JamiiForums
βœ”
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
NEC: MSIMAMIZI ATAKAYESABABISHA UCHAGUZI KURUDIWA ATALIPA FIDIA

> NEC itamchukulia hatua Msimamizi atakayefanya vitendo vitakavyosababisha Uchaguzi kuharibika ktk Jimbo au Kata kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Soma https://jamii.app/UchaguziJimbo
#Uchaguzi2020
TAKUKURU: NI MARUFUKU WAPIGA KURA KULA PILAU KWA WAGOMBEA WATAKAOSHINDA

> Mkuu wa TAKUKURU Geita amesema kitendo hicho ni kupokea rushwa ya vyakula

> Pia, aliyeshinda hawezi kuleta maendeleo kwasababu amemalizana na Wananchi kwenye Pilau

Soma - https://jamii.app/TAKUKURUPilauRushwa
#TZ2020
PROF. LIPUMBA: NITABORESHA BEI YA KOROSHO

> Mgombea Urais JMT kupitia CUF, Prof. Ibrahim Lipumba ameahidi kuboresha sekta muhimu za #Uchumi na #Kilimo

> Asema maendeleo ya Viwanda hutanguliwa au kuambatana na Mapinduzi ya Kilimo

Soma https://jamii.app/LipumbaKorosho
#Uchaguzi2020
NEC: WAGOMBEA MSIWE NA MATOKEO MFUKONI

> Mkurugenzi wa Uchaguzi, Dkt. Wilson Mahera amesema baadhi ya Wagombea wanajiaminisha kuwa wameshashinda

> Amesema NEC itahakikisha inatenda haki na kuwatangaza Wagombea watakaoshinda kihalali

Soma https://jamii.app/NECMatokeoWagombea
#Uchaguzi2020
NEC YASEMA HAINA TAARIFA YA MGOMBEA YEYOTE WA URAIS KUJITOA

> NEC imeeleza kuwa, kutofanya Kampeni kwa baadhi ya Wagombea wa Urais hakuwaondolei sifa ya kugombea

> Wagombea wote waliopitishwa watakuwepo ktk karatasi za kupigia kura

Soma https://jamii.app/NECWagombeaUrais
#Uchaguzi2020
DR. CONGO: ZAIDI YA WAFUNGWA 900 WATOROKA GEREZANI

> Wafungwa 900 wametoroka Gereza la Beni baada ya Wapiganaji kuvamia na kushambulia wakiwemo wa Kikundi cha Waasi cha ADF

> Kwa takwimu za UN, ADF imeua zaidi ya watu 1,000 tangu 2019

Soma https://jamii.app/Wafungwa900DRC
#JFLeo
TANZIA: MKURUGENZI MWENDESHAJI WA SHIRIKA LA TAIFA LA MAENDELEO AFARIKI DUNIA

> Prof. Damian Gabagambi afariki dunia Oktoba 20 ktk Hospitali ya Taifa ya Muhimbili

> Aliteuliwa na Rais kuwa Mkurugenzi Mwendeshaji wa NDC Machi 23, 2018

Soma https://jamii.app/ProfGabagambi
TANZANIA YAKOPA ZAIDI YA BILIONI 115 KUPAMBANA NA ATHARI ZA #COVID19

> AfDB imepitisha mkopo wa Dola Milioni 50.7 kwa #Tanzania

> Kwa mujibu wa AfDB, fedha hizo zitasaidia mpango wa Serikali wa takriban Bilioni 252 kupambana na #CoronaVirus

Soma https://jamii.app/MkopoCoronaTZ
#JFLeo
IGP SIRRO: POLISI IPO KUSIMAMIA HAKI, HAIPENDELEI

> Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Simon Sirro amesema Wanasiasa wasihofu, Polisi watampigia saluti yeyote atakayechaguliwa

> Pia, amewataka Wanasiasa watimize wajibu ili wasiingize Taifa ktk uhalifu

Soma https://jamii.app/IGPSirroHaki
#TZ2020
MAPISHI: JIFUNZE JINSI YA KUPIKA VITUMBUA

> Mahitaji ni mchele, tui zito la nazi, ute wa yai, unga wa sembe na wa ngano, hamira, hiliki na sukari

> Saga mchele na tui mpaka uwe laini. Tia yai, hamira na hiliki huku ukiendelea kusaga kisha weka sukari. Weka unga wa ngano na wa sembe na saga tena kidogo

> Weka kwenye chuma cha vitumbua na uanze kuchoma mpaka uone vimebadilika rangi

Soma https://jamii.app/MapishiVitumbua
RIPOTI: 85% YA WAFANYAKAZI WA NDANI WANADHALILISHWA NCHINI #QATAR

> Shirika la Amnesty International limearifu 85% ya Wanawake huporwa hati za kusafiri wanapowasili nchini humo

> Hunyimwa mishahara, chakula, hutemewa mate, hupigwa na kunyanyaswa kingono

Soma https://jamii.app/QataraWafanyakazi
NEC: HATUTARAJII KUONA MTU ANATANGAZA MATOKEO NJE YA UTARATIBU

> Tume ya Uchaguzi imesema Mamlaka ya kutangaza matokeo ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani yametolewa kwa Tume, Wasimamizi pamoja na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi

Soma https://jamii.app/MamlakaUchaguziNEC
#TZ2020
JOHN FUMBO: VYAMA VISIVYO NA WABUNGE VINATESEKA KWA KUKOSA RUZUKU

> Mgombea Urais kupitia DP amesema, wanakosa hata nauli za kuwafikisha Mawakala maeneo ya kuapishwa

> Ashauri fedha ziwe zinatolewa kwa Vyama vyote vinavyoshiriki Uchaguzi

Soma https://jamii.app/DPUkataUchaguzi
#TZ2020
DP: WASICHANA WATAKAOPATA UJAUZITO WATARUDI SHULENI

> Chama hicho kimesema endapo kitashinda, waliopata ujauzito watajifungua na kurudi Shule kwa kuwa elimu ni haki yao ya msingi

> Pia, kimeahidi kutoa elimu bure kikipata ridhaa ya kuongoza

Soma https://jamii.app/AhadiZaDP
#TZ2020
DKT. MAGUFULI AWAOMBA RADHI WATU WA MWANGA KWA KUCHELEWESHA MRADI WA MAJI

> Amewaomba radhi Wananchi wa Mwanga, Same na Korogwe kutokana na kutokamilika kwa mradi ambao ulitakiwa kukamilika 2017

> Ameahidi kusimamia mradi huo yeye mwenyewe

Soma https://jamii.app/MagufuliKilimanjaro
#TZ2020
ZANZIBAR: CCM YAWASILISHA MALALAMIKO ZEC BAADA YA WAFUASI WAKE KUSHAMBULIWA

> Naibu Katibu Mkuu wa CCM #Zanzibar amesema matukio hayo yanalenga kuwatisha wafuasi wao kupiga kura

> Asema Siasa za chuki na uhasama zimepitwa na wakati

Soma https://jamii.app/CCMZECZnz
#Uchaguzi2020
WILAYA YA MWANGA KUWA NA HOSPITALI 2 ZA WILAYA

> Mgombea Urais, Dkt. Magufuli ameahidi kufanya Kituo cha Afya cha Mwanga kuwa hospitali ya Wilaya

> Amesema Mwanga ina hospitali ya Wilaya iliyoko Usangi ila hakuna ubaya zikiwa mbili

Soma https://jamii.app/MwangaHospitali
#Uchaguzi2020
AFRIKA KUSINI: HAWKS WAMKAMATA β€˜NABII’ BUSHIRI KWA UTAKATISHAJI FEDHA

> Kitengo cha Uchunguzi wa Makosa ya Jinai (#Hawks) kimemfikisha Mahakamani β€˜Nabii’ Shepherd #Bushiri na mkewe Mary kwa tuhuma za kutakatisha takriban Tsh. Bilioni 14.4

Soma https://jamii.app/NabiiBushiri
ASKOFU KAKOBE: TUCHUNGE NDIMI ZETU, ULIMI UMEKUWA CHANZO KIKUBWA CHA MACHAFUKO

> Amesema maneno yasitamkwe tu kwasababu yanaweza kuwasha moto wa machafuko

> Asema machafuko yanapotokea kila kitu kinasimama ikimaanisha nchi inasimama

Soma https://jamii.app/ViongoziDiniAmani
#Uchaguzi2020