JamiiForums
βœ”
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
FUATILIA TAARIFA ZA KIRUSI CHA OMICRON KUTOKA VYANZO SAHIHI

Jamii inashauriwa kupata taarifa za #CoronaVirus pamoja na Kirusi kipya kwa Wataalamu wa Afya na vyanzo vinavyoaminika

Usisambaze taarifa mpya mpaka ujiridhishe imethibitishwa

Soma - https://jamii.app/TaarifaChanjo

#UVIKO3
SUDAN: Waziri Mkuu wa Sudan, Abdalla Hamdok ametaka kuwepo Makubaliano ya Kisiasa ili kulinda Taifa hilo

Maandamano zaidi yamepangwa kufanyika leo kuadhimisha miaka mitatu ya maandamano yaliyopelekea Omar al-Bashir kupinduliwa

Soma - https://jamii.app/SudanHamdok
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Prof. Abel Makubi amewaasa Wazazi kutopeleka watoto maeneo ya mikusanyiko isiyo ya lazima ili kupunguza hatari ya kupata maambukizi ya #COVID19

> Abiria wametakiwa kuelimishwa hatari ya kujazana ktk mabasi

Soma https://jamii.app/Dec25UVIKO

#UVIKO3
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Prof. Abel Makubi amewaasa wanaosafiri kwenda vijijini kwa sherehe za mwisho wa mwaka kuwalinda wazee dhidi ya maambukizi ya #COVID19

> Amesema kwa sasa visa vya maambukizi vinaongezeka kwa kasi

Soma https://jamii.app/WazeeVijijini
#UVIKO3
DR-CONGO: Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Jeshi la Uganda yametangaza kufanikiwa kuharibu ngome muhimu za Waasi wa ADF zilizopo Jimbo la Kivu na Ituri huko Kaskazini mwa DRC

> Kampeni dhidi ya ADF ilianza Novemba 30

Soma https://jamii.app/UgandaDRCWaasi
#JFLeo
Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) linaongoza kikao cha kujadili uwezekano wa Kombe la Dunia kufanyika kila baada ya Miaka 2 badala ya 4 ya sasa

CAF inaunga mkono mabadiliko hayo, lakini Mashirikisho ya Soka Ulaya na Kusini mwa #America yanapinga

Soma - https://jamii.app/TimeWorldCup
#Sports
SERIKALI: 80% YA WATANZANIA WALIOUGUA COVID-19 HAWAKWENDA HOSPITALI

Wizara ya Afya kupitia Ofisi ya Mpango wa Taifa wa Chanjo imesema 5% ya waliougua walifikishwa ICU

> Bado mwamko wa Chanjo unasuasua hasa Mikoa ya Kanda ya Ziwa

Soma https://jamii.app/WatzHospCorona
#UVIKO3
Wizara ya Afya imekanusha taarifa za uwepo wa wimbi la 4 la #COVID19 na kusema kuwa ongezeko la maambukizi halimaanishi uwepo wa wimbi hilo

> Imesema uwepo wa Wimbi jipya ni pale ongezeko la maambukizi linapokuwa kwa kipindi cha siku 14-21

Soma https://jamii.app/TzOmicron
#UVIKO3
UFILIPINO: Idadi ya vifo kutokana na Kimbunga kikali kilichoipiga Nchi hiyo imeongezeka kufikia Watu 375

Watu wengine 56 bado hawajulikani walipo, takriban Watu 380,000 wameyakimbia makazi yao huku wengine 500 wakijeruhiwa

Soma - https://jamii.app/DeathsStormPhill
#Philippines
UINGEREZA: Kutokana na Mataifa mengi kuweka ulazima wa Cheti cha uthibitisho wa kuchanjwa imebainika Matapeli wanawarubuni Watu kupitia #Facebook ili kuwauzia Vyeti feki

Facebook imesema itaondoa ujumbe wowote utakaobainika kufanya hivyo

Soma - https://jamii.app/FakeCoronaCards
#UVIKO3
#OMICRON: Wizara ya Afya ya #India imerekodi maambukizi 200 ya Omicron na maambukizi 5,326 ya aina nyingine za Virusi vya #COVID19 kwa saa 24 zilizopita

Aidha, vifo vipya 453 vimeripotiwa na kufanya idadi ya vifo kufikia 478,007

Soma https://jamii.app/OmicronIndia
#UVIKO3
Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), imebaini 42.1% ya Watu walio na Shinikizo la Damu ambalo huambatana na tatizo la kukoroma wako hatarini kukosa pumzi usingizini

Pia, Watu wanaougua Kisukari, wenye Mzio, Uzito uliopindukia na upana wa shingo uliokithiri, nao wamo hatarini kiafya kwa kukosa hewa usingizini

Soma - https://jamii.app/KoromaPumzi
#Afya
CHINA YAFUTA AKAUNTI ZA MITANDAO YA KIJAMII YA β€˜MALKIA WA MITANDAO’

Huang Wei mwenye wafuasi zaidi ya Milioni 110 afutiwa akaunti zake kwa tuhuma za kukwepa kodi

Anatuhumiwa kuuza vitu vya thamani ya takribani Tsh. Trilioni 3.07 bila kulipa kodi

Soma - https://jamii.app/MalkiaWaMitandao
UCHAGUZI WA LIBYA MASHAKANI. KAMATI ZA UCHAGUZI ZAVUNJWA SIKU 2 KABLA

Desemba 24, ni Siku ambayo Walibya kwa mara ya kwanza wangepata nafasi ya kuchagua Rais

Kuvunjwa Kamati hizo kunamaanisha uwezekano wa kufanyika Uchaguzi ni mdogo

Soma https://jamii.app/ElectionLibya

#ElectionLibya
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
GHANA: Wabunge wametwangana makonde #Bungeni baada ya kutokea ubishani wakati wa mjadala juu ya Sheria ya tozo ya Miamala ya Kidijitali

Ugomvi huo ulianza baada ya Mbunge wa Upinzani kumzuia Msaidizi wa Spika kunyanyuka kwenda kupiga kura

Soma - https://jamii.app/TozoGhanaMPs
#JFLeo
UMOJA WA ULAYA WAPITISHA SHERIA MPYA ZA USAFIRI

Cheti cha #COVID19 cha Umoja huo ni halali kutumika kwa Wasafiri kwa miezi tisa baada ya kukamilika kwa Chanjo

Sheria hizo mpya zitaanza kutumika katika Mataifa 27 ya Wanachama kuanzia Februari 1. Mataifa yatalazimika kuruhusu Wasafiri waliopata Chanjo kamili kuingia katika maeneo yao

Soma - https://jamii.app/EUWasafiri
#UVIKO3
πŸ‘1
UGANDA: WABUNGE 38 WALIOKUWA ARUSHA WAKUTWA NA CORONA

Safari ya Wabunge zaidi ya 200 na Wafanyakazi 125 imeingia doa baada ya kurudi kutoka kwenye mashindano ya Wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Jijini Arusha na kukutwa na #COVID19

Soma - https://jamii.app/MPUGCoronaAR

#UVIKO3
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imekipiga faini ya Tsh. milioni 2 Kituo cha Televisheni cha Wasafi kwa kosa la kurusha maudhui yaliyokashifu imani ya Kikristo

Pia, wametakiwa kuomba radhi watazamaji kuanzia Desemba 23 hadi 25 mara tatu kwa siku kila baada ya saa nne kwa kosa hilo

Soma - https://jamii.app/WasafiFainiTCRA
#JFLeo
SERIKALI YAILIPA PSSSF TSH. TRILIONI 2.17

Serikali imeanza kulipa madeni kwa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) ili Wastaafu wasisumbuke kupata stahiki zao

Deni lililobaki litaendelea kulipwa kwa mfumo wa Hati Fungani

Soma - https://jamii.app/DeniPSSSF

#JFLeo
Kikao cha 18 cha Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kimekubali Mchakato wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuwa Mwanachama

Baraza la Mawaziri EAC laagizwa kuanza mazungumzo na DR Congo kwa ajili ya kujiunga na Jumuiya hiyo

Soma - https://jamii.app/DRCEAC

#JFLeo