JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
SERIKALI KUKATA RUFAA UAMUZI KUHUSU SHERIA YA HUDUMA YA HABARI

> Ni baada ya Mahakama ya Afrika Mashariki kuitaka kuhakikisha vifungu vinaendana na Mkataba wa Jumuiya Ya Afrika Mashariki

> Yasema Mahakama inaunga mkono uhuru usio na mipaka

Zaidi, soma https://jamii.app/RufaaSheriaHabari
SERIKALI YATAIFISHA KILO 343 ZA DHAHABU TANGU APRILI 2018 HADI SASA

- Mwaka 2018, ilitaifisha Kilo 24 huku Kilo 319 zikitaifishwa juzi jijini Mwanza

- Kwa kipindi hicho pia imetaifisha Tani 75 na Kilo 25 za madini ya vito ikiwamo tanzanite

Zaidi, soma https://jamii.app/Kilo343DahabuYataifishwa
VIONGOZI WA KANISA KATOLIKI ROMBO WAFUNGA KUOMBEA ULEVI

> Kufunga kwa siku 9 kumuomba Mungu aiepushe jamii yao na ulevi uliopindukia hususani kwa vijana

> Inasemekana vijana wengi wanashindwa kuoa kwa sababu ya ulevi

Zaidi, soma https://jamii.app/MfungoUleviRMB
MICHEZO: GONZALO HIGUAIN ATANGAZA KUSTAAFU KUCHEZA TIMU YA TAIFA

- Mshambuliaji huyo wa Argentina amestaafu kuichezea timu ya Taifa baada ya kuifungia magoli 31 katika michezo 75

- Amesema "Kwa furaha ya wengi, sasa nitakuwa naangalia tu timu ikicheza nikiwa nje”

#JFLeo
BURUNDI: SERIKALI YAZUIA MATANGAZO YA BBC NA VOA

- Matangazo ya Shirika la habari la Uingereza(BBC) na Shirika la Habari la Marekani(VOA) yamezuiwa kwa muda usiojulikana

- Mashirika hayo yanashutumiwa kwa kutokuwa na weledi na kukiuka sheria

Zaidi, soma https://jamii.app/BBC-VOAvsBurundi
INDIA YADAIWA KUITUNGUA HELKOPTA YAKE IKIJARIBU KUTUNGUA NDEGE YA PAKISTANI

- Inaelezwa helkopta hiyo ilianguka muda mfupi baada ya kombora kurushwa

- Wanajeshi 6 waliokuwemo kwenye helkopta na raia mmoja aliyeangukiwa na mabaki, wamefariki

Zaidi, soma https://jamii.app/IndiaYalipuaNdegeYake
CHAD: MAHAKAMA YAENDELEA KUBARIKI KUFUNGIWA MITANDAO

> Mahakama imetupilia mbali ombi la Wanasheria la kuitaka kuamuru Serikali kuruhusu matumizi ya mitandao ya kijamii iliyofungiwa tangu Machi, 2018

> Mitandao hiyo yadaiwa kuhatarisha usalama wa nchi

Zaidi, soma https://jamii.app/InternetBanChad
ARUSHA: AFISA USALAMA AUNGANISHWA KWENYE KESI YA MKURUGENZI WA OBC

- Afisa huyo wa Wilaya ya Ngorongoro, Issa Selfu Ng’itu ameunganishwa kwenye kesi ya uhujumu uchumi ya Mkurugenzi wa OBC, Isaya Mollel(59) na kusomewa jumla ya mashtaka 15

Zaidi, soma https://jamii.app/AfisaUsalamaKesiOBC
MAREKANI: WIZARA YA ULINZI YAIDHINISHA UJENZI WA UKUTA

- ‘The Pentagon' imeidhinisha kuhamishiwa kwa Dola Bilioni 1 kwenda akaunti ya Wahandisi wa Jeshi kwa ajili ya ujenzi wa ukuta wa mpaka baina ya nchini hiyo na Mexico

Zaidi, soma https://jamii.app/UjenziWaidhinishwaKujengwaUSA
VATICAN: SHERIA MPYA KUHUSU UNYANYASAJI WA KINGONO YATANGAZWA

- Wafanyakazi wote katika Makao Makuu ya Kanisa Katoliki na Wanadiplomasia wanaomwakilisha Papa duniani kote wanatakiwa kutoa taarifa haraka juu ya madai ya unyanyasaji wa kingono

Zaidi, soma https://jamii.app/KatolikiSheriaNgono
RUKWA: RADI YAANGUSHA UKUTA WA NYUMBA NA KUUA MMOJA

- Mtu mmoja mkazi wa Kata ya Mkoe, Wilayani Kalambo, Girubat Lungwa(34) amefariki baada ya radi kubomoa ukuta wa nyumba yake kisha kuingia ndani na kusabisha kifo chake papo hapo

Zaidi, soma https://jamii.app/RadiYauaRukwa
RUVUMA: MWANAFUNZI APORWA BAISKELI NA KISHA KUUAWA

- Tariq Mohamed(16) wa darasa la 6 ameporwa baiskeli kisha kunyongwa hadi kufa katika tukio lililotokea Wilayani Tunduru

- Alifanyiwa unyama huo akitokea shambani alikotumwa kuchukua karanga

Zaidi, soma https://jamii.app/MwanafunziAnyongwaAfarikiRVM
IKULU, DAR: RAIS MAGUFULI AWATUNUKU KAMISHENI MAAFISA WANAFUNZI WA JWTZ

- Amewatunuku Maafisa Wanafunzi 146 kuwa na cheo cha Luteni Usu, Wanaume wakiwa 140 na Wanawake 6

- Walipata mafunzo katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi mkoani Arusha

Zaidi, soma https://jamii.app/MagufuliAtunukuKamisheni-Machi2019
IRINGA: WANAOKOPESHA FEDHA MITAANI WATAKIWA KUJISALIMISHA TRA

- RC Ally Hapi ameagiza wanaofanya biashara hizo mitaabi bila leseni kujisalimisha TRA ili wakadiriwe kodi

- Asema amebaini kuwa kuna watu wanafanya biashara hiyo kwa riba kubwa

Zaidi, soma https://jamii.app/WakopeshajiWatakiwaTRA-IRNG
MOSHI: MIUNDOMBINU YAHARIBIKA KUTOKANA NA MVUA KUBWA ILIYONYESHA

- Miti imeanguka katika barabara za Shanty Town, International School na Shule ya Sekondari Mawenzi

- Sehemu nyingine nguzo za umeme zimeanguka na kuharibu miundombinu ya umeme

Zaidi, soma https://jamii.app/MvuaMiundombinuMSH
SHINYANGA: WAGANGA WA JADI 19 MBARONI KWA KUPIGA RAMLI CHONGANISHI

- Ramli hizo zinadaiwa kusababisha mauaji ya Wananchi kutokana na imani potofu za kishirikina

- Pia wamekamatwa na nyara za Serikali ikiwemo mikia ya nyumbu na ngozi ya kenge

Zaidi, soma https://jamii.app/WagangaMbaroniJadiSHY
MICHEZO: Mchezo mmoja wa Ligi Kuu nchini England umemalizika ambapo Manchester City imefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Fulham

- City inayofikisha alama 77 magoli yake yamefungwa na Bernardo Silva dakika ya 5 na Sergio Aguero dakika ya 21

- Michezo inayofuata katika Ligi hiyo kwa siku ya leo ni kama inayoonekana pichani

#JFLeo
GAZA: TAKRIBANI WAPALESTINA 33 WAMEJERUHIWA NA JESHI LA ISRAEL

- Wapalestina hao waliokuwa miongoni mwa Waandamanaji wamejeruhiwa katika vurugu zilizozuka kati yao na Jeshi la Israel

- Inaelezwa baadhi walijeruhiwa kwa risasi za moto na baadhi kwa makopo ya gesi ya kutoa machozi

Zaidi, soma https://jamii.app/MaandamaniMwaka1Gaza
MATOKEO-EPL: HUDDERSFIELD YASHUKA DARAJA, MANCHESTER UNITED YASHINDA

- Imekuwa timu ya pili kushuka daraja kabla ya mwezi Machi kuisha kwenye historia ya Ligi baada ya kufungwa na Crystal Palace goli 2-0

- Man. Utd imefanikiwa kupata ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Watford na kuendelea kuweka hai ndoto zake za kumaliza ndani ya nne bora

#JFLeo
KAGERA: POLISI WAKAMATA MALI ZILIVYOPORWA NA MAJAMBAZI

- Mali hizo ni simu za mkononi 9, kompyuta mpakato na chaja yake, begi lenye nguo na pia polisi wamekamata bangi na kisu

- Jeshi la polisi bado linaendelea kuwatafuta majambazi hao

Soma https://jamii.app/PolisiWakamataVituKagera

#JFLeo