JamiiForums
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
BOEING YAKIRI KUWEPO HITILAFU KWENYE ‘SOFTWARE’ YA 737 MAX

> Yalazimika kurekebisha makosa kwenye “flight simulator software” ya 737 MAX baada ya ajali 2 zilizoua watu 346

> Licha ya kukiri haijasema ni lini waligundua tatizo hilo

Soma https://jamii.app/BoeingFault737MAX
SONGWE: MTOTO MWENYE ULEMAVU ATELEKEZWA NA WAZAZI WAKE

> Ameokotwa katika pori lililopo Bupingu na anatunzwa na kupatiwa matibabu kwenye hospitali ya Wilaya ya Ileje

> Matukio haya yamekuwa yakitokea mara kwa mara kwenye eneo hilo

Soma https://jamii.app/MtotoMlemavuAtelekezwa
AJALI: Basi la Kampuni ya Tahmeed lenye namba za usajili KCN 970R, linalofanya safari zake kati ya Dar na Mombasa, Kenya limegongana na Lori la mizigo lenye namba za usajili T235 AXJ, maeneo ya Jogoo, Jijini Dar

Kamanda wa Kikosi cha Usalama barabarani Wilaya ya Kinondoni, ASP Sadick Msangi amethibitisha kuwa hakuna Majeruhi wala Vifo katika Ajali hiyo
RAIS MAGUFULI NI MGENI RASMI KWENYE MASHINDANO YA KUHIFADHI QURAN

- Mshindi atapata Tsh. milioni 20 katika mashindano hayo yaliyoandaliwa na Taasisi ya Al Hikma Foundation

- Pia, Dkt. Jakaya Kikwete na Mhe. Ally Hassan Mwinyi wamehudhuria

Soma https://jamii.app/MashindanoYaKuhifadhiQuran
#JFLeo
MIILI YA VICHANGA WAWILI YAKUTWA MTONI

> Miili hiyo inayoaminiwa kuwa ya mapacha imekutwa Mto Nairobi nchini Kenya katika zoezi la usafi

> Gavana Sonko ametoa wiki 1 uchunguzi ufanyike ikiwa ni tukio la 8 la aina hii ndani ya kipindi kifupi

Soma https://jamii.app/VichangaMtoNairobi
KENYA: MAAFISA POLISI WAWILI WATIWA NGUVUNI KWA KULAZIMISHA KUJAZIWA MAFUTA BURE

> Walifika kwenye kituo cha mafuta kilichopo Kisumu majira ya saa 7 usiku wakiwa wanaendesha Pikipiki

> Walimpiga muhudumu wa kituo na dereva wa gari la mafuta

Soma https://jamii.app/KenyanPoliceArrested
UGANDA: 2 WAFARIKI, ZAIDI YA 13 HAWAONEKANI KATIKA AJALI YA BOTI

> Boti hiyo waliyokuwa wakisafiria ilipinduka katika Ziwa Albert, Magharibi mwa Uganda Jumapili jioni mita chache kutoka Runga

> Watu wengine 32 waliokuwa katika boti hiyo walifanikiwa kuogelea na kufika Pwani

Soma - https://jamii.app/BoatAccidentUG
KARAGWE, KAGERA: BASI LA KAMPUNI YA FIKOSHI LAGONGA TEMBO

> Tembo huyo amegongwa jana usiku katika eneo la Byenturege Kitengule wakati basi hilo lilipokuwa likitokea Mwanza

> Basi hilo lenye namba T 872 CJQ linafanya safari zake kati ya Mwanza na Karagwe

Soma > https://jamii.app/TemboKaragwe
DUBAI: MIGAHAWA YATAKIWA KUWEKA WAZI KALORI(CALORIES) ZILIZOPO KWENYE VYAKULA WANAVYOUZA

> Kwa kuanzia agizo hili litazihusu taasisi zenye matawi 5 ya migahawa na kufikia Novemba mwaka 2020 migahawa yote pamoja na hoteli itahusika

Soma => https://jamii.app/DubaiFoodMenus
TANZIA: Aliyewahi kuwa Waziri wa Michezo na Naibu Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Ali Juma Shamhuna amefariki dunia

> Alikuwa Mbunge wa Jimbo la Donge kuanzia mwaka 1995 kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM)

Soma https://jamii.app/RIPShamhuna
MAAFISA ARDHI WOTE WA MKOA WAHAMISHWA SABABU YA MIGOGORO

> Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi, William Lukuvi ameagiza hivyo kutokana na kukithiri kwa migogoro ya ardhi Mkoani Morogoro licha ya jitihada zinazofanywa na Serikali katika kutatua migogoro ya ardhi

> Aidha, ameamua kuirejesha kanda ya Mashariki ambayo sasa itakuwa kanda maalum ya ardhi ya mkoa huo

Soma - https://jamii.app/UhamishoArdhiMRG
MBUNGE STEVEN MASELE AWASILI BUNGENI KWA AJILI YA KUJOHIWA

> Mbunge huyo wa Shinyanga Mjini (CCM) ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika(PAP) atahojiwa na Kamati ya Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge, kujibu tuhuma zinazomkabili za utovu wa nidhamu

Soma - https://jamii.app/MaseleKamatiMaadili
KAMPUNI YA GOOGLE YATANGAZA KUACHA KUFANYA KAZI NA KAMPUNI YA HUAWEI

> Kampuni kubwa ya Teknolojia duniani(Google) imetangaza leo kuacha kufanya kazi na kampuni ya simu ya nchini China Huawei, kufuatia amri ya Marekani ya kuzuia matumizi ya vifaa vya Huawei kwa madai kuwa vinahatarisha usalama

> Simu zote za Huawei zenye mfumo wa 'Android' hazitaweza kufanya 'Updates'

Soma - https://jamii.app/GoogleBanHuawei
#JFTeknolojia
POLISI TABORA WAAGIZWA KUZIACHIA PIKIPIKI ZOTE WALIZOKAMATA

> Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora limepewa saa kadhaa leo Mei 20, kuziachia pikipiki zote walizozikamata na ikifika jioni bila agizo hilo kutekelezwa, watakumbana na Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola

> Ametaja makosa ya pikipiki kutakiwa kupelekwa kituo cha Polisi kuwa ni kesi za uhalifu, zinazoibiwa na zisizo na wenyewe na kwamba makosa mengine ni ya kulipa faini

Soma - https://jamii.app/LugolaPolisiPikipiki
TANZIA: BRIGEDIA MSTAAFU, HASSAN NGWILIZI AFARIKI

> Amefariki muda mfupi uliopita ktk Hospitali ya Jeshi Lugalo alipokuwa akipatiwa matibabu

> Aliwahi kuwa Mbunge wa Mlalo-Lushoto, Waziri wa TAMISEMI na Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya Bunge

Soma - https://jamii.app/RIPBrigediaNgwilizi
#JFLeo
NAIROBI, KENYA: WAWILI WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA KUIBA BIBLIA

> Biblia hizo zipatazo 800 zina thamani ya TSh. 20,987,764/= na walizipata kwa njia ya udanganyifu

> Hata hivyo wamekana mashtaka na kuachiwa kwa dhamana

Soma > https://jamii.app/WaibaBiblia
TATIZO LA KUKOSA CHOO AU KUPATA CHOO KIGUMU

> Kwa kawaida mtu anapaswa kupata choo cha uhakika japo mara moja kwa siku, kutegemeana na mlo wake wa kila siku

> Mtu mwenye tatizo hili huwa na dalili kadhaa, ikiwemo kutumia nguvu na muda mwingi wakati wa kujisadia. Ulimi huwa na utandu mweupe na hutoa harufu mbaya mdomoni na tumbo kujaa wakati wote

> Tatizo hili husababishwa zaidi na ulaji mbaya wa vyakula, kuacha kula matunda na kutokunywa maji ya kutosha kwa siku

Kufahamu tiba, soma - https://jamii.app/ConstipationDisease
#JFAfya
NYERI, KENYA: MWANAFUNZI AJIUA NA KUACHA UJUMBE WA LAWAMA KWA BABA YAKE

> Joan Mumbi(19) ameacha ujumbe unaoeleza kuwa shinikizo la Baba yake kutaka afanye vyema kwenye masomo huku yeye akiomba kuhamishwa shule ni moja ya sababu

Soma > https://jamii.app/MwanafunziAjiuaNyeri
NAPE AIOMBA SERIKALI KUMRUHUSU CAG KUKAGUA MALIPO YA KOROSHO

> Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye amesema kuwa zoezi la ulipaji wakulima wa Korosho limetawaliwa na dhuluma pamoja na rushwa, huku akibainisha kuwa zaidi ya wakulima 1,181 mpaka sasa katika jimbo lake hawajalipwa pesa zao

> Ameishauri Serikali kumruhusu Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, kwenda kufanya ukaguzi katika zoezi hilo ili kuubaini ukweli

Soma - https://jamii.app/MalipoKoroshoCAG
#JFLeo
MKE WANGU ALINICHONGEA NIKAFUKUZWA KAZI, SASA ANANITESA

> Mdau wa JamiiForums anasema alikuwa akifanya kazi aliyotafutiwa na Mke wake na ndiye aliyesuka mpango wa kumuachisha kazi

> Anaomba ushauri wa hatua ya kuchukua kwani kwa sasa amekutwa Baba wa Nyumbani

Soma > https://jamii.app/MkeWanguAnanitesa