JamiiForums
52.9K subscribers
34.3K photos
2.43K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
WATU 13 WAMEUAWA KATIKA SHAMBULIO LA RISASI

- Wengine 4 wamejeruhiwa akiwemo Afisa wa Polisi hapo jana huko Virginia Beach, Marekani

- Mfanyakazi wa Idara ya nishati na maji aliwafyatulia risasi wafanyakazi wenzake kabla ya kuuawa na Polisi

Zaidi, soma https://jamii.app/ShambulioRisasiVirginia
MCHEZAJI WA ZAMANI WA ARSENAL NA REAL MADRID, JOSE ANTONIO REYES, AFARIKI

- Amefariki pamoja na binamu zake wawili leo asubuhi katika ajali ya gari iliyotokea Utrera nje kidogo ya Seville nchini Uhispania

- Ameacha mke na watoto watatu, Wasichana wawili na Mvulana mmoja

#JFLeo
CHINA YATANGAZA NYONGEZA YA USHURU KWA BIDHAA ZA MAREKANI

- Imefanya hivyo huku ikijitayarisha kutoa orodha ya kampuni mbaya za kigeni

- Inadaiwa inataka kuiadhibu Marekani na kampuni za kigeni zinazoacha kufanya kazi na kampuni ya Huawei

Zaidi, soma https://jamii.app/ChinaTariffsUSA
LIVERPOOL YATAWAZWA KUWA MABINGWA WAPYA ULAYA

- Imefanikiwa kuwa bingwa wa michuano ya Klabu Bingwa Ulaya baada ya kuifunga Tottenham goli 2-0 katika mchezo wa fainali

- Liverpool sasa inakuwa imechukua kombe hilo mara 6 huku kwa Tottenham hii ilikuwa fainali ya kwanza
WAZIRI KALEMANI: MAGARI MAPYA YA WIZARA YA NISHATI YATATUMIA GESI BADALA YA MAFUTA

> Amesema lengo la uamuzi huo ni kubana matumizi ya mafuta, kutunza mazingira na kuhamasisha wizara nyingine na watu binafsi kutumia gesi

> Aidha, Aprili 2019, Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania, lilianza mazungumzo na mradi wa mabasi yaendayo kasi ili kuyawezesha mabasi hayo kutumia nishati ya gesi

Soma https://jamii.app/MagariYaGesi
MAREKANI KUCHUNGUZA MITANDAO YA KIJAMII YA WANAOOMBA ‘VISA’

- Hii ni kulingana na Sheria Mpya za Idara ya Maswala ya Kigeni

- Waombaji watatakiwa kutoa majina ya akaunti wanazotumia, anwani za miaka mitano, pamoja na namba za simu

Soma https://jamii.app/USSocialMediaInfo
IKULU: RAIS MAGUFULI KUFANYA MKUTANO NA WAFANYABIASHARA WAKUBWA WA 5 KUTOKA KILA WILAYA

- Mkutano huo utafanyika tarehe 7 Juni, 2019 kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kikwete, kuanzia saa 8:00 asubuhi

- Wakuu wa Mikoa kupendekeza majina ya wafanyabiashara hao

Soma https://jamii.app/MagufuliNaWafanyabiashara
SERENGETI: HIFADHI BORA BARANI AFRIKA KWA MWAKA 2019

- Tuzo hiyo imetolewa jana nchini Mauritius na Taasisi ya World Travel Awards

- Mwaka jana pia Serengeti ilishinda tuzo hiyo kupitia mtandao wa safari za utalii wa safaribookings

Zaidi, soma https://jamii.app/SerengetiHifadhiBora-2019
HASHIM RUNGWE ATAKIWA KURIPOTI KITUO CHA POLISI KESHO

> Wito huo ni baada ya mkutano wa viongozi wa vyama 8 vya upinzani na Waandishi wa habari

> Katika mkutano huo, viongozi wa vyama hivyo wametangaza kutoshiriki uchaguzi wa marudio kwenye Kata 32

Zaidi, soma https://jamii.app/PolisiVsRungwe
WATU 10 WAMEUAWA KATIKA SHAMBULIO LA KUJITOA MUHANGA

- Na wengine 20 wamejeruhiwa siku ya Jumamosi katika shambulio hilo la bomu la kujitoa muhanga mjini Raqa, ngome ya zamani ya Wanamgambo wa Dola la Kiislamu, Kaskazini mwa Syria

Zaidi, soma https://jamii.app/10WalipuliwaRaqqa
WANAOFANYA MIAMALA YA FEDHA KWA MTANDAO WATAKIWA KUTOA TAARIFA KABLA

> Kanuni mpya za kudhibiti utakatishaji fedha, zinataka taarifa za mtu anayefanya muamala wa fedha zenye thamani ya Dola za Marekani 10,000(zaidi ya Tsh mil. 20) au zaidi, kutoa taarifa Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu kabla ya kufanya muamala huo

Soma - https://jamii.app/KanuniMiamalaFedha
KHARTOUM, SUDAN: KAMBI YA WAANDAMANAJI YAVAMIWA, MABOMU NA RISASI ZARINDIMA

- Jeshi limeziba barabara kuzuia Waandamanaji wanaotaka Jeshi likabidhi utawala kwa raia

- Mtu mmoja ameripotiwa kufariki huku raia kadhaa wakiwekwa chini ya ulinzi

Zaidi, soma https://jamii.app/GunfireProtestorsKhartoum
KIPINDUPINDU, DAR: WATATU WAFARIKI, 55 WALAZWA

- Temeke vifo ni 2 na Wagonjwa 34; Ilala, kifo kimoja na wagonjwa 19 na Kinondoni kuna wagonjwa 2

- Waziri Ummy ametaja baadhi ya maeneo korofi kuwa ni Keko, Tandika, Buza, Kariakoo, Mchikichini, Kivule na Vingunguti

Zaidi, soma https://jamii.app/KipindupinduChaua-Dar
UEFA SUPER CUP: MARA YA KWANZA VILABU VYA ENGLAND KUKUTANA

- Bingwa wa Klabu Bingwa Ulaya, Liverpool itachuana na Bingwa wa Europa Ligi, Chelsea mnamo Agosti 14, 2019

- Liverpool imekuwa Bingwa baada ya kuifunga Tottenham huku Chelsea ikiwa Bingwa kwa kuifunga Arsenal
SERIKALI KUTOBADILI VYUO VYA MAENDELEO KUWA VYA UFUNDI STADI

> Naibu Waziri wa Elimu, William Ole Nasha amesema Serikali haina mpango wa kuvibadili Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi kuwa Vyuo vya Ufundi Stadi (VETA) bali imejikita katika kuboresha vyuo hivyo kwa kuvikarabati na kuviongezea vifaa ili viweze kutoa mafunzo bora

Soma - https://jamii.app/VyuoMaendeleoVeta
BUNGENI: MAONI YA UPINZANI KUHUSU WIZARA YA FEDHA, YAZUILIWA

- Spika Ndugai amedai hotuba hiyo ina makosa na imejaa maneno yasiyofaa

- Sababu nyingine ni Mbunge Halima Mdee aliyesimamishwa kuhudhuria mikutano 2 kushiriki kuandaa hotuba hiyo

Zaidi, soma https://jamii.app/HotubaFedhaUpinzaniYafutwa
MITAA YOTE KWENYE MAJIJI KUWEKEWA UMEME IFIKAPO JUNI 30

> Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani ameliagiza Shirika la Umeme Tanzania kuhakikisha mitaa yote kwenye majiji, inapatiwa umeme ifikapo Juni 30, mwaka huu ili maeneo hayo yafanane na hadhi ya jiji

Soma - https://jamii.app/UmemeMitaaJiji
IKULU, DAR: ASKOFU GWAJIMA AKUTANA NA RAIS MAGUFULI

- Rais Magufuli amekutana na kuzungumza na Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Dkt. Josephat Gwajima leo Juni 3, 2019 Ikulu jijini Dar

Zaidi, soma https://jamii.app/GwajimaMagufuli-Ikulu