JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MWANZA: WANAFUNZI 103 WA SHULE ZA MSINGI WAPATA MIMBA NDANI YA MWAKA

> Utoro umetajwa kuwa moja ya sababu ya kuzorotesha elimu jijini Mwanza ambapo kwa mwaka 2017/18, wanafunzi 2,646 wa shule za msingi waliacha masomo kwasababu mbalimbali wakiwamo 103 waliopata mimba

> Wengine waliacha shule kwasababu ya magonjwa, utoro, vifo na utovu wa nidhamu

Soma - https://jamii.app/MimbaUtoroElimuMWZ
ALIYEFUKUZWA UHISPANIA NA REAL MADRID, ATEULIWA KUINOA SEVILLA

- Julen Lopetegui(52) amesaini mkataba wa miaka 3 kuinoa Klabu ya Sevilla ya Uhispania

- Alifukuzwa kuinoa timu ya Taifa ya Uhispania siku 2 kabla ya Kombe la Dunia 2018 kuanza

Zaidi, soma https://jamii.app/LopeteguiKuinoaSevilla
MWALIMU MBARONI KWA KUKUTWA NA SILAHA(AK-47) DARASANI

> Mwalimu wa shule ya Msingi Naan, Solomon Letato (30) mkazi wa Kijiji cha Enguserosambu, Loliondo anashikiliwa na Polisi akihusishwa na matukio ya ujambazi wa kutumia silaha baada ya kukutwa darasani na silaha ya kivita aina ya AK-47 ikiwa na risasi 5

> Pia anatuhumiwa kujihusisha na biashara haramu ya nyara za Serikali yakiwemo meno ya tembo na pembe za Faru

Soma - https://jamii.app/MwlSilahaAK47
TARIME, MARA: KIONGOZI WA MWENGE AKATAA KUZINDUA MIRADI

- Mzee Mkongea amesema mradi wa maji wa Mtaa wa Gamasara, haujakidhi vigezo kwani nondo hazijapimwa

- Mradi wa daraja katika Kijiji cha Kiterere, una ukosefu wa alama za barabarani

Zaidi, soma https://jamii.app/MwengeKutozinduaMiradi-TRM
HESLB YATOA MWONGOZO WA UTOAJI MIKOPO KWA MWAKA 2019/20

- Imetangaza mwongozo huo ikiwa ni maandalizi ya kukaribisha maombi ya mikopo

- Itaanza kupokea maombi ya mikopo kwa mwaka wa masomo 2019/20 kuanzia Juni 15 hadi Agosti 15, 2019

Zaidi, soma https://jamii.app/HeslbMikopo2019-20
JAY-Z ATANGAZWA KUWA RAPA BILIONEA WA KWANZA DUNIANI

> Jay-Z ametangazwa rasmi na Jarida la Forbes kuwa ndiye bilionea wa kwanza wa Muziki wa HipHop huku akikadiriwa kuwa na utajiri wa jumla ya dola bilioni 1

> Anamiliki hisa za dola milioni 70 kwenye kampuni ya usafiri ya Uber, dola milioni 70 kwenye masuala ya sanaa, dola milioni 50 kwenye umiliki wa majumba ya kupangisha na muziki, umiliki wa ‘Tidal’ inayouza nyimbo mtandaoni pamoja na umiliki wa Kampuni ya Roc Nation

Soma - https://jamii.app/JayZNetWorth1Bl
#JFLeo
BEI KIKOMO ZA MAFUTA KWA MWEZI JUNI 2019 ZAONGEZEKA

- Ni bei za mafuta kwa jumla na rejareja yanayoingia nchini kupitia bandari za Dar, Tanga na Mtwara

- Ni kutokana na mabadiliko ya bei ktk soko la ndani na ongezeko la bei ktk soko la dunia

Zaidi, soma https://jamii.app/BeiMafutaJuni-2019
OMAN: Katika kusheherekea sikukuu ya Idd El Fitr, Serikali imefanywa uamuzi wa kuwaachia huru wafungwa 478 ambao kati ya hao 240 ni raia wa kigeni

> Wamesamehewa vifungo vyao na kuachiliwa huru baada ya hati ya msamaha iliyosainiwa na Sultani Kabus bin Said kusambazwa

#JFInternational
SUDAN: WAPINZANI WAKATAA UCHAGUZI ULIOITISHWA NA JESHI

- Viongozi wameitisha maandamano mapya na kukataa mpango wa uchaguzi mpya

- Chama cha Wanataaluma kimesema sio Wanajeshi wala washirika wake, watakaomua mustakabali wa watu wa Sudan

Zaidi, soma https://jamii.app/MilitaryCallsElection
MWEZI WAANDAMA, SIKUKUU YA EID AL FITR KUSHEREHEKEWA KESHO

- Mufti wa Tanzania, Sheikh Mkuu Abubakar Zubeir ametangaza kuwa mwezi umeonekana katika maeneo mbalimbali nchini

- Swala ya Idd Kitaifa itaswaliwa Tanga na kuongozwa na Mufti Zubeir

Zaidi, soma https://jamii.app/MweziWaandamaEidKesho
MWISHO WA MATUMIZI YA PASIPOTI ZA ZAMANI NI JANUARI 2020

> Msemaji Idara ya Uhamiaji, Ally Mtanda amewataka watu wote wanaotarajia kusafiri safari za nje ya nchi hivi karibuni kuhakikisha wanabadilisha pasipoti zao hadi kufikia Julai 2019

> Kisheria pasipoti inatakiwa kuwa hai angalau miezi 6 ili iweze kuombewa visa

Soma - https://jamii.app/PassportRenewal
Bodi, Menejimenti na Wafanyakazi wa Jamiiforums wanapenda kuwatakia Waislamu wote Kheri, Amani na Baraka katika sikukuu ya Eid al-Fitr baada ya Kumaliza mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani

#JFLeo #EidMubarak
MBEYA: MBARONI WAKIDAIWA KUMUUA MFANYABIASHARA WA UFUTA

- Watu 2 wa familia moja, wanashikiliwa na Polisi wakidaiwa kumuua Oswald Malambo na kumpora Tsh. Milioni 55

- Inadaiwa waliweka sumu kwenye kinywaji cha Oswald wakiwa wote baa

Zaidi, soma https://jamii.app/MuuzaUfutaAuawa-Mbeya
DANIEL STURRIDGE NA ALBERTO MORENO KUONDOKA LIVERPOOL

- Wanaondoka majira haya ya joto baada ya mikataba yao kumalizika

- Sturridge(29) amefunga magoli 67 katika mechi 160 tangu alipojiunga Januari 2013 huku Moreno(26) akicheza mechi 141 tangu ajiunge Agosti 2014
BENI: KUNDI LA WAASI LA ADF LAUA WATU 12

- Kundi la The Allied Democratic Forces(ADF) limewaua watu hao katika mji wa Beni Mashariki mwa nchi ya DR Congo

- Waasia hao pia walivamia kambi ya Jeshi ya Rwangoma na kuua Wanajeshi wawili

Zaidi, soma https://jamii.app/ADFLaua12Beni-DRC
SERIKALI YATOA KANUNI MPYA KWA WANUNUZI NA WAUZAJI WA MKAA

> Wanunuaji wa mkaa na samani wanatakiwa wawe na risiti za bidhaa kutoka kwenye maeneo ya mauzo yaliyosajiliwa

> Adhabu kwa atakayezikiuka ni faini ya Tsh 500,000 hadi Tsh milioni 12 au kifungo kati ya miezi 6 hadi miaka 5

Soma - https://jamii.app/KanuniBidhaaMisitu
VITUO VYA HABARI VYAPIGWA FAINI KWA MADAI YA KURUSHA HABARI ZA UONGO

> Kamati ya Maudhui ya TCRA imetoa adhabu ya kulipa faini kwa kusambaza na kutangaza habari zisizo na ukweli

> Vituo hivyo ni: Azam Media Ltd na Gilly Bonny Online TV

Soma - https://jamii.app/FainiVituoHabari
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
RC wa Iringa, Ally Hapi akizungumzia Tamko la Wanahabari waliompa siku 7 kuomba radhi kutokana na kauli yake ya kugawa Vitambulisho vya Wafanyabiashara Wadogo kwa Wanahabari

Anasema, “Nikajiuliza Mkuu wa Mkoa unampa siku 7, unaelewa maana ya Mkuu wa mkoa? Nilipoona nikacheka. Mimi ni mwakilishi wa Rais.”
WANAFUNZI WAZAMA ZIWANI WAKITALII, WATATU WAPOTEZA MAISHA

> Wanafunzi 3 kati ya 5 wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Makurugusi, Wilayani Chato wamepoteza maisha baada ya mtumbwi waliokuwa wakiutumia kufanya utalii wa ndani kuzama Ziwa Victoria jana asubuhi

Soma - https://jamii.app/WanafunziVifoUtalii