JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
RAIS MSTAAFU ANAWEZA KUFUNGULIWA MASHTAKA NA OFISI YA DPP

> Haya yameelezwa na Jaji Mkuu Mstaafu, Barnabas Samatta katika Mjadala wa Uwajibikaji uliandaliwa na Taasisi ya Wajibu Institute katika Chuo cha Sheria Tanzania(Law School of Tanzania) Jijini Dar es Salaam

> Jaji Samatta amefafanua kuwa Rais mstaafu ana kinga lakini ina mipaka. Kinga haihusu mambo aliyofanya akiwa Rais bali yale aliyofanya kama Rais

#JFLeo
MTUHUMIWA WA MAUAJI YA NEW ZEALAND AFIKISHWA MAHAKAMANI

> Mshukiwa wa shambulio lililotokea jana jijini Christchurch, na kuua watu 49, Brenton Terrant (28) tayari amefikishwa Mahakamani

> Wengine wawili bado wanahojiwa na Polisi

Soma - https://jamii.app/MosqueShootingSuspect
#JFInternational
WALEMAVU WA MIGUU KUPEWA VIUNGO VYA BANDIA BURE

> Walemavu wa viungo vya miguu 600 wanatarajiwa kufanyiwa uchunguzi na kupatiwa miguu bandia katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI)

> Uchunguzi kwa wagonjwa utafanyika mwezi Aprili na wale watakaotakiwa kutumia viungo hivyo watapewa mwezi Mei

Soma - https://jamii.app/MiguuBandiaBure
#JFLeo
WAZAZI NA JAMII WATAJWA KUWA CHACHU YA ONGEZEKO LA RUSHWA

> Watajwa kupokea fedha nyingi toka kwa watoto wao bila maelezo na kuwa kichocheo cha kuendelea kwa ulaji rushwa miongoni mwa watumishi wa umma

> Pia tabia ya kumuona kijana wao asiyetajirika haraka kama mjinga na asiyejituma imekuwa ikiwafanya watumishi kujikita katika vitendo vya rushwa

Soma - https://jamii.app/WazaziJamiiRushwa
PROF. LIPUMBA ATANGAZA MAKATIBU WAKUU WA CUF TAIFA

> Amemtangaza ndugu Khalifa Suleiman Khalifa kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho

> Pia amtangaza Magdalena Sakaya Naibu Katibu Mkuu kwa upande wa Tanzania Bara

Soma => https://jamii.app/MakatibuCUFTaifa

#JFLeo
Maoni ya Jaji Mstaafu, Barnabas Samatta kuhusu uwezekano wa Rais Mstaafu kushtakiwa
Maoni ya Jaji Mstaafu, Barnabas Samatta kuhusu “Mahakama ya Mafisadi”
RAIS MAGUFULI AITAKA TBA KUTOA MAELEZO YA MATUMIZI YA BILIONI 10

> Rais Magufuli amefanya ziara ya kushtukiza katika mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi ya Askari Magereza wa Gereza la Ukonga, Dar

> Ameagiza mradi huo ukabidhiwe kwa JWTZ

Soma > https://jamii.app/RaisMagufuliVsTBA

#JFLeo
SENETA APIGWA KWA UBAGUZI WA DINI

> Seneta Fraser Anning wa Queensland, Australia amepigwa na yai na kijana mmoja baada ya kudai Waislamu wanaohamia New Zealand ndio chanzo cha shambulio lililotokea Msikini na kuua watu 49

Soma > https://jamii.app/NZSenator

#JFInternational
SHAMBULIO LA KIGAIDI, NEW ZEALAND: IDADI YA WALIOFARIKI YAFIKIA 50

- Idadi hiyo inafikiwa huku majeruhi wawili wakiwa katika hali mbaya

- Aidha, waliojeruhiwa pia ni 50 huku 36 miongoni mwao wakiwa bado wamelazwa hospitalini

Zaidi, soma https://jamii.app/DeathTollRises50-NWZLND
PAPUA, INDONESIA: TAKRIBANI WATU 50 WAMEFARIKI KWA MAFURIKO

- Maafisa wa Serikali wamesema idadi hiyo inaweza kuongezeka wakati uokoaji ukiendelea

- Mafuriko hayo yaliyosababishwa na mvua kubwa na maporomoko ya ardhi yamejeruhi watu wengine 50

Zaidi, soma https://jamii.app/FloodsIndonesia-Machi2019
ARDHI KUSAJILIWA KIELEKTRONIKI KWA SHILINGI 5,000

- Wizara ya Ardhi imezindua mpango wa kusajili kila kipande cha ardhi na kutoa leseni au hati ya kieletroniki itakayodumu miaka mitano

- Kuanza Dar es Salaam na kisha kuendelea mikoa yote

Zaidi, soma https://jamii.app/ElectronicLandLicence
MARA: MALIGHAFI ZISIZO NA KIBALI ZA KUTENGENEZEA POMBE ZAKAMATWA

- Kituo cha Forodha Sirari kimekamata mapipa 386 ya lita za ujazo 96,500 yenye malighafi ya thamani ya Tsh. Milioni 246.6

- Yalikuwa yakisafirishwa kinyemela kwenda Kenya

Zaidi, soma https://jamii.app/MalighafiZakamatwaSirari
NASSARI ASEMA ATAENDA MAHAKAMANI ASIPOPATA HAKI YAKE

- Asema hakuhudhuria Bunge la Novemba 2018 na Januari 2019 kutokana na mke wake kuwa na matatizo ya kiafya

- Asema alimtaarifu Spika kupitia anuani aliyopewa na Msaidizi wa Spika

Zaidi, soma https://jamii.app/NassariAongeaKuvuliwaUbunge
TANZIA: WAKILI SHUKURU MLWAFU AFARIKI

- Amefariki dunia leo nyumbani kwake jijini Dodoma baada ya kuugua kwa muda mrefu

- Alikuwa akifundisha sheria UDOM na ndiye aliyefungua kesi kupinga Wafanyakazi kukatwa 15% ya mshahara na HESLB

Zaidi, soma https://jamii.app/WakiliMlwafuAfariki
SERIKALI YAAHIDI KUMALIZA MALIPO YA KOROSHO KABLA YA MACHI 31, 2019

> Yasema uhakiki umekamilika kwa kiasi kikubwa ikiwemo kuwabaini 'Kangomba' wote

> Hadi sasa Tani 222,684 zimekusanywa na Sh. Bilioni 596.9 kati ya Bilioni 723 zimeshalipwa

Zaidi, soma https://jamii.app/MalipoKoroshoMachi31
TAKRIBANI WATU 150 WAMEFARIKI KUTOKANA NA KIMBUNGA

- Mamia wengine hawajulikani walipo baada Kimbunga Idai kuzikumba nchi za Malawi, Msumbuji na Zimbabwe

- Aidha, zaidi ya watu Milioni 1.5 wameathiriwa na Kimbunga hicho katika nchi hizo tatu

Zaidi, soma https://jamii.app/KimbungaChauaZimbabwe
GEITA: UKUSANYAJI WA MADUHULI SEKTA YA MADINI WAONGEZEKA

- Kati ya mwaka 2011 hadi 2018 ukusanyaji wa maduhuli katika sekta ya madini umetoka Tsh. Bilioni 24 hadi Tsh. Bilioni 114.7

- Moja ya sababu ni mabadiliko ya kisheria yenye manufaa

Zaidi, soma https://jamii.app/UkusanyajiMaduhuliMadiniWapanda
KENYA: WAKILI AMPIGA RISASI MWANAE NA KUMUUA

- Wakili Assa Kibagedi anasema alimpiga mwanae risasi kwa bahati mbaya akiwa anaihifadhi silaha ndani ya gari walimokuwepo wote

- Wakili huyo kwa sasa yupo kituo cha Polisi huku tukio hilo likiendelea kuchunguzwa zaidi

Zaidi, soma https://jamii.app/WakiliAuaMwanaeKNY