JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MFUMUKO WA BEI MWEZI FEBRUARI WABAKI 3% HUKU VYAKULA VIKISHUKA BEI

- Ofisi ya Takwimu(NBS) imebainisha kuwa asilimia hizo ni sawa na Januari 2019

- Inamaanisha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma haijabadilika kwa miezi miwili

Zaidi, soma https://jamii.app/MfumukoBei-Feb2019
IRAN: WAPENZI WAKAMATWA BAADA YA KUCHUMBIANA HADHARANI

- Ni kwa kukiuka maadili ya kidini ambapo kuonesha hadharani mapenzi kumepigwa marufuku nchini humo

- Polisi imedai kitendo hicho kimechochewa na utamaduni wa mataifa ya Magharibi

Zaidi, soma https://jamii.app/MbaroniKuchumbianaHadharani-IRN
TCRA YAFICHUA ‘MADUDU’ VITUO VYA REDIO KANDA YA ZIWA

> Yawapa miezi 4 kurekebisha mapungufu mbalimbali yaliyobainika walipofanya ukaguzi kwenye vituo takribani 36

> Wafanyakazi hawana mikataba, wana elimu zisizokidhi na baadhi ya vituo havina vyoo

Zaidi, soma https://jamii.app/TCRA-RedioKandaZiwa
COLOMBIA: WATU 14 WAMEFARIKI KATIKA AJALI YA NDEGE

- Imepata ajali jana huko San Carlos de Guaroa ikiwa inatokea San Jose del Guaviare kuelekea Villavicencio

- Ni muda mchache baada ya rubani kutuma ishara ya dharura kwa kituo cha udhibiti

Zaidi, soma https://jamii.app/14WafaAjaliNdege-CLMB
NDEGE YA SHIRIKA LA NDEGE LA ETHIOPIA YAPATA AJALI, WENGI WAHOFIWA KUFARIKI

- Boeing 737 imepata ajali ikiwa safarini kutoka Addis Ababa, Ethiopia kuelekea Nairobi, Kenya

- Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, ndege hiyo ilikuwa na abiria 149 pamoja na Wafanyakazi 8

Zaidi, soma https://jamii.app/ETHAirlines-Boeing737Crashes
WATU WOTE KWENYE NDEGE ILIYOPATA AJALI LEO ETHIOPIA WAFARIKI

> Ni 157, idadi ikijumuisha abiria 149 na wafanyakazi 8 wa ndege

> Imetajwa kuwa na raia kutoka nchi 33 tofauti

> Sababu za ajali bado hazijafahamika

Zaidi, soma https://jamii.app/ETHAirlines-Boeing737Crashes
ALGERIA: WANAFUNZI WA VYUO WAPEWA LIKIZO YA MAPEMA

- Ni ili kudhoofisha maandamano ya Wanafunzi hao ambao wanapinga Rais Abdelaziz Bouteflika kugombea kwa muhula wa 5

- Likizo hiyo huwa ya wiki 2 kuanzia Machi 21 hadi Aprili 5 kila mwaka

Zaidi, soma https://jamii.app/VyuoVyafungwaMapemaALG
MANUFAA YA KULA WADUDU KIAFYA NA KIMAZINGIRA

> Wana virutubisho karibu vyote yaani protini, madini mengi na asidi za amino

> Pia wanaweza kula taka, hawatoi gesi zinazoongeza joto duniani, hawahitaji maji mengi wala eneo kubwa la kuwafuga

Zaidi, soma https://jamii.app/FaidaKulaWadudu
SERIKALI: WAPINZANI WANAOMTUKANA RAIS KWENYE VIKAO VYA NDANI WAKAMATWE

- Waziri Lugola ametoa agizo hilo kwa Polisi akiwataka washirikiane na Wakuu wa Mikoa na Wilaya

- Asema baadhi ya wapinzani wanatukana, wanabeza na kuchonganisha Wananchi na Serikali

Zaidi, soma https://jamii.app/WapinzaniWanaotukanaWakamatwe
SHINYANGA: AUAWA KATIKA UGOMVI WA RABA

> Daniel Gudugudu(30) ameuawa kwa kuchomwa kisu kwenye mkono wa kushoto na Rashid Mustapha(48) huko Nyihogo wilayani Kahama

> Chanzo cha tukio hilo ni ugomvi uliotokana na kudaiana viatu aina ya raba zenye rangi nyeusi

Zaidi, soma https://jamii.app/MauajiKisuSHY
NHC KUWAFUKUZA WADAIWA SUGU KATIKA MAJENGO YAKE

- Ni kwa wale walioshindwa kulipa kodi ya pango ya jumla ya Tsh. Milioni 44.3

- Ni mpango wa kutaka kumaliza kukusanya kodi ambapo hadi sasa shirika limekusanya zaidi ya Tsh. Bilioni 1.9(73%)

Zaidi, soma https://jamii.app/WadaiwaNHCKuondolewa
TUNISIA: WAZIRI AJIUZULU KUTOKANA NA VIFO VYA WATOTO

> Waziri wa Afya, Abdurrauf esh-Sherif amejiuzulu baada ya kutokea vifo 11 vya watoto ktk Hospitali ya Serikali mjini Tunis

> Uchunguzi unafanyika kubaini sababu ya vifo hivyo

Soma - https://jamii.app/WaziriAjiuzuluVifoWatoto
#JFInternational
SERIKALI YATAKA TAARIFA ZA WAAJIRI WALIOFUKUZA KAZI WANAWAKE BAADA YA KUPATA UJAUZITO

> Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ametaka apewe taarifa hasa za sekta binafsi za waliowafukuza Wanawake kazi au kuwashusha vyeo kwa sababu wamepata ujauzito

Soma > https://jamii.app/UjauzitoKazi

#JFLeo
CHINA, ETHIOPIA ZASITISHA KUTUMIA BOEING 737 MAX 8

> China imeyaamuru mashirika ya ndege ya ndani ya nchi kusimamisha matumizi ya ndege aina ya Boeing 737 MAX 8 kufuatia ajali iliyotokea Ethiopia na nyingine nchini Indonesia

> Shirika la ndege la Ethiopia nalo limetangaza kusitisha safari za ndege zake zote aina ya Boeing 737 Max 8 kuanzia Machi 10 mwaka huu kama tahadhari ya ziada licha ya kuwa bado chanzo cha ajali iliyotokea jana na kuua watu 157 bado hakijafahamika mpaka sasa

Soma - https://jamii.app/ChinaBansBoeing737
#JFInternational
UINGEREZA: MBUNGE AITUHUMU QATAR KWA KUTOA RUSHWA FIFA

> Taifa la Qatar linatuhumiwa kutoa kiasi cha zaidi ya Shilingi za Kitanzania Bilioni 937 kwa FIFA ili ipewe uenyeji wa Kombe la Dunia mwaka 2022

Zaidi, soma => https://jamii.app/FIFAQatarScandal

#JFLeo
AJINYONGA BAADA YA UGOMVI NA SHANGAZI KUHUSU CHAPATI

> Binti Sharon (20), mkazi wa Kisumu, Kenya, amejinyonga hadi kufa baada ya ugomvi na shangazi yake kuhusu chapati

> Alitumia fedha ya chakula cha familia kujinunulia chapati na maharage

Soma - https://jamii.app/BintiAjinyongaChapati
#JFLeo
MPANDA, KATAVI: WANAFUNZI WALALA BWALONI BAADA YA BWENI KUTEKETEA KWA MOTO

> Ni Wanafunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Msaginya wamelazimika kulala katika bwalo la chakula tangu mabweni yao yateketee kwa moto wiki iliyopita

Zaidi, soma => https://jamii.app/WanafunziWalalaBwaloni

#JFLeo
MAKAMU WA RAIS KUMUWAKILISHA RAIS KWENYE MKUTANO WA ANS UGANDA

> Samia Suluhu anaondoka nchini leo kuelekea Kampala kwenye Mkutano wa "Africa Now Summit"

> Atazungumzia mada ya Uongozi unaohitajika kuchochea mabadiliko ya Kijamii na Uchumi Afrika

Soma - https://jamii.app/SamiaMkutanoANS
#JFLeo
MWENDELEZO: KISANDUKU CHA TAARIFA KUTOKA NDEGE YA ETHIOPIA CHAPATIKANA

> Kisanduku(Black Box) cha kurekodia taarifa za ndege wakati wa safari kilichokuwa cha ndege ya Boeing 737 MAX 8 iliyoanguka na kuua watu 157 chapatikana

Soma => https://jamii.app/ETHAirlines-Boeing737Crashes

#JFInternational