JamiiForums
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
DKT. MAGUFULI: JINA LANGU LIPO NAMBA MOJA, USIHANGAIKE KUANGALIA KWINGINE

> Amewaambia Wananchi wasihangaike kuangalia kwingine kwasababu wale hawawahusu

> Asema, Uchaguzi ni wakati wa kuamua kama wanataka maendeleo au 'blah blah'

Soma - https://jamii.app/JPMKorogwe
#Uchaguzi2020
MAALIM SEIF: TULIKUBALIANA KUMUUNGA MKONO LISSU NA MEMBE AKIWEPO

> Baada ya kuona Kampeni zao zinasuasua, Kamati ya Uongozi ilikutana na Bernard Membe akiwepo

> Membe alitoa tarehe akisema ikifika hajaanza kampeni, ni bora kumuunga Lissu

Soma - https://jamii.app/MaalimMembeLissu
#TZ2020
DKT. MAGUFULI: NI WAKATI WA KUBORESHA MASLAHI YA WAFANYAKAZI

> Amesema "Miaka 5 iliyopita tumeimarisha uchumi, sasa 5 ijayo tutakuwa na jukumu la kuongeza mishahara. Huwezi kupandisha mishahara wakati huna uchumi, wengine wanazungumza tu"

Soma https://jamii.app/MaslahiWafanyakazi
#TZ2020
MAALIM SEIF: WAZANZIBARI WAMECHOKA, WAMEDHAMIRIA KULINDA DEMOKRASIA

> Mgombea Urais wa ACT-Wazalendo amesema wanakwenda tarehe 27 na 28 wakiwa tayari kwa lolote litakalotokea kulinda #Demokrasia na #Haki ya watu kumchagua Rais wanayemtaka

Soma - https://jamii.app/MaalimHakiZnz
#TZ2020
TUME YA UCHAGUZI: KILA MPIGA KURA ARUDI NYUMBANI BAADA YA ZOEZI HILO

> Ofisa Elimu Kitengo cha Mpiga Kura, amesema hakuna mtu atakayeruhusiwa kukaa Mita 100 kusubiri matokeo

> Amesema ni kosa kukiuka utaratibu uliowekwa siku ya kupiga kura

Soma https://jamii.app/KuraMita100
#TZ2020
NEC YAIFUTA ADHABU YA MBATIA KUFUNGIWA KUFANYA KAMPENI

> Mgombea Ubunge wa Vunjo, James Mbatia alizuiliwa kufanya Kampeni kwa siku 7 mpaka Oktoba 23 kwa kutumia kipeperushi cha Kampeni ambacho hakijaidhinishwa na Msimamizi wa Uchaguzi

Soma https://jamii.app/MbatiaAdhabu
#Uchaguzi2020
MGOMBEA URAIS WA UPDP AAHIDI KUTOA HUDUMA ZA AFYA BURE

> Twalib Kadege amesema #Tanzania ina Rasilimali nyingi kama Madini na Hifadhi za Taifa na Serikali inapaswa kukusanya fedha kwenye vyanzo hivyo ili itekeleze sera ya Matibabu bure

Soma https://jamii.app/UPDPHudumaBure
#Uchaguzi2020
NEC: MSIMAMIZI ATAKAYESABABISHA UCHAGUZI KURUDIWA ATALIPA FIDIA

> NEC itamchukulia hatua Msimamizi atakayefanya vitendo vitakavyosababisha Uchaguzi kuharibika ktk Jimbo au Kata kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Soma https://jamii.app/UchaguziJimbo
#Uchaguzi2020
TAKUKURU: NI MARUFUKU WAPIGA KURA KULA PILAU KWA WAGOMBEA WATAKAOSHINDA

> Mkuu wa TAKUKURU Geita amesema kitendo hicho ni kupokea rushwa ya vyakula

> Pia, aliyeshinda hawezi kuleta maendeleo kwasababu amemalizana na Wananchi kwenye Pilau

Soma - https://jamii.app/TAKUKURUPilauRushwa
#TZ2020
PROF. LIPUMBA: NITABORESHA BEI YA KOROSHO

> Mgombea Urais JMT kupitia CUF, Prof. Ibrahim Lipumba ameahidi kuboresha sekta muhimu za #Uchumi na #Kilimo

> Asema maendeleo ya Viwanda hutanguliwa au kuambatana na Mapinduzi ya Kilimo

Soma https://jamii.app/LipumbaKorosho
#Uchaguzi2020
NEC: WAGOMBEA MSIWE NA MATOKEO MFUKONI

> Mkurugenzi wa Uchaguzi, Dkt. Wilson Mahera amesema baadhi ya Wagombea wanajiaminisha kuwa wameshashinda

> Amesema NEC itahakikisha inatenda haki na kuwatangaza Wagombea watakaoshinda kihalali

Soma https://jamii.app/NECMatokeoWagombea
#Uchaguzi2020
NEC YASEMA HAINA TAARIFA YA MGOMBEA YEYOTE WA URAIS KUJITOA

> NEC imeeleza kuwa, kutofanya Kampeni kwa baadhi ya Wagombea wa Urais hakuwaondolei sifa ya kugombea

> Wagombea wote waliopitishwa watakuwepo ktk karatasi za kupigia kura

Soma https://jamii.app/NECWagombeaUrais
#Uchaguzi2020
DR. CONGO: ZAIDI YA WAFUNGWA 900 WATOROKA GEREZANI

> Wafungwa 900 wametoroka Gereza la Beni baada ya Wapiganaji kuvamia na kushambulia wakiwemo wa Kikundi cha Waasi cha ADF

> Kwa takwimu za UN, ADF imeua zaidi ya watu 1,000 tangu 2019

Soma https://jamii.app/Wafungwa900DRC
#JFLeo
TANZIA: MKURUGENZI MWENDESHAJI WA SHIRIKA LA TAIFA LA MAENDELEO AFARIKI DUNIA

> Prof. Damian Gabagambi afariki dunia Oktoba 20 ktk Hospitali ya Taifa ya Muhimbili

> Aliteuliwa na Rais kuwa Mkurugenzi Mwendeshaji wa NDC Machi 23, 2018

Soma https://jamii.app/ProfGabagambi
TANZANIA YAKOPA ZAIDI YA BILIONI 115 KUPAMBANA NA ATHARI ZA #COVID19

> AfDB imepitisha mkopo wa Dola Milioni 50.7 kwa #Tanzania

> Kwa mujibu wa AfDB, fedha hizo zitasaidia mpango wa Serikali wa takriban Bilioni 252 kupambana na #CoronaVirus

Soma https://jamii.app/MkopoCoronaTZ
#JFLeo
IGP SIRRO: POLISI IPO KUSIMAMIA HAKI, HAIPENDELEI

> Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Simon Sirro amesema Wanasiasa wasihofu, Polisi watampigia saluti yeyote atakayechaguliwa

> Pia, amewataka Wanasiasa watimize wajibu ili wasiingize Taifa ktk uhalifu

Soma https://jamii.app/IGPSirroHaki
#TZ2020
MAPISHI: JIFUNZE JINSI YA KUPIKA VITUMBUA

> Mahitaji ni mchele, tui zito la nazi, ute wa yai, unga wa sembe na wa ngano, hamira, hiliki na sukari

> Saga mchele na tui mpaka uwe laini. Tia yai, hamira na hiliki huku ukiendelea kusaga kisha weka sukari. Weka unga wa ngano na wa sembe na saga tena kidogo

> Weka kwenye chuma cha vitumbua na uanze kuchoma mpaka uone vimebadilika rangi

Soma https://jamii.app/MapishiVitumbua
RIPOTI: 85% YA WAFANYAKAZI WA NDANI WANADHALILISHWA NCHINI #QATAR

> Shirika la Amnesty International limearifu 85% ya Wanawake huporwa hati za kusafiri wanapowasili nchini humo

> Hunyimwa mishahara, chakula, hutemewa mate, hupigwa na kunyanyaswa kingono

Soma https://jamii.app/QataraWafanyakazi
NEC: HATUTARAJII KUONA MTU ANATANGAZA MATOKEO NJE YA UTARATIBU

> Tume ya Uchaguzi imesema Mamlaka ya kutangaza matokeo ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani yametolewa kwa Tume, Wasimamizi pamoja na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi

Soma https://jamii.app/MamlakaUchaguziNEC
#TZ2020