JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
RAIS MAGUFULI AUOMBA UMOJA WA ULAYA NA MAREKANI KUIONDOLEA VIKWAZO ZIMBABWE

> Rais Magufuli amesisitiza kwamba Zimbabwe ipo kwenye njia sahihi ya kuufufua uchumi wake chini ya Serikali ya Rais Emmerson Mnangagwa

Zaidi, soma => https://jamii.app/MagufuliVikwazoZimb
WAZIRI MBARAWA: MIRADI 88 IMEJENGWA CHINI YA KIWANGO

- Waziri huyo wa Maji, amekiri kuwepo kwa miradi hiyo ya maji iliyojengwa kati ya mwaka 2010 na 2015

- Amesema Serikali imekuwa ikikarabati vyanzo vya maji na pia imetenga Tsh. Milioni 135

Zaidi, soma https://jamii.app/Miradi88MajiChiniKiwango
CHELSEA YANYAKUA KOMBE LA EUROPA LIGI

- Imechukua ubingwa huo baada ya kuifunga Arsenal goli 4-1 katika fainali iliyofanyika Baku, Azerbaijan

- Magoli ya Chelsea yamefungwa na Giroud(49’), Pedro(60’) na Hazard(65’ na 72’) huku goli la Arsenal likifungwa na Iwobi(69’)
TABORA: ADAIWA KUMUUA MUMEWE KISA WIVU WA MAPENZI

- Sada Abdallah anatuhumiwa kumuua mumewe kwa kumpiga na kisha kumsukuma na kusababisha aangukie kisogo

- Alikuwa akimtuhumu mumewe huyo kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Mwanamke mwingine

Zaidi, soma https://jamii.app/AmuuaMumeweMapenzi-TBR
JE, WAIJUA HISTORIA YA NENO KILIMANJARO?

> Asili ya neno hili ni makosa ya kisarufi yaliyofanywa na wageni kutoka Ulaya

> Wazawa waliuita Kilimakyaro (Kilimakirefu) lakini makosa ya kimatamshi ya Wageni yalipelekea kuzaliwa neno Kilimanjaro

Soma > https://jamii.app/HistiriaKilimanjaro

#JFHistoria
SERIKALI: NGUVU YA SOKO CHANZO KUTOSHUKA BEI YA TAULO ZA KIKE

- Imesema bei haijashuka licha ya kuondoa Kodi ya Ongezeko la Thamani katika taulo hizo

- Imeeleza bei inatokana na sababu mbalimbali zikiwemo gharama za malighafi na uwekezaji

Zaidi, soma https://jamii.app/BeiTauloKikeKutoshuka
BAKWATA: BARAZA LA EID EL FITR KUFANYIKA TANGA

> Taarifa rasmi ya BAKWATA imeeleza kuwa sikukuu hiyo itafanyika Juni 5/6 kulingana na mwandamo wa mwenzi

> Baraza la Eid litafanyika mkoani Tanga na Waziri Mkuu, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi

Soma > https://jamii.app/EidalFitrTz
RUKWA: MWALIMU MBARONI KWA KUMPIGA MWANAFUNZI HADI KUMSABABISHIA UPOFU

- Mwalimu Peter Silamba wa Sekondari ya Kate, Wilayani Nkasi anatuhumiwa kumpiga machoni kwa fimbo, Nicholaus Kwimba(17) wa kidato cha 3 wakati akimuadhibu kwa uchelewaji

Zaidi, soma https://jamii.app/MwalimuUpofuMwanafunzi-RKW
ARUSHA: WATAKAO KAMATWA NA MIFUKO YA PLASTIKI KUFUNGIWA UWANJA WA SHEIKH AMRI ABEID

> Jeshi la Polisi limesema litalazimika kufanya hivyo endapo mahabusu zitakuwa zimejaa

> Watuhumiwa watahifadhiwa uwanjani hapo hadi watakapofikishwa Mahakamani

Soma > https://jamii.app/MifukoPlastikiArusha
ISRAEL: WAZIRI MKUU ASHINDWA KUUNDA SERIKALI. BUNGE KUVUNJWA

- Israel itafanya uchaguzi mpya Septemba 2019 baada ya Wabunge kupitisha hoja ya kulivunja Bunge kufuatia Waziri Mkuu, Benjamin Netanyahu kushindwa kuunda Serikali ya muungano

Zaidi, soma https://jamii.app/UchaguziMpyaIsrael
KIEV: BUNGE LA UKRAINE LAKATAA WAZIRI MKUU KUJIUZULU

> Wabunge kwa kupiga kura wamekataa ombi la Waziri Mkuu, Volodymyr Groyman kujiuzulu

> Wasema endapo Waziri Mkuu atajiuzulu hatua hiyo inaweza kuzua machafuko na ghasia nchini humo

Soma > https://jamii.app/BungeVsUkrainePM
SERIKALI: SI LAZIMA WATUMISHI WOTE WA UMMA KUWA NA LAINI ZA TTCL

- Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas amebainisha kuwa Viongozi wanaohudumiwa stahili ya simu watapewa vocha za TTCL lakini hakuna agizo la ulazima kwa Watumishi wengine

Zaidi, soma https://jamii.app/LainiTTCLWatumishi
MBOZI: MILIONI 15.2 ZA MAUZO YA VITAMBULISHO VYA ‘WAMACHINGA’ HAZIONEKANI

- Fedha hizo ni za Wafanyabiashara wadogo 760 waliopewa vitambulisho katika Halmashauri ya Mbozi

- Baadhi ya Watendaji wameshindwa kuwasilisha fedha ama vitambulisho

Zaidi, soma https://jamii.app/FedhaVitambulisho-Mbozi
MICHEZO: INTER MILAN IMETHIBITISHA KUVUNJA MKATABA NA KOCHA LUCIANO SPALLETI

- Klabu hiyo inadaiwa kuwa imeshampitisha Kocha wa zamani wa Chelsea, Antonio Conte kama mrithi wa Spalleti

- Aidha, Conte anadaiwa kutaka kuwasajili Romelu Lukaku na Victor Moses akiwa Inter Milan
MICHEZO: Klabu ya Yanga imemsajili Mchezaji wa klabu ya APR ya Rwanda, Issa Bigirimana kwa mkataba wa miaka miwili

- Hadi sasa Yanga imewasajili Patrick Sibomana, Abdulaziz Makame, Mohammed Ali Camara na Ally Sonso
MKATABA WA BIASHARA HURIA AFRIKA WAANZA KUFANYA KAZI

- Umoja wa Afrika unasema mkataba huo utawezesha kufanyika biashara zitakazofika thamani ya USD Trillioni 2.5

- Unaanza kufanya kazi baada ya nchi 22(idadi iliyokuwa inahitajika) kuridhia

Zaidi, soma https://jamii.app/BiasharaHuriaAfrikaKuanza
SHINYANGA: MWANAFUNZI WA DARASA LA 4 AKATISHA MASOMO KWA UJAUZITO

> Ni Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Welezo mwenye umri wa miaka 11 amekatisha masomo baada ya kukutwa na ujauzito wa miezi 7

> Alipewa ujauzito mwaka 2018 na mwanaume ambaye hajafahamika

Soma > https://jamii.app/UjauzitoMiaka11
ASHIKILIWA NA TAKUKURU KWA KUMPA RUSHWA MWANASHERIA WA CCM

ILALA, DAR: TAKUKURU inawashikilia watu 3 akiwemo mmiliki wa Kampuni ya Motrax, Chandulal Ladwa ambaye anatuhumiwa kutoa rushwa ya laki 2 ili apendelewe kwenye miradi ya chama hicho

Soma => https://jamii.app/RushwaCCM

#JFLeo
UFILIPINO YAZIRUDISHA KONTENA 69 ZA TAKA ZA PLASTIKI NCHINI CANADA

> Takataka hizo ziliingizwa kati ya mwaka 2013 hadi 2014 kwa kile kilichoelezwa kuwa ni malighafi kwa ajili ya kuchakatwa na kutengenezea bidhaa mpya

Zaidi, soma => https://jamii.app/TrashPhilippinesCanada
ZANZIBAR: AOLEWA NA ALIYEMBAKA KUFICHA AIBU YA FAMILIA

> Mwanaume alikiri kosa la kubaka na kuomba mambo yamalizwe kwani anania ya kumuoa binti huyo

> Hata hivyo binti alitelekezwa huku Mtoto aliyejifungua akiwa na tatizo la kuvuja mkojo kwenye kibofu

Kwa kisa hiki, soma > https://jamii.app/UbakajiNdoaZNZ