JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
VENEZUELA: RAIS WA MPITO AKABILIWA NA KIFUNGO CHA MIAKA 30

> Kiongozi wa upinzani Venezuela, Juan Guaidó, anaandamwa na kifungo cha miaka 30 baada ya kukiuka agizo la kumtaka asitoke nje ya nchi, lililotolewa na Mahakama ya Juu

Soma - https://jamii.app/GuaidoJail30Yrs
#JFInternational
SEHEMU YA KIWANDA CHA BORA YATEKETEA KWA MOTO

> Janga hilo limekikumba kiwanda hicho cha Viatu kilichopo maeneo ya TAZARA jijini Dar

> Kikosi cha zima moto tayari kimefika eneo la tukio na kuendelea na juhudi za uokoaji

Zaidi, soma => https://jamii.app/MotoKiwandaBora
BARIADI: MTU MMOJA AMEFARIKI BAADA YA KUANGUKIWA NA KIFUSI CHA MGODI

> Aidha, watu wengine watatu pia wanahofiwa kufariki katika mgodi huo

> Tukio hilo limetokea katika mgodi wa dhahabu wa Burambaka uliopo katika Kijiji cha Gasuma

Soma => https://jamii.app/MgodiBurambaka

#JFLeo
NJOMBE: WATU 4 AKIWEMO MTOTO WA MIAKA 15 KUFIKISHWA MAHAKAMANI KWA MAUAJI

> Mtoto David Kasila mwenye umrinwa miaka pamoja na Mariano Malekela, Edwin Malekela na Kalistus Costa wanatarajiwa kufikishwa mahakamani Machi 4, 2019

Zaidi, soma => https://jamii.app/MtotoMauajiNjombe

#JFLeo
JESHI LA POLISI LINAMSHIKILIA MSANII DUDU BAYA

> Msanii Godfrey Tumaini maarufu 'Dudu Baya' anashikiliwa na Jeshi la Polisi katika Kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam kwa mahojiano

> Anatuhumiwa kumkashfu na kutoa lugha za kejeli kwa marehemu, Ruge Mutahaba
TRUMP AKATAA KUIONDOLEA VIKWAZO KOREA KASKAZINI

> Rais wa Marekani, Donald Trump alitoka katikati ya mkutano na Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un baada ya Kim kuitaka Marekani kuiondolea nchi yake vikwazo vyote ilivyoiwekea

Soma - https://jamii.app/UsVsNorthKorea
#JFInternational
MAJARIBIO YA CHANJO YA UKIMWI NCHINI YALETA MATUMAINI

> Utafiti wa awali wa chanjo ya UKIMWI umeonesha kuwa, ina uwezo wa kusisimua na kufanya mwili wa binadamu utengeneze kinga dhidi ya ugonjwa huo

> Chanjo hiyo ilitengenezwa nchini Sweden

Zaidi https://jamii.app/ChanjoUKIMWITanzania
KIWANDA CHA MABEHEWA KUJENGWA NCHINI

> Mkurugenzi wa kampuni ya Kiluwa Group, Mohammed Kiluwa amefanya makubaliano na Kampuni ya Afrika Jambo Group ya Afrika Kusini kujenga kiwanda cha mabehewa nchini kitakachogharimu dola milioni 150

Soma - https://jamii.app/UjenziKiwandaMabehewa
#JFLeo
BIASHARA: Wanawake wafanyabiashara ndogo ndogo wakigomea kulipa ushuru wa Tsh. 500

> Wanawake hao wameeleza kuwa hawawezi kulipa ushuru huo kwakuwa tayari wametimiza sharti la kuwa na vitambulisho vya Serikali

#JFBiashara
UCHUMI: BOT YATOA TAARIFA BAADA YA UKAGUZI WA MADUKA YA KUBADILISHIA FEDHA, DAR

> Benki Kuu yasema imebaini maduka mengi hayafanyi kazi hiyo kwa kufuata kanuni na taratibu zilizowekwa

> BOT imeanza kuyafutia leseni za biashara maduka hayo

Soma > https://jamii.app/BOTVsForexDar

#JFUchumi
HATMA RUFAA YA MBOWE NA MATIKO KUJULIKANA KESHO

> Hatma ya dhamana ya Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko inatarajiwa kujulikana kesho Machi Mosi, ambapo uamuzi utatolewa na Mahakama ya Rufani kuhusu rufaa aliyokata DPP

Soma - https://jamii.app/HukumuRufaaMbowe
#JFLeo
ELIMU YA URAIA: JE, UNAWEZA KUMUOMBA POLISI AKUSAIDIE MATATIZO YA KIFAMILIA?

> Inawezekana kama tatizo ikiwa lina asili ya kijinai

> Iwapo kinachotokea ni uhalifu kama kumpiga vibaya mwanamke/mtoto, au wanandugu kujamiiana

Zaidi, soma > https://jamii.app/Mambo101Polisi

#JFCivicSpace
HISTORIA YA MASHUJAA NA MAKUMBUSHO YA VITA VYA MAJIMAJI

> Vita ya Maji Maji vilivyotokea kati ya Mwezi Julai 1905 mpaka Agosti 1907 na ilianza katika vilima vya Umatumbi Kaskazini mwa mji wa Kilwa na kiongozi aliitwa Kinjeketile

> Watu hawa walipigana kupinga kukandamizwa na kulazimishwa na Wakoloni wa Kijerumani namna ya kuishi, mazao ya kuzalisha na nani wa kumtumikia

> Jina la vita limetokana na imani ya matumizi ya dawa iliyochanganywa na Maji, punje za Mahindi

Tembelea - https://jamii.app/HistoriaVitaMajimaji
#JFHistoria
HISTORIA YA VITA VYA KAGERA (TANZANIA NA UGANDA)

> Vita kati ya Tanzania na Uganda, au Vita ya Kagera ilidumu kwa miezi sita kuanzia Novemba 1978 hadi Aprili 1979 na ndiyo iliyouangusha utawala wa Iddi Amin Dada uliodumu kwa muda wa miaka 8

> Vita hiyo ilianza rasmi siku ya maadhimisho ya Uhuru wa Uganda, Oktoba 9, 1978 baada ya mwanajeshi wa Uganda kuvuka mpaka na kuingia Tanzania kukutana na mpenzi wake ambaye alikuwa raia wa Tanzania

Fahamu zaidi - https://jamii.app/HistoriaVitaKagera
#JFHistoria
DEREVA WA MWENDOKASI KIZIMBANI KWA KUMKATA ABIRIA KIDOLE

> Khalid Shaha(43), amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni kujibu shtaka la kumkata kidole Godfrey Liwa kwa kioo cha gari

> Amekana shtaka hilo na kuachiwa kwa dhamana

Soma > https://jamii.app/DARTMahakama
#JFLeo
BALOZI ZA NCHI MBALIMBALI NCHINI ZALAANI KUFUNGIWA KWA GAZETI LA THE CITIZEN

> Wasema wamezoea kupata habari kutoka kwenye gazeti hilo kila siku asubuhi

> Wahoji, adhabu hiyo inaendana na kosa wanalotuhumiwa?

#JFLeo #JFCivicSpace