JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
URUSI YAPIGA MARUFUKU UWEPO WA KANISA LA MASHAHIDI WA YEHOVA

> Mahakama ya Juu nchini Urusi imekubali ombi la Serikali kuorodhesha kanisa la Mashahidi wa Yehova kama kundi la kidini lililoharamishwa kwa madai ya kusambaza nyaraka zenye ujumbe wa kuchochea chuki dhidi ya makundi mengine

Soma - https://jamii.app/BanJehovahWitnesses
KENYA: AMSHONA MWANAYE MDOMO KWA KUTOFANYA VIZURI SHULENI

- Mwanamke mmoja kutoka Naivasha, Kaunti ya Nakuru amemshona mdomo mtoto wake wa kiume wa darasa la 5

- Inadaiwa kuwa Mwanamke huyo aliumizwa sana na maendeleo ya mtoto wake shuleni

Zaidi, soma https://jamii.app/AmshonaMdomoKufeli-KE
MTOTO AMUUA BABA YAKE WAKATI AKIMUOKOA MAMA YAKE ASISHAMBULIWE

> Edison Mwananjela (18) mkazi wa Mkoani Rukwa anadaiwa kumuua baba yake mzazi, Galus Mwananjela (42) kwa kumshambulia na mpini wa jembe kichwani na kumvunja mikono kwa madai ya kuchoshwa na tabia ya baba yake ya kumpiga mara kwa mara mama yake

Soma - https://jamii.app/KijanaAuaBaba
KENYA KUPIGA MARUFUKU MATUMIZI YA CHUPA ZA PLASTIKI

> Rais Uhuru Kenyatta jana alitangaza kupiga marufuku ya matumizi ya chupa za plastiki nchini humo kuanzia Juni 5, 2020 na marufuku hiyo itatekelezwa katika maeneo yenye ulinzi kama vile Mbuga za Kitaifa, fukwe za bahari, misituni na maeneo ya uhifadhi

Soma - https://jamii.app/BanPlastickBottles
TETESI ZA SOKA: Inadaiwa Klabu ya Brighton ya ligi Kuu England inaongoza mbio za kumuwania Mshambuliaji wa Tanzania, Mbwana Samatta

- Aidha, Samatta mwenye thamani ya Paundi Milioni 12(Tsh. 34,930,999,680), pia anawaniwa na Aston Villa, Watford, Leicester na Burnley
SUDAN: UPINZANI WAKATAA MAZUNGUMZO. VIFO VYADAIWA KUFIKA 108

- Umekataa mazungumzo mapya na Jeshi baada ya jana Jeshi kupendekeza

- Aidha, Serikali imesema watu 46 wameuawa kwenye vurugu huku Madaktari wanaouhusiana na Upinzani wakidai ni 108

Zaidi, soma https://jamii.app/108KilledSudanProtest
CAF YAFUTA MATOKEO YA FAINALI YA PILI YA MABINGWA WA AFRIKA

> Shirikisho la Soka Barani Afrika limeyafuta matokeo yaliyoipa Ubingwa Esperance ya Tunisia dhidi ya Wydad Casablanca ya Morocco

> Mechi hiyo itarudiwa baada ya mashindano ya AFCON Afrika Kusini, Juni 30
TRA YAANZISHA MSAKO WA KODI, WASIOTOA NA KUDAI RISITI KUPIGWA FAINI

> Mamlaka ya Mapato Tanzania, Mkoa wa Kodi Kariakoo umetoa tangazo la kukamata mizigo au bidhaa ambazo hazitakuwa na risiti halali ambapo kwa wasiotoa risiti watatozwa faini ya Tsh. milioni 3 hadi milioni 4.5 na wale wasiodai risiti watatozwa faini ya Tsh. milioni 1.5 kwa kila kosa

Soma - https://jamii.app/MsakoFainiRisiti
SERIKALI YAKUSUDIA KUSHUSHA UMRI WA VIJANA KUPATA HUDUMA ZA UKIMWI

> Serikali inatarajia kupeleka Muswada wa sheria Bungeni wa kushusha umri wa kuridhia vijana kupata huduma za UKIMWI bila ridhaa ya wazazi kutoka miaka 18 hadi 15 ili kupunguza wimbi la maambukizi mapya ya Virusi Vya UKIMWI(VVU)

> Kwa siku, zaidi ya watu 200 hupata maambukizi mapya ya VVU huku kati yao 80 wakiwa ni vijana wenye umri wa miaka 15 hadi 24

Soma - https://jamii.app/UmriMaambukiziVVU
MOROGORO: VIONGOZI WATATU WA BAVICHA MBARONI

- Ni Mwenyekiti wa BAVICHA, Patrick Ole Sosopi pamoja na Daniel Ngogo na mwingine ambaye jina lake halijafahamika

- Wamewakamatwa wakiwa Ifakara wakituhumiwa kufanya kampeni za nyumba kwa nyumba

Zaidi, soma https://jamii.app/MwenyekitiBavichaMbaroni
SRI LANKA YAPITISHA SHERIA YA KUZUIA MATAMSHI YA CHUKI NA HABARI ZA UONGO

- Ni ili kuimarisha usalama wa Taifa, baada ya mashambulio ya bomu Sikukuu za Pasaka

- Watakaosambaza habari za uongo kufungwa hadi miaka 5 au faini ya Tsh. 13,041,567

Zaidi, soma https://jamii.app/SheriaHabariUongo-SLNK
UJERUMANI: AFUNGWA MAISHA KWA KUUA WAGONJWA 85

- Muuguzi wa zamani, Niels Högel(42) aliwaua Wagonjwa wengi kwa kuwapa dawa ya kusimamisha mapigo ya moyo na kisha kuwaokoa

- Alikuwa akifanya hivyo ili kupata sifa kwa Wafanyakazi wenzake

Zaidi, soma https://jamii.app/MuuguziAua85-UJR
SUDAN YASIMAMISHWA KUSHIRIKI SHUGHULI ZOTE ZA AU

> Umoja wa Afrika umeisimamisha Sudan kushiriki shughuli zote za Umoja huo kufuatia hatua ya Jeshi la nchi hiyo kuwashambulia waandamanaji wanaopigania utawala wa kiraia na kuua watu wengi

> Aidha, Umoja wa Mataifa unapanga kuwaondoa wafanyakazi wake Sudan

Soma - https://jamii.app/AUBansSudan
UFARANSA: RAIS WA CAF AKAMATWA NA POLISI

- Rais wa Shirikisho la Soka Barani Afrika, Ahmad Ahmad(59) amekamatwa leo jijini Paris

- Inadaiwa kukamatwa kwake kunahusishwa na vitendo vya rushwa na utumiaji mbaya wa madaraka

Zaidi, soma https://jamii.app/RaisCAFMbaroniRushwa
SRI LANKA: Watu 28 wamefariki na zaidi ya 18,000 wameambukizwa virusi vya ugonjwa wa Dengue katika miezi mitano ya kwanza ya mwaka 2019
-
Mpaka Mei 31, jumla ya matukio 18,760 ya Dengue yaliripotiwa, idadi kubwa zaidi ikiripotiwa kutoka Wilaya ya Colombo ikiwa na kesi 4,066, Gampaha kesi 2,480 na Jaffna Kaskazini kesi 1,887
ZIMBABWE YAANZA MAZUNGUMZO YA KUONDOLEWA VIKWAZO

- Mabalozi wa nchi za Umoja wa Ulaya wamekutana na Serikali katika awamu ya kwanza ya mazungumzo

- Umoja wa Mataifa uliondoa sehemu kubwa ya vikwazo vya kiuchumi ila imekuwa haisaidii kifedha

Zaidi, soma https://jamii.app/ZimbabweMazungumzoVikwazo
TANZANIA YANG'ARA KWENYE MASHINDANO YA MISS LANDSCAPE DUNIA

> Mwakilishi wa Tanzania kwenye mashindano ya Miss Landscape ya dunia, Anitha Mlay ameibuka mshindi wa pili, huku nafasi ya kwanza ikichukuliwa na mrembo kutoka Marekani katika fainali za mashindano zilizofanyika jana, Juni 5

> Shindano hilo limeshirikisha warembo kutoka mataifa 41

Soma - https://jamii.app/TzWinsMissLandscape
CHINA YADAIWA KUZIFADHILI SERIKALI ZA KIDIKTETA

- Wabunge nchini Marekani na Watetezi wa #HakiZaBinadamu wanaishutumu China kwa kueneza mfumo wa kiimla na kuzisaidia Serikali kandamizi za kidikteta, kuwapeleleza na kuwadhibiti raia wake

Zaidi, soma https://jamii.app/ChinaSerikaliDikteta
TANZANIA KUANZA KUUZA TENA BIDHAA ZA MALIASILI MAREKANI

> Miaka mitano iliyopita, Marekani ilizuia bidhaa zinazotokana na shughuli za uwindaji kutoka Tanzania, kutokana na kile ambacho ilidai ni kutokuwa na imani na jinsi Tanzania ilivyokuwa ikiendesha jitihada za uhifadhi wa maliasili na mazingira

Soma - https://jamii.app/MauzoBidhaaMaliasili