JamiiForums
52.9K subscribers
34.3K photos
2.43K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Maoni ya Jaji Mstaafu, Barnabas Samatta kuhusu uwezekano wa Rais Mstaafu kushtakiwa
Maoni ya Jaji Mstaafu, Barnabas Samatta kuhusu “Mahakama ya Mafisadi”
RAIS MAGUFULI AITAKA TBA KUTOA MAELEZO YA MATUMIZI YA BILIONI 10

> Rais Magufuli amefanya ziara ya kushtukiza katika mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi ya Askari Magereza wa Gereza la Ukonga, Dar

> Ameagiza mradi huo ukabidhiwe kwa JWTZ

Soma > https://jamii.app/RaisMagufuliVsTBA

#JFLeo
SENETA APIGWA KWA UBAGUZI WA DINI

> Seneta Fraser Anning wa Queensland, Australia amepigwa na yai na kijana mmoja baada ya kudai Waislamu wanaohamia New Zealand ndio chanzo cha shambulio lililotokea Msikini na kuua watu 49

Soma > https://jamii.app/NZSenator

#JFInternational
SHAMBULIO LA KIGAIDI, NEW ZEALAND: IDADI YA WALIOFARIKI YAFIKIA 50

- Idadi hiyo inafikiwa huku majeruhi wawili wakiwa katika hali mbaya

- Aidha, waliojeruhiwa pia ni 50 huku 36 miongoni mwao wakiwa bado wamelazwa hospitalini

Zaidi, soma https://jamii.app/DeathTollRises50-NWZLND
PAPUA, INDONESIA: TAKRIBANI WATU 50 WAMEFARIKI KWA MAFURIKO

- Maafisa wa Serikali wamesema idadi hiyo inaweza kuongezeka wakati uokoaji ukiendelea

- Mafuriko hayo yaliyosababishwa na mvua kubwa na maporomoko ya ardhi yamejeruhi watu wengine 50

Zaidi, soma https://jamii.app/FloodsIndonesia-Machi2019
ARDHI KUSAJILIWA KIELEKTRONIKI KWA SHILINGI 5,000

- Wizara ya Ardhi imezindua mpango wa kusajili kila kipande cha ardhi na kutoa leseni au hati ya kieletroniki itakayodumu miaka mitano

- Kuanza Dar es Salaam na kisha kuendelea mikoa yote

Zaidi, soma https://jamii.app/ElectronicLandLicence
MARA: MALIGHAFI ZISIZO NA KIBALI ZA KUTENGENEZEA POMBE ZAKAMATWA

- Kituo cha Forodha Sirari kimekamata mapipa 386 ya lita za ujazo 96,500 yenye malighafi ya thamani ya Tsh. Milioni 246.6

- Yalikuwa yakisafirishwa kinyemela kwenda Kenya

Zaidi, soma https://jamii.app/MalighafiZakamatwaSirari
NASSARI ASEMA ATAENDA MAHAKAMANI ASIPOPATA HAKI YAKE

- Asema hakuhudhuria Bunge la Novemba 2018 na Januari 2019 kutokana na mke wake kuwa na matatizo ya kiafya

- Asema alimtaarifu Spika kupitia anuani aliyopewa na Msaidizi wa Spika

Zaidi, soma https://jamii.app/NassariAongeaKuvuliwaUbunge
TANZIA: WAKILI SHUKURU MLWAFU AFARIKI

- Amefariki dunia leo nyumbani kwake jijini Dodoma baada ya kuugua kwa muda mrefu

- Alikuwa akifundisha sheria UDOM na ndiye aliyefungua kesi kupinga Wafanyakazi kukatwa 15% ya mshahara na HESLB

Zaidi, soma https://jamii.app/WakiliMlwafuAfariki
SERIKALI YAAHIDI KUMALIZA MALIPO YA KOROSHO KABLA YA MACHI 31, 2019

> Yasema uhakiki umekamilika kwa kiasi kikubwa ikiwemo kuwabaini 'Kangomba' wote

> Hadi sasa Tani 222,684 zimekusanywa na Sh. Bilioni 596.9 kati ya Bilioni 723 zimeshalipwa

Zaidi, soma https://jamii.app/MalipoKoroshoMachi31
TAKRIBANI WATU 150 WAMEFARIKI KUTOKANA NA KIMBUNGA

- Mamia wengine hawajulikani walipo baada Kimbunga Idai kuzikumba nchi za Malawi, Msumbuji na Zimbabwe

- Aidha, zaidi ya watu Milioni 1.5 wameathiriwa na Kimbunga hicho katika nchi hizo tatu

Zaidi, soma https://jamii.app/KimbungaChauaZimbabwe
GEITA: UKUSANYAJI WA MADUHULI SEKTA YA MADINI WAONGEZEKA

- Kati ya mwaka 2011 hadi 2018 ukusanyaji wa maduhuli katika sekta ya madini umetoka Tsh. Bilioni 24 hadi Tsh. Bilioni 114.7

- Moja ya sababu ni mabadiliko ya kisheria yenye manufaa

Zaidi, soma https://jamii.app/UkusanyajiMaduhuliMadiniWapanda
KENYA: WAKILI AMPIGA RISASI MWANAE NA KUMUUA

- Wakili Assa Kibagedi anasema alimpiga mwanae risasi kwa bahati mbaya akiwa anaihifadhi silaha ndani ya gari walimokuwepo wote

- Wakili huyo kwa sasa yupo kituo cha Polisi huku tukio hilo likiendelea kuchunguzwa zaidi

Zaidi, soma https://jamii.app/WakiliAuaMwanaeKNY
WATUMISHI 12 NJOMBE KUKAMATWA KWA TUHUMA ZA UBADHILIFU

> Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka ameagiza kukamatwa kwa watumishi 12 akiwemo Mkurugenzi wa Halmashauri kwa ubadhilifu wa Tsh bilioni 5.5 za ujenzi wa kituo cha mabasi

Soma - https://jamii.app/WatumishiKamatwaUbadhilifu
#JFLeo
GEITA YAPATA SOKO LA MADINI, WATOROSHAJI KUADHIBIWA KISHERIA

> Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ametoa tahadhari kwa wadau wote wa madini kuwa atakayekamatwa anatorosha madini, atachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo utaifishaji wa madini atakayokuwa akiyatorosha

> Ametoa tahadhari hiyo jana wakati akifungua soko la madini la Mkoa wa Geita ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais Magufuli la kuitaka mikoa yote ianzishe masoko ya madini

Soma - https://jamii.app/SokoMadiniGeita
#JFLeo
MAHAKAMA KUU YAMTAMBUA PROF LIPUMBA KAMA MWENYEKITI HALALI WA CUF

> Kesi ilifunguliwa na Bodi ya Wadhamini wa chama hicho wanaomuunga mkono Maalim Seif baada ya Msajili wa Vyama vya Siasa kudai anamtambua Lipumba kama Mwenyekiti halali

Soma > https://jamii.app/MahakamaKuuLipumba

#JFLeo
MALI ZA MANJI ZAZUILIWA KUTOKANA NA DENI LAKE NBC

> Mahakama Kuu imezuia mali za mfanyabiashara maarufu nchini, Yusuph Manji kutokana na madeni anayodaiwa na Benki ya NBC

> Anadaiwa zaidi ya Tsh bilioni 25 ambazo hajazirejesha kwa wakati

Soma - https://jamii.app/ZuioManjiNBC
#JFLeo
JESHI LA POLISI LAUA MTU MMOJA AKIDAIWA KUWA JAMBAZI

> Jeshi la Polisi Wilayani Muheza Mkoani Tanga limemuua kwa kumpiga risasi Mkazi wa Dar es Salaam, Mwinyiheri Nuhu, akidaiwa alikuwa akijihusisha na ujambazi

> Yeye na wenzake walivamia nyumba ya Mfanyabiashara Ally Nassoro Wilayani Muheza wakiwa na bunduki juzi usiku na kupora Tsh. milioni moja

Soma - https://jamii.app/JambaziKifoPolisi
#JFLeo