JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
WAZIRI MKUU: MPAKA WA HOLILI HAUKO SALAMA, NJIA ZA PANYA ZIMEKITHIRI

> Amesema mpaka huo kati ya Tanzania na Kenya uliopo wilayani Rombo(Kilimanjaro) una njia nyingi za panya zinazotumiwa wahalifu kupitisha silaha na bidhaa za magendo

Soma > https://jamii.app/MajaliwaMpakaHolili

#JFLeo
BAADHI YA SIFA ZINAZOWASILISHWA ILI KUMJUA MTU ANAYEKUFAA KIMAPENZI

> Hatangoja kujua nini unahitaji kwa kuwa hana sababu ya kusubiri kuombwa ndiyo atoe msaada

> Ni yule atakayejua wakati gani huna furaha au una furaha na atakuwa na wewe katika hali ya raha na shida pia

> Atakupenda kwa moyo wake wote na wala si kwa ajili ya shinikizo fulani (pesa au mali) na ataonesha kuthamini nafasi yako mbele ya wengine

Zaidi, soma - https://jamii.app/SifaMpenziKweli
#JFMahusiano
MICHEZO: Klabu ya Barcelona yainyuka Sevilla kwa mabao 4 kwa 2

> Mshambualiaji raia wa Argentina, Lionel Messi afunga mabao 3 maarufu kama 'hat-trick'

> Hii ni hat-trick ya 32 kwa Messi tangu aanze kuitumikia Klabu ya Barcelona ktk La Liga

> Messi amebakiza hat-trick 2 ili kuifikia rekodi iliyowekwa na Cristiano Ronaldo aliyefunga 34 akiwa na Real Madrid

#JFSports
WATAALAMU 9 WA ARDHI WAPOTEZA MAISHA KWENYE AJALI

> Watu 9, wataalam wa idara ya Ardhi wamefariki baada ya gari aina ya Land Cruiser walilokuwa wakisafiria kutumbukia mtoni Wilayani Kilombero mkoani Morogoro

> Gari hiyo ilikuwa na watu 13

Soma - https://jamii.app/WataalamuArdhiWafariki
MTWARA: KOROSHO ZARUDISHWA KWA WAKULIMA ZIKIDAIWA HAZINA UBORA

- Zaidi ya tani 68 za korosho zimekataliwa kuingizwa kwenye maghala makuu ya TANECU ili ziuzwe

- Wakulima wamedai pamoja na kuzichambua na kuzianika zikubaliwe bado zimekataliwa

Zaidi, soma https://jamii.app/WakulimaWarudishiwaKorosho
KOCHA WA YANGA ASEMA ANAWEZA KUONDOKA MWISHO WA MSIMU HUU

- Kocha Mwinyi Zahera amesema anaweza kuondoka kutokana na Wanachama na Mashabiki kutompa ushirikiano

- Aidha, zipo tetesi zinazodai kuwa Kocha huyo anaenda kuifundisha klabu ya Azam

Zaidi, soma https://jamii.app/ZaheraAtishiaKuondoka
MKURUGENZI HALMASHAURI YA ROMBO APEWA SIKU 16 KUTOA TSH. MILIONI 114

- Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza Mkurugenzi Magreth John, apeleke fedha hizo katika kijiji cha Holili

- Ni 20% ya mauzo ya madini ya pozolana ambayo Wananchi wanadai hawajalipwa

Zaidi, soma https://jamii.app/FedhaMadiniHoliliKLM
SERIKALI: MFANYABIASHARA MDOGO ANAYEGOMA KUCHUKUA KITAMBULISHO ATALIPA KODI

> Yasema kama Tsh. 20,000/- zinaonekana nyingi wanaweza kulipa kwa awamu

> Viongozi waonywa kutotoa kitambulisho kabla ya mfanyabiashara kumaliza malipo kuepusha kutoroka

Zaidi, soma https://jamii.app/VitambulishoUmachingaVsKodi
RAIS WA KOREA KASKAZINI ATUMIA TRENI KWENDA KUKUTANA NA RAIS TRUMP

- Kim Jong Un anakwenda Vietnam kushiriki kikao chake cha pili na Rais wa Marekani, Donald Trump

- Kikao kitafanyika Februari 27 na Februari 28, 2019 katika mji mkuu wa Vietnam, Hanoi

Zaidi, soma https://jamii.app/Kim-TrumpSummit
ISRAEL YATUMA CHOMBO KWENDA MWEZINI

> Kimeitwa Beresheet kikimaanisha "Mwanzo" kwa lugha ya Kiyahudi na kinatarajiwa kutua mwezini Aprili 11, 2019

> Kimebeba Biblia ya dijitali, Bendera na wimbo wa Taifa la Israel na michoro ya Watoto

Zaidi, soma https://jamii.app/IsraelChomboMwezini-2019
DEREVA ALIYEFARIKI KATIKA AJALI ILIYOUA WATU 19 SONGWE KUSHTAKIWA

- Kamanda wa Usalama barabarani, Fortunatus Muslim ameagiza hivyo iwapo dereva atakutwa na makosa

- Pia, mmiliki wa lori anatakiwa kujibu tuhuma za kuruhusu gari bovu kutembea barabarani

Zaidi, soma https://jamii.app/DerevaAliyefarikiKushtakiwa
ALGERIA: MAMIA WAANDAMANA KUPINGA RAIS BOUTEFLIKA KUGOMBEA URAIS

- Wanapinga Rais wa sasa Abdelaziz Bouteflika aliyeiongoza nchi hiyo tangu mwaka 1999, kugombea tena kwa awamu ya 5 katika uchaguzi ujao

- Hata hivyo, Rais huyo anaonekana atashinda kutokana na Upinzani kuwa dhaifu na kugawanyika

Zaidi, soma https://jamii.app/AlgeriansVsPresBouteflika
KOCHA WA YANGA AKANA KUTAKA KUJIUNGA NA AZAM FC

- Kocha Mwinyi Zahera amesema habari hizo zinazozunguka kwenye mitandao ya kijamii ni za uongo na za hovyo

- Amesema hajawasiliana na Kiongozi yeyote wa klabu ya Azam na wala hawafahamiani

Zaidi, soma https://jamii.app/ZaheraAtishiaKuondoka
KENYA: WIZARA YA ARDHI YASHINDWA KUELEZEA MATUMIZI YA TSH. BILIONI 46O

- Ripoti ya mwaka 2017/18 ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali imebainisha hivyo

- Imeelezwa kuna utofauti uliodhahiri na Makadirio yasiyo sahihi katika taarifa za fedha za Wizara hiyo

Zaidi, soma https://jamii.app/Ksh20bnHazionekaniWizarani
HALIMA MDEE AACHIWA KWA DHAMANA BAADA YA SAA 24

- Mbunge huyo wa Kawe(CHADEMA) alikuwa akishikiliwa katika Kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar

- Alikamatwa akidaiwa kutoa maneno ya uchochezi katika mkutano wa hadhara alioufanya Februari 21, 2019

Zaidi, soma https://jamii.app/MdeeApataDhamana-Feb2019
TATIZO LA KUKOSA USINGIZI (INSOMNIA) NA TIBA YAKE

> Hutokana na upungufu wa homoni, magonjwa mbalimbali, msongo wa mawazo

> Wenye tatizo wanashauriwa kutumia asali mbichi vijiko viwili kila usiku

Zaidi, soma https://jamii.app/TatizoKukosaUsingizi
MICHEZO: Klabu ya Manchester United ikiwa nyumbani imelazimishwa sare ya bila bila na Klabu ya Liverpool katika mchezo wa Ligi Kuu nchini England

- Kwa matokeo haya Man Utd inafikisha alama 52 ikiwa nafasi ya 5 huku Liverpool akiendelea kuongoza Ligi akiwa na alama 66
AMCHOMA MOTO MTOTO MIKONONI KWA MADAI YA KUDOKOA CHAKULA

- Polisi mkoani Dodoma inamshikilia Eliza Deni(23) kwa tuhuma za kumfanyia hivyo mtoto wake wa kambo, Jackson Denis(5)

- Atafikishwa Mahakamani kujibu shtaka hilo siku za hivi karibuni

Zaidi, soma https://jamii.app/MtotoAchomwaMotoDOM-2019
MANCHESTER CITY IMEFANIKIWA KUTETEA UBINGWA WA CARABAO CUP

- Imefanikiwa kuchukua ubingwa huo baada ya kuigaragaza klabu ya Chelsea kwa penati 4-3

- Klabu hizo zilimaliza dakika 90 zikiwa hazijafungana na kusababisha kwenda hatua hiyo ya matuta
KONDOA, DODOMA: WATUHUMIWA WA UJAMBAZI WAUAWA

> Wameuawa kwa kupigwa na Wananchi wa kijiji cha Kinyasi baada ya kuvamia kituo cha mafuta

> Walifanya uporaji wa zaidi ya shilingi milioni kumi katika kituo hicho

Zaidi, soma => https://jamii.app/MajambaziKondoa

#JFLeo