JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MANCHESTER UNITED YAMPA OLE GUNNAR SOLSKJAER MKATABA WA KUDUMU

- Amepewa mkataba wa miaka mitatu baada ya kukabidhiwa timu hiyo kama kocha wa muda Desemba 2018 alipotimuliwa Jose Mourinho

- Tangu akabidhiwe timu hiyo ameshinda michezo 14 kati ya 19 aliyoiongoza

#JFLeo
TUNDU LISSU AANDIKA BARUA YA KUDAI POSHO NA MSHAHARA WAKE

> Amemwandikia barua Katibu wa Bunge akitaka malipo hayo yafanyike ndani ya siku 14 vinginevyo ataenda Mahakamani

> Katibu wa Bunge, Stephen Kigaigai akana kupokea barua hiyo

Soma > https://jamii.app/LissuVsKatibuBunge
JE, WAIJUA HISTORIA YA NENO DALADALA?

> Miaka 1980 kulikuwa na shida ya usafiri Dar, nauli ikaongezeka na kufikia shilingi 5

> Makondakta walianza kuita 'Kariakoo dala dala!' maana shilingi 5 ilikuwa sawa na dola 1 ya Marekani

Soma > https://jamii.app/HistoriaDaladala

#JFHistoria
RAIS MAGUFULI ATEMBELEA NDEGE YA SERIKALI INAYOPAKWA RANGI YA ATCL

- Ndege hiyo aina ya Foker 50 iliyokuwa inabeba Viongozi inabadilishwa iwe ya ATCL na ianze kubeba abiria

- Mapema leo akiwa Ikulu, Rais amesema kuwa upakaji rangi wa ndege hiyo umegharimu Tsh. Milioni 5
KESI YA MEMBE DHIDI YA MUSIBA YAPIGWA KALENDA

- Bernad Membe amefika Mahakama Kuu kwa ajili ya kesi ya madai ya fidia ya Tsh. Bilioni 10 dhidi ya Cyprian Musiba

- Imeahirishwa baada ya Musiba kuomba muda wa kuwasilisha majibu dhidi ya Membe

Soma https://jamii.app/KesiMembe-MusibaYaahirishwa
DURBAN, AFRIKA KUSINI: MAGARI 7 YATEKETEZWA NA MOTO KATIKA GHASIA ZA MGOMO WA MADEREVA

> Mgomo wa madereva wa magari ya mizigo ulianza Jumapili ktk viunga vya KwaZulu-Natal

> Madereva wazawa wanadai wageni wanachukua kazi zao

Soma > https://jamii.app/MgomoMaderevaSA
BURUDANI: JE, NI NINI KIMESABISHA MUZIKI WA DANSI USHUKE?

> Kuanzia miaka ya 1970 hadi miaka ya katikati ya 2000 muziki wa dansi ulisikika na kujizolea mashabiki kila kona ya nchi

> Lakini kwa sasa bendi nyingi zimesambaratika ama wanamuziki wake kufanya kazi ya kuimba kwenye baa ili kupata pesa ya kujikimu

#JFBurudani
LISHE BORA: 35% YA WATOTO CHINI YA MIAKA 5 NCHINI WAMEDUMAA

- Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani(WFP) nchini, Michael Dunford amesema hali hiyo inachangiwa na matumizi ya nafaka pekee katika kuandaa lishe ya Watoto

Soma https://jamii.app/LisheDuniWatotoWadumaa

#JFLeo #LisheBora
BOEING YATANGAZA MATENGENEZO KATIKA NDEGE ZAKE AINA YA 737 MAX

- Imetangaza mabadiliko kwenye mfumo wake wa kuzuia ajali unaohusishwa na ajali mbili za ndege za aina hiyo

- Itaweka mfumo wa kuashiria ajali ambao awali ulikua si wa lazima

Zaidi, soma https://jamii.app/MatengezoBoeing737Max
SOMALIA: MLIPUKO WA BOMU WAUA WATU 15

> Gari iliyotegwa bomu imelipuka karibu na Hoteli moja iliyopo Mji Mkuu Mogadishu. Al-Shabaab watuhumiwa kuhusika

> Watu 17 wamekimbizwa Hospitali baada ya kujeruhiwa katika mlipuko huo.

Zaidi, soma => https://jamii.app/BomuLaua15Somalia
BANGLADESH: BINTI AJIFUNGUA MAPACHA SIKU 26 BAADA YA KUJIFUNGUA MTOTO MMOJA

> Imeelezwa kuwa Binti huyo wa miaka 20 alianza kujisikia maumivu makali yasiyo ya kawaida ndipo alipoelezwa kuwa anaujauzito wa kujifungua

Zaidi kuhusu kisa hiki, soma > https://jamii.app/MimbaAjabu
MWANZA: SERIKALI YAFUNGA MACHIMBO YA UDONGO YALIYOUA MTU MMOJA

- Ni machimbo ya udongo wa kutengeneza majiko ya mkaa katika eneo la milima ya Mabumbani

- DC wa Nyamaghana, Dkt. Philis Nyimbi amesema eneo hilo ni hatarishi na si salama

Soma https://jamii.app/MachimboUdongoYafungwaMWZ
KILOSA, MOROGORO: ASKARI MAGEREZA ADAIWA KUMUUA RAIA

- Lepeli Mandero(20) anadaiwa kuuawa na Askari Magereza baada ya kuingiza mifugo kwenye shamba la gereza la Mbigiri

- Baba wa Marehemu amegoma kumzika mwanae hadi uchunguzi utakapofanyika

Zaidi, soma https://jamii.app/AskariAdaiwaKuua-Kilosa
MABARAZA NA BODI ZA MITIHANI AFRIKA MASHARIKI YAUNGANA

- Waanzisha umoja wa nchi za Afrika Mashariki katika tathmini ya elimu

- Katibu Mkuu wa NECTA, Dkt. Charles Msonde ameteuliwa kuwa Rais wa Umoja huo huku Katibu akitokea Uganda

Zaidi, soma https://jamii.app/MabarazaEAYaungana
KENYA: AKIRI KULAWITI MTOTO MMOJA KATI YA 9 ALIOKUWA ANATUHUMIWA

- Mtuhumiwa David Mutuku Katuku alikiri hayo mbele ya Mahakama ya Kaunti ya Machakos

- Anatuhumiwa kunyanyasa kijinsia Watoto katika kituo cha kulea watoto cha ‘Martyrs of Uganda’

Zaidi, soma https://jamii.app/MwaumeAmlawitiMtoto-KE
KIGOGO PCCB MBARONI

Mkurugenzi wa Mipango wa TAKUKURU, Kulthum A. Mansoor anayetuhumiwa kuwadhulumu viwanja wafanyakazi wa taasisi hiyo, amekamatwa na kufikishwa Kituo cha Polisi Oysterbay

> Sept 2018, Rais Magufuli aliagiza ashughulikiwe

Zaidi, soma https://jamii.app/KigogoPCCB
COMORO: KIONGOZI WA UPINZANI AKAMATWA, RISASI ZARINDIMA KATIKA KAMBI YA JESHI

> Ni saa chache baada ya wagombea wa upinzani kuunda Baraza la Mpito na kupanga kumtoa Rais Assoumani madarakani wakidai hajashinda kwa haki katika Uchaguzi wa Machi 24

Zaidi, soma https://jamii.app/KiongoziUpinzaniAkamatwaCMR
OMBI LA NASSARI KUFUNGUA KESI DHIDI YA SPIKA LAKATALIWA

- Mahakama Kuu Dodoma yakubali mapingamizi ya Serikali na kukataa ombi lake la kufungua kesi ya msingi dhidi ya Spika wa Bunge na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya kupinga kuvuliwa Ubunge

Zaidi, soma https://jamii.app/NassariAshindwaKesiUbunge
LUGOLA: WALIOPANGA KUVURUGA AMANI ZANZIBAR WATAKAMATWA KAMA KUKU

- Asema kuna watu wanaoaminika ni Vyama vya Siasa kumbe ni magenge ya wanasiasa wanaotaka kuvuruga amani

- Asisitiza watakamatwa mmoja mmoja kabla mipango yao haijatekelezwa

Zaidi, soma https://jamii.app/WaletaVuruguKukamatwaZNZ