JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
NDEJEMBI: TIMU ZINAPOFUNGWA NA YANGA ZIKUBALIANE NA MATOKEO

- Akiwa Bungeni Dodoma, Naibu Waziri wa Utumishi na Utawala Bora amesema baadhi ya Viongozi wa Timu wamekuwa wakitoa kauli ya kwamba walihongwa hususan wanapofungwa na Yanga

Soma > https://jamii.app/RushwaSoka

#Sports
BURKINA FASO: TAKRIBAN WANAKIJIJI 30 WAUAWA

- Wanamgambo wanaosadikika wa kundi la Jihad wamevamia kijiji cha Kodyel na kufanya mauaji hayo

- Mashambulio yameongezeka Nchini humo katika Mikoa inayopakana na #Niger na #Mali

Soma > https://jamii.app/MauajiBurkinafaso

#HumanRightsViolations
ETHIOPIA: MZOZO WA #TIGRAY KUTENGANISHA WATOTO NA WAZAZI WAO

- Zaidi ya #Watoto 5,000 watenganishwa na wazazi wao kutokana na mapigano yanayoendelea

- Watoto hao wako ktk hatari ya kupata njaa, kunyanyasika kimwili na kingono

Soma > https://jamii.app/WatotoTigray
NDALICHAKO: SERIKALI ITAONDOA TOZO YA 6% YA KULINDA THAMANI KTK MIKOPO YA ELIMU JULAI 1

- Pia, Serikali imeiagiza Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi kuondoa tozo ya adhabu ya 10% ambayo inatozwa kwa wanaochelewa kulipa Mikopo

Soma - https://jamii.app/TozoMikopoElimu
MBUNGE: WIZARA YA ELIMU IKUBALI MFUMO UNA TATIZO

- Akiwa Bungeni, Bernadeta Mushashu amesema Wizara ifungue mjadala mpana tuangalie kitu gani kinakosekana na tuongeze nini

- Pia, ametoa wito kwa Serikali kuweka mkakati wa kuajiri Walimu

Soma > https://jamii.app/MfumoElimu
LIGI YA MABINGWA ULAYA: NANI KUTINGA FAINALI, MAN CITY AU PSG?

- Mchezo wa pili wa Nusu Fainali kati ya Manchester City dhidi ya PSG kuchezwa hii leo majira ya saa 4:00 usiku

- Mchezo wa kwanza katika hatua hiyo Manchester City iliibuka na ushindi wa goli 2-1

- Ili kutinga Fainali PSG inahitaji kushinda si chini ya magoli 2-0 wakati Man City ikihitaji sare au ushindi wowote
MBUNGE: WATOTO 15 KATI YA 45 DARASANI HAWAFUNDISHIKI

- Neema Lugangira amesema suala la Lishe Shuleni linapaswa kupewa uzito, na hali ya Udumavu inachangia Watoto kutofaulu na kufundishika kwa kiasi kikubwa

Soma > https://jamii.app/WatotoLishe
SIMBACHAWENE: KITAMBULISHO CHA NIDA HAKIHALALISHI KUWA RAIA WA TANZANIA

- Waziri huyo ameeleza Uraia wa Tanzania una #Sheria na mchakato wake

- Kitambulisho ni kwa ajili ya kuwatambua Watu na hutolewa hata kwa Wakimbizi na Wahamiaji wakazi

Soma - https://jamii.app/NIDAUraia
JOSE MOURINHO ATANGAZWA KUWA KOCHA MPYA WA AS ROMA

- AS Roma ya Italia imemtangaza Mourinho (58) kuwa Kocha wake ikiwa ni wiki mbili tangu kibarua chake kiote nyasi akiwa Tottenham

- Amesaini kandarasi ya miaka mitatu na ataanza kuinoa AS Roma mwanzoni mwa msimu ujao

#JFSports
MEXICO: 23 WAFARIKI NA 70 WAJERUHIWA BAADA YA BARABARA YA JUU KUPOROMOKA

- Sehemu ya barabara ya juu iliporomoka na kusababisha treni kuanguka ktk barabara ya chini iliyokuwa na watu wengi

- Kiwango cha barabara hiyo kimewahi kulalamikiwa

Soma > https://jamii.app/AjaliMexico