JamiiForums
βœ”
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MAALIM SEIF: TUTATOA KIPAUMBELE KWA WANAWAKE WASIBAKI KUWA WASINDIKIZAJI

> Amesema, ACT-Wazalendo itahakikisha nafasi nyingi za Uongozi zinashikiliwa na Wanawake

> Amesema, Wanawake ni jeshi kubwa linalotegemewa kuleta ushindi ktk Uchaguzi

Soma - https://jamii.app/ACTWanawakeUongozi
#TZ2020
DKT. SHEIN: KIWANGO CHA ELIMU ZANZIBAR HAKIJASHUKA

> Amepinga hoja zinazotolewa na baadhi ya watu kuwa, kiwango cha elimu kimeshuka

> Amesema kuna idadi kubwa ya Wanafunzi wanafaulu vizuri na kuzungumza Lugha za kigeni ikiwemo Kiingereza

Soma - https://jamii.app/SheinElimuZnz
#JFLeo
USHAURI WA MAMBO YA KUFANYA ILI KUKUSAIDIA UJIFUNGUE KWA NJIA YA KAWAIDA

> Jitahidi kufanya mazoezi kila siku kipindi chote wa ujauzito ili uwe tayari kuhimili changamoto zote za kujifungua. Kataa kuishi maisha ya 'stress' kila wakati

> Jitahidi kuutunza uzito wako. Zuia kuongezeka uzito uliopitiliza (Obesity). Anza kujifunza na kufuatilia taarifa zinazohusu namna gani ya kukabiliana na uchungu

Zaidi, soma - https://jamii.app/KujifunguaKawaida
LISSU (BAHI): CHADEMA ITARUDISHA UHURU WA KUONGEA ITAKAPOCHUKUA NCHI

> Itafanya hivyo kwasababu uhuru wa kuongea, kuhoji masuala ya maendeleo unakosekana

> Amewataka wananchi kupiga kura kukataa kodi na wizi wa Vitambulisho vya Ujasiriamali

Soma https://jamii.app/KampeniLissu
#TZ2020
MDAU: MTOTO WA MASIKINI AMBAYE SILAHA YAKE PEKEE NI ELIMU ATAJIAJIRI VIPI?

> Mdau wa JamiiForums.com anasema, japokuwa Tanzania kuna fursa mbalimbali, bado kumekuwa na wimbi kubwa la watu ambao hawana ajira

> Anasema wengi wanaowaambia vijana wajiajiri ni Wanasiasa na watu waliofanikiwa ambao wanapigana vikumbo kuwatafutia watoto wao ajira kwenye mashirika yanayolipa vizuri

Zaidi, soma - https://jamii.app/VijanaMafanikio
SIFA BAINIFU ZA WATOTO WALIOZALIWA KABLA YA KUHITIMU MUHULA (NJITI)

> Baadhi ya sehemu za mfumo wao wa neva hazijakua vyema

> Watoto hawa wana kiwango kidogo cha mafuta ya ngozi, hasa mafuta ya rangi ya kahawia

Soma > https://jamii.app/UzaziMtotoNjiti
WEMA SEPETU KUWANIA TUZO ZA HAPAWARDS 2020

> Msanii huyo wa Filamu anawania Tuzo za Hollywood And African Prestigious Awards za nchini Marekani katika kipengele cha Muigizaji Bora wa Kike wa Tamthilia za Kiafrika kupitia Tamthilia ya Karma

Soma - https://jamii.app/SepetuHAPAwards
MGOMBEA ADC: KAZI YA SERIKALI NI KUPANGA NJIA BORA ZA MATUMIZI YA RASILIMALI

> Mgombea Urais kupitia ADC, Queen Sendiga akiwa Mtwara ameahidi kurejesha ujenzi wa Kiwanda cha Gesi kama CCM ilivyoahidi awali na baadaye ikafanya tofauti

Soma - https://jamii.app/ADCRasilimali
#Uchaguzi2020
SABAYA: POLISI NAO NI BINADAMU, HUWA WANACHUKIA

> Mkuu wa Wilaya ya Hai amesema "Jeshi la Polisi ni Chombo cha Dola na wanaolitumikia ni binadamu, nao wanafika mahali wanakasirika"

> Amesema, Mbowe alitaka kufanya Kampeni eneo lisilotakiwa

Soma - https://jamii.app/HasiraPolisi
DKT. SHEIN: KAMPENI ZA DKT. MWINYI ZINAFIKIA JAMII, WAPO WALIOJARIBU WAKAISHIA NJIANI

> Amesema, mtindo wa Kampeni unaofanywa na Mgombea Urais wa #Zanzibar kupitia CCM, unalenga kuleta mabadiliko baada ya kufahamu changamoto za wananchi

Soma - https://jamii.app/SheinMwinyiZnz
#TZ2020
MADARAKA NA WAJIBU WA MBUNGE KWA MUJIBU WA KATIBA

> Kumuuliza Waziri swali kuhusu mambo ya umma ya Jamhuri ya Muungano ambayo yako ktk wajibu wake.

> Kujadili utekelezaji wa kila Wizara wakati wa Bunge wa kila mwaka wa Bajeti

Soma > https://jamii.app/WajibuMbunge

#Uchaguzi2020
OKTOBA 11: SIKU YA KIMATAIFA YA MTOTO WA KIKE

> Ni Siku inayolenga kutambua changamoto za Mtoto wa Kike, kuthamini na kuwezesha utekelezaji wa Haki zake

> Kaulimbiu ya Kitaifa inasema "Tumuwezeshe Mtoto wa Kike, Kujenga Taifa lenye usawa"

Soma https://jamii.app/GirlChildDay
#IDG2020
NDUGAI: HII NI AWAMU YANGU YA MWISHO, SITARAJII KUGOMBEA UBUNGE TENA

> Job Ndugai ambaye amekuwa Mbunge wa Kongwa tangu mwaka 2000 ametoa kauli hiyo leo akiwa Kanisani

> Amewataka wenye nia njema ya kuongoza Jimbo hilo kujiandaa na kujipanga

Soma https://jamii.app/NdugaiUbunge
JE, UNAFAHAMU RUSHWA YA NGONO NI NINI?

> Rushwa ya ngono ni pale ambapo Mtu aliye katika mamlaka na katika kutekeleza mamlaka yake akitaka au akiweka upendeleo wa ngono kama kigezo cha kutoa ajira, cheo, haki, au huduma ya upendeleo

Soma > https://jamii.app/NgonoRushwa

#KemeaRushwa
JE, UNAIFAHAMU ADHABU YA KUOMBA/KUTOA RUSHWA YA NGONO?

> Mtu atakayethibitika kuomba au kutoa rushwa ya ngono atakuwa amefanya kosa, ataadhibiwa kwa faini isiyozidi Tsh. Mil 5 au kifungo cha miaka isiyozidi 3 au vyote kwa pamoja.

Soma > https://jamii.app/NgonoRushwa

#KemeaRushwa
MOTO WAUNGUZA SEHEMU YA MLIMA KILIMAJARO

- Inaelezwa kuwa moto huo unaoteketeza sehemu ya Mlima huo umezuka leo mchana

- Mamlaka zimesema zinaendelea na juhudi za kuzima moto huo na taarifa zaidi zitatolewa

Soma > https://jamii.app/MotoKilimanjaro

#JFLeo #MotoKilimanjaro
HALIMA MDEE AFUNGIWA KUFANYA KAMPENI KWA SIKU 7

> Mgombea Ubunge katika Jimbo la Kawe kupitia CHADEMA, Halima Mdee amefungiwa kufanya Kampeni kwa siku saba kuanzia leo, Oktoba 12 mpaka 18 akidaiwa kukiuka maadili ya Uchaguzi

Soma - https://jamii.app/KampeniBanMdee
#Uchaguzi2020
UNYANYASAJI WA KIJINSIA BADO NI CHANGAMOTO ZANZIBAR

> Ndani ya miaka 3, watoto 88 wamepewa ujauzito na 50 kati yao wameozeshwa

> Kuanzia Januari 2019 - Agosti 2020 kuna kesi 761 za watoto kunyanyaswa huku 147 wakiingiliwa kinyume na maumbile

Soma https://jamii.app/UkatiliWatotoZbar