JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MAAFA YA KIMBUNGA MSUMBIJI: IDADI YA VIFO YAHOFIWA KUFIKIA 1,000

> Kimbunga hicho kililikumba Jiji la Beira lililopo katika pwani ya nchi hiyo.

> Kimbunga 'Idai' kinaelezwa kuwa kilikuwa na kasi ya Kilomita 177 kwa saa

Zaidi, soma => https://jamii.app/CycloneIdai1000

#JFLeo
THAILAND: ASKARI POLISI WAPELEKWA KAMBI YA KUPUNGUZA UZITO

> Jumla ya Askari 200 wamehusika kwenye progamu hiyo ya majaribio ya wiki mbili

> Kupitia programu hiyo wapo Askari waliopungua uzito kutoka kilo 80 hadi 60

Zaidi, soma => https://jamii.app/ThaiPorkyPolisi

#JFInternational
HISTORIA: LITI KIDANKA MWANAMKE SHUJAA ALIYEILINDA NGOME YA WANYATURU KWA NYUKI

> Ni Liti Lerti Kidanka aliyewaongoza watu wa kabila la Wanyaturu Mkoani Singida katika mapambano dhidi ya utawala wa Kijerumani

Kupata historia hii adhimu,fungua > https://jamii.app/LetiKidanka

#JFHistoria
MVUA KUBWA NA THELUJI VYASABABISHA MAAFA MAREKANI

> Mvua kubwa na theluji vimesababisha vifo vya watu wawili huku wengine wawili wakiwa hawajulikani walipo

> Mamlaka zinaendelea na shughuli zake za utafutaji na uokoaji katika maeneo yaliyoathirika na mafuriko

Soma - https://jamii.app/FloodsDeathUS
#JFInternational
WALIOLIPWA FEDHA ZA KOROSHO KUBANDIKWA KWENYE OFISI ZA VIJIJI

> Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga ameagiza kubandikwa kwa majina ya wakulima wote waliolipwa fedha za Korosho na kiasi walicholipwa ikiwa ni hatua ya kuondokana na taarifa potofu zinazotolewa na baadhi yao kuwa hawajalipwa na kuichafua Serikali

Soma - https://jamii.app/MajinaMalipoKorosho
#JFLeo
HIVI NDIVYO SHERIA INAVYOMLINDA MTOTO ANAYEFANYA KAZI ZA NYUMBANI

> Ingawa sheria inasema Mtoto mwenye miaka 14 ana haki ya kufanya kazi, inakwenda mbali kutaka aajiriwe kufanya ‘kazi nyepesi’ na kupata malipo stahiki

Zaidi, soma > https://jamii.app/WatotoAjira

#JFCivicSpace
WAKIMBIZI WADAIWA KULA CHAKULA CHA MSAADA CHENYE SUMU

> Shirika la chakula duniani, WFP limesitisha shughuli ya kugawanya chakula cha misaada kwa wakimbizi nchini Uganda baada ya madai kuibuka kuwa watu 2 wamefariki na wengine zaidi ya 200 kulazwa katika Hospitali ya Karamoja Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo baada ya kutumia unga wa uji unaodaiwa kuwa na sumu

> Shirika la msalaba mwekundu limeripoti kuwa waathiriwa wanaonesha ishara za kuugua ugonjwa wa akili huku wengi wao wakilalamika kuumwa tumbo

Soma - https://jamii.app/SumuChakulaWFP
#JFLeo
MAFURIKO INDONESIA: TAKRIBANI WATU 89 WAFARIKI

> Idadi hiyo inaweza kuongezeka kutokana na mamia ya watu kutokujulikana walipo tangu kutokea kwa janga hilo

> Idadi ya majeruhi mpaka sasa ni 150 huku waliookolewa ni 6,800

Soma > https://jamii.app/MafurikoIndonesia

#JFInternational
WALIOKUWA VIONGOZI WAANDAMIZI WA CUF WAPEWA KADI ACT WAZALENDO

> Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo amemkabidhi Maalim Seif kadi namba 1 na Juma Haji Duni namba 10

> Ismail Jussa, Mbalala Maharangande na Sheweji Mketo nao wakabidhiwa

Soma > https://jamii.app/MaalimKadiACT

#JFLeo
KENYA YAKUMBWA NA BAA LA NJAA

> Serikali ya Kenya inasema Kaunti zaidi ya 10 nchini humo zinakabiliwa na baa la njaa kutokana na ukame unaosababishwa na kukosekana kwa mvua

> Kaunti ya Turkana ndipo kumeathiriwa zaidi ambapo vifo tayari vimeanza kuripotiwa

Soma - https://jamii.app/NjaaKaunti10KE
#JFInternational
TANZANIA YATOA MSAADA WA CHAKULA NA DAWA

> Msaada huo ni kwa Msumbiji, Zimbabwe na Malawi zilizokumbwa na janga la kimbunga

> Kimbunga hicho kimepelekea mafuriko makubwa yaliyosababisha idadi kubwa ya vifo na uharibifu wa miundombinu

Soma > https://jamii.app/TzYatoaMsaada

#JFLeo
GLOOMY SUNDAY: WIMBO UNAODAIWA KUSABABISHA ZAIDI YA WATU 100 WAJIUE

> Uliotungwa mwaka 1933 na Rezso Seress, msanii kutoka Hungary. Alitunga maneno ya wimbo huo na kupiga ala ya huzuni ikiwa ni baada ya kuachwa na mpenzi wake

Kwa kisa hiki, soma > https://jamii.app/GloomySundayVifo
UFAHAMU KUHUSU 'PROCESSOR' YA SIMU

> Processor katika simu ni kifaa ambacho huchukua maelezo kutoka kwenye software na kufanya kazi za kimahesabu na kimantiki pamoja na kutoa na kuingiza vitu ili simu yako ifanye kazi kwa ufanisi

> Simu nyingi zinatumia processor aina ya 'arm' na wana aina yao ya processor inayoitwa 'A series' ambayo ndiyo inatumika sana kwenye simu na inajumuisha; cortex A5, A6, A7, A8, A9, A12 na A15

Zaidi, tembelea - https://jamii.app/ProcessorSimu
#JFTeknolojia
LIPUMBA: MAALIM SEIF HAJAHAMA CHAMA BALI ALIFUKUZWA

> Mwenyekiti wa CUF Taifa, Prof. Ibrahim Lipumba amesema kuwa kabla ya Maalim Seif kukihama chama hicho tayari alikuwa ameshafukuzwa kuwa mwanachama wa CUF kwenye mkutano mkuu uliopita, baada ya kubaini hana nia njema na chama na anataka kukidhoofisha

> Amewataka wanaotaka kumfuata Maalim Seif kuchanganya akili zao na kutokurupuka

Soma - https://jamii.app/LipumbaVsMaalimCUF
#JFLeo
VITU VYA KUZINGATIA UNAPOTAKA KUNUNUA KOMPYUTA

> Waranti: Hii itakusaidia wewe mtumiaji kupata msaada pale kifaa kitakapopata matatizo kama hujaiharibu mwenyewe unaweza kubadilishiwa ukapewa nyingine

> Processor: Kuna tofauti kubwa sana kati ya processor za single core kama pentium processors, duo-core, na quad core processors. Kwa mtumiaji wa kawaida processor za intel i3 inamtosha, watumiaji wa kati i5 na kwa wale wakubwa i7 ndio ya kwao

> RAM: Kwa watumiaji wadogo RAM ya 2Gb ni kubwa kutosha matumizi yote ila watumiaji wakubwa hasa wale 'professionals' wanatakiwa kutumia kuanzia 4 - 6 GB

Fahamu zaidi - https://jamii.app/MuongozoKununuaPC
#JFTeknolojia
MTOTO AMUUA MPENZI WA MAMAKE

> Mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika Kijiji cha Deriat kaunti ya Kericho, Kenya amemuua mzee (65) kwa kumchoma kisu kifuani baada ya kumkuta akishiriki tendo la ndoa na mama yake

> Adai huyo si babake na hivyo hana mamlaka ya kulala nyumbani kwao

Soma - https://jamii.app/AuaMpenziMama
#JFInternational
MATUMIZI YA SIMU YACHANGIA DOLA BILIONI 2.5 KATIKA UCHUMI WA TANZANIA

> Simu zimerahisisha huduma za mawasiliano, uzalishaji, na kuchangia kwenye pato la taifa

> Ajira kwa watu milioni 1.5 sawa na 2.6% ya idadi ya Watanzania zimetengenezwa

Soma > https://jamii.app/TzDigitalIndustry

#JFLeo
MTOTO WA MWAKA MMOJA AFIA KWENYE DIMBWI LA MAJI

> Mtoto Alex Fredrick Sanga, mwaka mmoja na miezi saba, Mkazi wa Mapinduzi, Mkoani Mbeya amekutwa amefariki kwenye korongo lenye maji ambalo lipo jirani na nyumbani kwao

> Marehemu alikuwa akicheza na wenzake wakati mama yake akifua na baada ya muda akatoweka

Soma - https://jamii.app/MtotoKifoDimbwi
#JFLeo
MAMA AMCHOMA MTOTO WAKE KWA MAJI MOTO

> Mkazi wa Kijiji cha Ndachi Mkoani Dodoma, Asha Juma anashutumiwa kwa kosa la kumchoma mwanae, Godfrey Banda (13) mikono kwa maji ya moto kwa kile kilichoelezwa kuwa ni udokozi wa nyama

Soma - https://jamii.app/AchomaMtotoMaji
#JFLeo
BUKOBA: BASI LA KAMPUNI YA FRESTER LALIGONGA BASI LA DAR LUX

> Ajali imetokea baada ya basi la Frester lililokuwa likitoka Bukoba kuelekea Mwanza kuligonga basi la Kampuni ya Dar Lux lililokuwa likielekea Dar

> Abiria wachache wamejeruhiwa

Soma > https://jamii.app/FresterVsDarLuxBukoba

#JFLeo