JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
BEI KIKOMO ZA MAFUTA KWA MWEZI JUNI 2019 ZAONGEZEKA

- Ni bei za mafuta kwa jumla na rejareja yanayoingia nchini kupitia bandari za Dar, Tanga na Mtwara

- Ni kutokana na mabadiliko ya bei ktk soko la ndani na ongezeko la bei ktk soko la dunia

Zaidi, soma https://jamii.app/BeiMafutaJuni-2019
OMAN: Katika kusheherekea sikukuu ya Idd El Fitr, Serikali imefanywa uamuzi wa kuwaachia huru wafungwa 478 ambao kati ya hao 240 ni raia wa kigeni

> Wamesamehewa vifungo vyao na kuachiliwa huru baada ya hati ya msamaha iliyosainiwa na Sultani Kabus bin Said kusambazwa

#JFInternational
SUDAN: WAPINZANI WAKATAA UCHAGUZI ULIOITISHWA NA JESHI

- Viongozi wameitisha maandamano mapya na kukataa mpango wa uchaguzi mpya

- Chama cha Wanataaluma kimesema sio Wanajeshi wala washirika wake, watakaomua mustakabali wa watu wa Sudan

Zaidi, soma https://jamii.app/MilitaryCallsElection
MWEZI WAANDAMA, SIKUKUU YA EID AL FITR KUSHEREHEKEWA KESHO

- Mufti wa Tanzania, Sheikh Mkuu Abubakar Zubeir ametangaza kuwa mwezi umeonekana katika maeneo mbalimbali nchini

- Swala ya Idd Kitaifa itaswaliwa Tanga na kuongozwa na Mufti Zubeir

Zaidi, soma https://jamii.app/MweziWaandamaEidKesho
MWISHO WA MATUMIZI YA PASIPOTI ZA ZAMANI NI JANUARI 2020

> Msemaji Idara ya Uhamiaji, Ally Mtanda amewataka watu wote wanaotarajia kusafiri safari za nje ya nchi hivi karibuni kuhakikisha wanabadilisha pasipoti zao hadi kufikia Julai 2019

> Kisheria pasipoti inatakiwa kuwa hai angalau miezi 6 ili iweze kuombewa visa

Soma - https://jamii.app/PassportRenewal
Bodi, Menejimenti na Wafanyakazi wa Jamiiforums wanapenda kuwatakia Waislamu wote Kheri, Amani na Baraka katika sikukuu ya Eid al-Fitr baada ya Kumaliza mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani

#JFLeo #EidMubarak
MBEYA: MBARONI WAKIDAIWA KUMUUA MFANYABIASHARA WA UFUTA

- Watu 2 wa familia moja, wanashikiliwa na Polisi wakidaiwa kumuua Oswald Malambo na kumpora Tsh. Milioni 55

- Inadaiwa waliweka sumu kwenye kinywaji cha Oswald wakiwa wote baa

Zaidi, soma https://jamii.app/MuuzaUfutaAuawa-Mbeya
DANIEL STURRIDGE NA ALBERTO MORENO KUONDOKA LIVERPOOL

- Wanaondoka majira haya ya joto baada ya mikataba yao kumalizika

- Sturridge(29) amefunga magoli 67 katika mechi 160 tangu alipojiunga Januari 2013 huku Moreno(26) akicheza mechi 141 tangu ajiunge Agosti 2014
BENI: KUNDI LA WAASI LA ADF LAUA WATU 12

- Kundi la The Allied Democratic Forces(ADF) limewaua watu hao katika mji wa Beni Mashariki mwa nchi ya DR Congo

- Waasia hao pia walivamia kambi ya Jeshi ya Rwangoma na kuua Wanajeshi wawili

Zaidi, soma https://jamii.app/ADFLaua12Beni-DRC
SERIKALI YATOA KANUNI MPYA KWA WANUNUZI NA WAUZAJI WA MKAA

> Wanunuaji wa mkaa na samani wanatakiwa wawe na risiti za bidhaa kutoka kwenye maeneo ya mauzo yaliyosajiliwa

> Adhabu kwa atakayezikiuka ni faini ya Tsh 500,000 hadi Tsh milioni 12 au kifungo kati ya miezi 6 hadi miaka 5

Soma - https://jamii.app/KanuniBidhaaMisitu
VITUO VYA HABARI VYAPIGWA FAINI KWA MADAI YA KURUSHA HABARI ZA UONGO

> Kamati ya Maudhui ya TCRA imetoa adhabu ya kulipa faini kwa kusambaza na kutangaza habari zisizo na ukweli

> Vituo hivyo ni: Azam Media Ltd na Gilly Bonny Online TV

Soma - https://jamii.app/FainiVituoHabari
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
RC wa Iringa, Ally Hapi akizungumzia Tamko la Wanahabari waliompa siku 7 kuomba radhi kutokana na kauli yake ya kugawa Vitambulisho vya Wafanyabiashara Wadogo kwa Wanahabari

Anasema, “Nikajiuliza Mkuu wa Mkoa unampa siku 7, unaelewa maana ya Mkuu wa mkoa? Nilipoona nikacheka. Mimi ni mwakilishi wa Rais.”
WANAFUNZI WAZAMA ZIWANI WAKITALII, WATATU WAPOTEZA MAISHA

> Wanafunzi 3 kati ya 5 wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Makurugusi, Wilayani Chato wamepoteza maisha baada ya mtumbwi waliokuwa wakiutumia kufanya utalii wa ndani kuzama Ziwa Victoria jana asubuhi

Soma - https://jamii.app/WanafunziVifoUtalii
UINGEREZA: IDADI YA WANAOUGUA MAGONJWA YA ZINAA YAONGEZEKA

> Takwimu zinaonesha mwaka 2018 kulikuwa na wagonjwa 447,694 waliobainika kwa mara ya kwanza na maradhi hayo, kiwango hicho kikiwa ni sawa na ongezeko la 5% juu ya idadi ya mwaka 2017 cha watu 422,147

> Makundi yaliyomo hatarini ni vijana pamoja na wanaume wanaofanya ngono na wanaume wenzao

Soma - https://jamii.app/STDsPatientsUK
KIZIMBANI KWA KUCHAPISHA MAUDHUI ‘YOUTUBE’ BILA KIBALI

- Charles Kombe(24), John Chuwa(28), Amos Warema(27) na Raymond Mkoroka(30) wamefikishwa katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar

- Wanatuhiwa kuchapisha maudhui hayo bila kibali cha TCRA

Zaidi, soma https://jamii.app/KizimbaniMaudhuiYouTubeKibali
CHRISTIAN ERIKSEN ATAMANI KUONDOKA TOTTENHAM HOTSPURS

- Mchezaji huyo anayehusishwa kujiunga na Real Madrid amesema anatamani kujaribu kitu kipya

- Kiungo huyo aliyebakiza mwaka 1 kwenye mkataba wake amesema kama ni kuondoka Spurs basi itakuwa kwa ajili ya timu kubwa
KENYA: WATOTO WAMUUA MPENZI WA MAMA YAO BAADA YA KUMKUTA NYUMBANI

> Ndugu wawili katika kijiji cha Kilungu, kaunti ya Makueni wamekamatwa na Polisi baada ya kumshambulia kwa panga na kumuua Onesmus Kivuna aliyedaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mama yao walipomkuta kwenye nyumba ya mama yao jana majira ya saa nne usiku

Soma - https://jamii.app/WatotoMpenziMama
SHINYANGA: MBARONI KWA KUJIFANYA AFISA USALAMA NA KUTAPELI

- Mrisho Zabroni(37) na Mgema Patrick(25) wamekamatwa Wilayani Kahama kwa kutaka kutapeli

- Walitaka kumtapeli Abdallah Moro ambaye ghala lake la kuhifadhia bidhaa lilifungwa na TFDA

Zaidi, soma https://jamii.app/AfisaTISSFekiMbaroni
UINGEREZA: DUNIA YAADHIMISHA MIAKA 75 YA D-DAY

> Rais Donald Trump ameungana leo na viongozi wa nchi 16 katika kuadhimisha miaka 75 tangu kuanza kwa operesheni ya kijeshi mwaka 1944 iliyoikomboa Ulaya kutoka mikononi mwa Wanazi wa Ujerumani, maarufu kama D-Day

> Wanazi wa Ujerumani walikuwa wameyakalia maeneo makubwa ya Ulaya katika vita vikuu vya pili

Soma - https://jamii.app/75YrsD-Day