JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
WAASI RWANDA: HAKUNA NJIA NYINGINE ZAIDI YA KUPIGANA NA KAGAME

- Msemaji wa NLF, Meja Sankara amesema Rais Kagame ni Muuaji na Dikteta hivyo watapigana naye ili kuikomboa Rwanda

- Waasi wanashikilia barabara ya Kigali hadi Ruzizi

Soma https://jamii.app/WaasiVsKagame
UPINZANI KUANDAMANA KUSHINIKIZA BUNGE KUFANYA KAZI NA CAG

- Vijana wa ACT-Wazalendo, NCCR Mageuzi, CHAUMA, UPDP na Vyama vingine vitatu kuandamana Jijini Dodoma Aprili 9, 2019

- Wamwomba Spika wa Bunge au Naibu Spika ayapokee maandamano yao Bungeni

Soma https://jamii.app/MaandamanoDOMCAG
SPIKA NDUGAI: LISSU AMESHALIPWA MADAI YAKE YOTE

- Spika amesema, Lissu ameshalipwa madai yake yote na kama kuna madai mengine awasiliane na mamlaka husika na si kuandika kwenye Mitandao ya Jamii

- Amisisitiza yeye hawezi kuzuia haki ya mtu

Soma https://jamii.app/MalipoyaLissuYamekamilika
- Waziri wa Mambo ya ndani, Kangi Lugola amemsimamisha kazi Mkuu wa Upelelezi wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Mbogwe, Geita.

- Aidha, Waziri Lugola amemsimamisha kazi Mkaguzi wa Jeshi Wilayani humo, kwa tuhuma za kupokea rushwa

Soma https://jamii.app/MkuuUpeleleziMbogwe
MICHEZO: Klabu ya Arsenal ya Uingereza imekula kipigo cha goli 1-0 kutoka kwa Klabu ya Everton

- Arsenal inabaki na alama 63 sawa na Chelsea na alama 1 nyuma ya Tottenham
WAVAMIA OFISI ZA TRA NA KUIBA NYARAKA, LAPTOP NA PESA

- Wezi wavamia ofisi iliyopo Kahama, Shinyanga na kuondoka na kompyuta mpakato moja, baadhi ya nyaraka za kodi na Shilingi milioni 2

- Uchunguzi unaendelea kubaini wahusika na lengo lao

Zaidi, soma https://jamii.app/WiziTRAKahama
MAGARI YAENDAYO KASI YATISHIA UWEPO WA DUMA

- Utafiti warekodi ongezeko la vifo vya wanyama hao katika mbuga ya Serengeti kutokana na kugongwa na magari ya watalii yaendayo kasi licha ya faini kuwa kubwa

- Watafiti wahofia kupotea kwao

Zaidi, soma https://jamii.app/VifoDumaMwendokasi
AFYA: UMUHIMU WA KUOTA JUA ASUBUHI

> Watu wengi huwa na upungufu wa vitamini D kwasababu hawapati mwanga wa Jua ambao huchochea uzalishaji wa seli katika ngozi ya mwili

> Vitamini D husaidia kuboresha afya ya mifupa na meno

Zaidi, soma => https://jamii.app/FaidaZaJua

#JFAfya
MUME AMUUA MKEWE BAADA YA KUMFUMANIA

> Julius Rotich amemuua mkewe katika kijiji cha Kaplelach, Kaunti ya Kericho nchini Kenya baada ya kumfumania akishiriki mapenzi na jamaa mwingine chumbani mwao usiku wa kuamkia Aprili 6

> Alimshambulia mkewe kwa panga na kisha kujisalimisha Polisi

Soma - https://jamii.app/KifoMkeFumanizi
SIMBA NA TEMBO WAUA MTU ANAYEDAIWA KUWA JANGILI

> Mtu aliyedhaniwa kuwa jangili wa wanyama aina ya faru amekanyagwa na Tembo na kuliwa na Simba katika Hifadhi ya Taifa ya Kruger, nchini Afrika Kusini

> Fuvu pamoja na suruali yake vilipatikana siku ya Alhamisi

Soma - https://jamii.app/KifoJangiliMbugani
KAMBI YA UPINZANI KUPANGUA BARAZA LA MAWAZIRI VIVULI

> Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe amesema watapangua Baraza la Mawaziri Vivuli na kuwaondoa wabunge wa CUF kutokana na baadhi yao kumuunga mkono Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba

> Ikitokea hivyo, CUF imesema wataandika barua kwa Spika Ndugai ili kuomba ziwepo kambi mbili za upinzani Bungeni

Soma - https://jamii.app/WaziriKivuliUpinzani
KILIMANJARO: TAKUKURU YABAINI UFISADI WA BILIONI 1.5

> Ufisadi huo umefanyika katika mradi unaoendelea wa ujenzi wa majengo 6 ya Hospitali ya wilaya ya Siha

> Vifaa vilivyonunuliwa kwa ajili ya mradi viko chini ya kiwango

Soma > https://jamii.app/UfisadiSiha
MAREKANI: WAZIRI WA USALAMA WA NDANI AJIUZULU

> Waziri wa Usalama wa Ndani wa Marekani, Kirstjen Nielsen (46), alijiuzulu Jumapili jioni baada ga mkutano aliofanya na Rais Donald Trump Ikulu mjini Washington DC

> Kamishna wa forodha na ulinzi wa mipakani, Kevin McAleenan, atakaimu nafasi iliyoachwa wazi na Nielsen

Soma - https://jamii.app/KujiuzuluWaziriUsalama
RPC DODOMA: ATAKAYEANDAMANA KESHO ATAPIGWA MPAKA ATACHAKAA

> Kamanda Muroto ametoa kauli hiyo baada ya vijana wa ACT-Wazalendo kutangaza maandamano ya kulishinikiza Bunge kufuta azimio lake la kutofanya kazi na CAG, Profesa Assad

Zaidi, soma => https://jamii.app/RPCDodomaVsACT
BABA MBARONI KWA KUMBAKA MTOTO WAKE

> Jeshi la Polisi Mkoani Geita linamshikilia mkazi wa Kata ya Nyankumbu, Selemani Mathis (35), kwa tuhuma za kumbaka binti yake (4)

> Mtoto huyo alikuwa akiishi na baba yake baada ya wazazi wake kutengana

Soma - https://jamii.app/BabaUbakajiMtoto
UZALISHAJI MIFUKO YA PLASTIKI KUSITISHWA JULAI 2019

> Serikali imesema iwapo watakubaliana na taasisi mbalimbali wanazotarajia kukutana nazo wiki hii wanaweza kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki kuanzia Julai mwaka huu

> Kauli hiyo imetolewa leo Aprili 8 Bungeni, na Waziri January Makamba wakati akijibu swali la Mbunge Magdalena Sakaya

Soma - https://jamii.app/ZuioMifukoPlastiki
LUSINDE: 2020 TUFANYE UCHAGUZI WA MADIWANI NA WABUNGE, RAIS AENDELEE

> Mbunge wa Jimbo la Mtera(CCM), Livingstone Lusinde amesema hatua hiyo itasaidia kupunguza gharama kubwa ambazo taifa itazitumia katika uchaguzi huo

Soma > https://jamii.app/KauliLusinde
POLISI WAUA WATU 5 WANAODHANIWA KUWA MAJAMBAZI

> Watu 5 wanaodhaniwa kuwa majambazi wameuawa baada ya kutokea kwa majibizano ya risasi kati yao na Polisi Wilayani Korogwe mkoani Tanga walipofanya jaribio la uporaji kwenye mashamba ya Mkonge

Soma https://jamii.app/PolisiMajambaziKorogwe
MACHAKOS, KENYA: WATUHUMIWA WATATU WA UTEKAJI WA AFISA WA UMOJA WA MATAIFA WAUAWA

> Walikutwa ktk barabara ya Kitui wakijifanya maafisa wa usalama barabarani na kusimamisha magari ndipo walipowekwa chini ya ulinzi na Askari Polisi

Soma > https://jamii.app/WatekajiKenya