wanaopigania utawala wa kiraia na kuua watu wengi

> Aidha, Umoja wa Mataifa unapanga kuwaondoa wafanyakazi wake Sudan

Soma - https://jamii.app/AUBansSudan
UFARANSA: RAIS WA CAF AKAMATWA NA POLISI

- Rais wa Shirikisho la Soka Barani Afrika, Ahmad Ahmad(59) amekamatwa leo jijini Paris

- Inadaiwa kukamatwa kwake kunahusishwa na vitendo vya rushwa na utumiaji mbaya wa madaraka

Zaidi, soma https://jamii.app/RaisCAFMbaroniRushwa
SRI LANKA: Watu 28 wamefariki na zaidi ya 18,000 wameambukizwa virusi vya ugonjwa wa Dengue katika miezi mitano ya kwanza ya mwaka 2019
-
Mpaka Mei 31, jumla ya matukio 18,760 ya Dengue yaliripotiwa, idadi kubwa zaidi ikiripotiwa kutoka Wilaya ya Colombo ikiwa na kesi 4,066, Gampaha kesi 2,480 na Jaffna Kaskazini kesi 1,887
ZIMBABWE YAANZA MAZUNGUMZO YA KUONDOLEWA VIKWAZO

- Mabalozi wa nchi za Umoja wa Ulaya wamekutana na Serikali katika awamu ya kwanza ya mazungumzo

- Umoja wa Mataifa uliondoa sehemu kubwa ya vikwazo vya kiuchumi ila imekuwa haisaidii kifedha

Zaidi, soma https://jamii.app/ZimbabweMazungumzoVikwazo
TANZANIA YANG'ARA KWENYE MASHINDANO YA MISS LANDSCAPE DUNIA

> Mwakilishi wa Tanzania kwenye mashindano ya Miss Landscape ya dunia, Anitha Mlay ameibuka mshindi wa pili, huku nafasi ya kwanza ikichukuliwa na mrembo kutoka Marekani katika fainali za mashindano zilizofanyika jana, Juni 5

> Shindano hilo limeshirikisha warembo kutoka mataifa 41

Soma - https://jamii.app/TzWinsMissLandscape
CHINA YADAIWA KUZIFADHILI SERIKALI ZA KIDIKTETA

- Wabunge nchini Marekani na Watetezi wa #HakiZaBinadamu wanaishutumu China kwa kueneza mfumo wa kiimla na kuzisaidia Serikali kandamizi za kidikteta, kuwapeleleza na kuwadhibiti raia wake

Zaidi, soma https://jamii.app/ChinaSerikaliDikteta
TANZANIA KUANZA KUUZA TENA BIDHAA ZA MALIASILI MAREKANI

> Miaka mitano iliyopita, Marekani ilizuia bidhaa zinazotokana na shughuli za uwindaji kutoka Tanzania, kutokana na kile ambacho ilidai ni kutokuwa na imani na jinsi Tanzania ilivyokuwa ikiendesha jitihada za uhifadhi wa maliasili na mazingira

Soma - https://jamii.app/MauzoBidhaaMaliasili
WHO: MAAMBUKIZI MAPYA MILIONI 1 YA MAGONJWA YA ZINAA HUTOKEA KILA SIKU

- Magonjwa hayo ni pamoja na kisonono, kaswende na trichomoniasis

- Aidha, Wataalamu wanahofu magonjwa hayo kuwa sugu kiasi cha kutotibiwa na dawa zilizopo sasa

Zaidi, soma https://jamii.app/WHOMaambukiziZinaa
LUGOLA KUANZA KUKAGUA PIKIPIKI KWENYE VITUO VYA POLISI

> Waziri wa Mambo ya Ndani amesema kuanzia Juni 15 ataanza ziara katika vituo mbalimbali vya Polisi kukagua utekelezaji wa agizo lake kuhusu Jeshi hilo kuzishikilia bodaboda zenye makosa ya kofia ngumu au kupakia abiria zaidi ya watatu

Soma - https://jamii.app/LugolaUkaguzibodaboda
IKULU, DAR: RAIS MAGUFULI AKUTANA NA WAFANYABIASHARA

- Anazungumza na Wafanyabiashara wa 5 kutoka wilaya zote nchini pamoja na Wajumbe wa Baraza la Biashara la Taifa

- Lengo ni kufahamu changamoto za Wafanyabiashara na kusikiliza mawazo yao

Zaidi, soma https://jamii.app/MagufuliWafanyabiashara-Ikulu
CHINA NA URUSI ZATIA SAINI KUZUIA MATUMIZI YA FEDHA YA MAREKANI

> Rais Xi Jinping wa China ametangaza habari ya kutiwa saini mapatano ya kufutwa kwa sarafu ya dola ya Marekani katika miamala ya kibiashara ya nchi yake na Urusi na badala yake sarafu za mataifa hayo zitachukua nafasi ya dola katika mabadilishano

Soma - https://jamii.app/RussiaChinaBanDollar
KLABU YA SIMBA YAPANGA KUJITOA MICHUANO YA KAGAME CUP

> Mkurugenzi wa klabu hiyo, Crescentus Magori amedai kutokana na sababu za kubadilika kwa ratiba ya CAF, michuano ya Afcon itakuwa ngumu kwa klabu hiyo kushiriki mashindano ya Kagame Cup kwa kuwa inatarajia kwenda kuweka kambi ya mwezi mmoja nje ya nchi kujiandaa na msimu wa 2019/20

Soma - https://jamii.app/SimbaKujitoaKagameCup
#JFMichezo