JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
TUNDU LISSU: NITABADILI MFUMO WA UTAWALA KUPITIA MABADILIKO YA KATIBA

> Amesema "Uchaguzi huu tunahitaji kufanya Mabadiliko na moja ni manyanyaso ya wananchi kuuziwa Vitambulisho vya wajasiriamali. Kwanini muuziwe vitambulisho?"

Soma - https://jamii.app/LissuNyakanazi
#Uchaguzi2020
CHAMA CHA ADC KINAENDELEA NA KAMPENI MKOANI TANGA

> Mgombea Urais wa Chama hicho, Queen Cuthbert Sendiga leo anaendelea na kampeni zake Wilayani Kilindi ktk Kata za Songe, Madoti, Kwamwambe, Mafisa, Kisangasa na Kwadiboma

Soma - https://jamii.app/ADCTanga

#Uchaguzi2020 #TZ2020
KENYA: WALIMU WATAKIWA KUFIKA SHULENI SEPTEMBA 28

> Tume ya Elimu kutoka Taasisi ya Maendeleo ya Mitaala (KICD) imependekeza Shule kufunguliwa Oktoba

> Waziri wa Elimu amesema tarehe rasmi itatangazwa baada ya Kamati kufanya mazungumzo

Soma - https://jamii.app/WalimuShuleKE
INDIA: WATU 10 WAFARIKI BAADA YA JENGO KUPOROMOKA

> Jengo hilo liliwekwa katika orodha ya majengo hatari na taarifa ya wakazi kuondolewa ilitolewa

> Watu 20 hadi 25 wanahofiwa kukwama chini na jitihada za uokoaji zinaendelea

Soma - https://jamii.app/BuildingCollapseIndia
FAHAMU ILANI YA CHADEMA INASEMA NINI KUHUSU UHURU WA KUJIELEZA

> Itahakikisha Sheria zote zinazokandamiza uhuru wa habari zitafutwa na kila mwananchi atakuwa huru

> Itachunguza matukio ya vifo na utekaji wa waandishi wa habari

Zaidi, soma https://jamii.app/IlaniCDM
#Uchaguzi2020
ILANI YA ACT-WAZALENDO INASEMAJE KUHUSU UHURU WA KUJIELEZA?

> Ndani ya siku 100 za kwanza itafuta Sheria zote zinazobana, kuminya na kufifisha haki/uhuru wa kujieleza

> Itatengeneza majukwaa na mifumo itakayowawezesha Watu kutoa maoni

Soma - https://jamii.app/IlaniACT
#Uchaguzi2020
RUVUMA: WATU 71 WANYWA TOGWA INAYODHANIWA KUWA NA SUMU, WANUSURIKA KIFO

> Ni ktk sherehe ya kidini ijulikanayo kama Sadaka. Baadhi wamesema walianza kuharisha na kutapika baada ya kuinywa

> Mkuu wa Wilaya amepiga marufuku togwa kwenye sherehe

Soma https://jamii.app/TogwaSumuRVM
SHERIA YA GHARAMA ZA UCHAGUZI

Kwa mujibu wa kifungu cha 23 kifungu kidogo cha 7; ni jukumu la Serikali kuhakikisha kuwa njia za usafirishaji zinakuwepo kwa wapiga kura wote ambao wanahitaji kufika kwenye vituo vyao vya kupigia kura

Soma => https://jamii.app/GharamaUchaguzi

#KemeaRushwa
ACT-WAZALENDO YAMUUNGA MKONO MGOMBEA URAIS WA CHADEMA

- Akifanya Kampeni Jimbo la Donge leo, Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo Taifa, Maalim Seif Sharif Hamad amemuidhinisha Tundu Lissu kuwa Mgombea wao wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Soma - https://jamii.app/MaalimLissuUrais
#Uchaguzi2020
MEMBE: MIMI NDIYE MGOMBEA URAIS KUPITIA ACT-WAZALENDO

> Bernard Membe amekanusha taarifa za kuwa wamejiunga na CHADEMA katika ngazi ya Urais

> Amesema yeye ndiye aliyekabidhiwa Ilani ya Chama ili kuinadi kote nchini kwenye Uchaguzi

Soma https://jamii.app/MembeACT-CDM

#Uchaguzi2020
MAREKANI YAITAKA KENYA KUIUNGA MKONO ISRAEL HADHARANI

> Nchi hiyo imesema hakutakuwa na Makubaliano ya Biashara Huria (FTA) Kenya isipofanya hivyo

> Vilevile, imeitaka Kenya kukemea vitendo vinavyoathiri biashara kati ya Marekani na Israel

Soma https://jamii.app/USKenyaFTA
ILANI YA CHAUMMA INASEMAJE KUHUSU KATIBA MPYA?

> Itahakikisha Rasimu ya #Katiba inarejeshwa kama ilivyopendekezwa na wananchi

> Itaweka misingi ya Mgawanyo wa Mamlaka ktk Mihimili ya Dola itakayoondoa utaratibu wa Mihimili kuingiliana

Soma - https://jamii.app/IlaniCHAUMMA
#TZ2020
MGAYWA (SAU): KILA MTANZANIA ATAPEWA KIPANDE CHA ARDHI NA KIWANJA

> Mgombea huyo amesema, kodi ya kiwanja haitakuwepo kuanzia tarehe 28 atakapokuwa Rais

> Ameongeza, ardhi ni mali ya Wananchi isipokuwa iko chini ya udhamini wa Rais

Soma - https://jamii.app/SAUViwanjaBure

#Uchaguzi2020
SHINYANGA: BINTI WA DARASA LA 5 AOZESHWA KWA NG'OMBE 8 NA TSH. LAKI 6

> Watu 4 wanashikiliwa na Polisi kwa tuhuma ya kumuozesha Mwanafunzi kwa tamaa ya mali

> Mwanafunzi huyo amekabidhiwa ktk kituo cha kulelea watoto ili aendelee na masomo

Soma https://jamii.app/NdoaMwnf5
ILANI YA NCCR-MAGEUZI INASEMAJE KUHUSU KATIBA MPYA?

> Itakamilisha mchakato wa kupata #KatibaMpya kupitia Bunge la Katiba kwa kujumuisha makundi yote

> Ukiukaji wa #Katiba utakuwa kosa la jinai na Rais atapunguziwa madaraka yake

Soma - https://jamii.app/IlaniNCCR
#Uchaguzi2020
DKT. MAGUFULI AAGIZA ELIMU YA VITAMBULISHO VYA WAJASIRIAMALI ITOLEWE

> Amesema Vitambulisho havilazimishwi kwa wafanyabiashara na vinatolewa ili wenye biashara ndogondogo waweze kufanya biashara mahali popote nchini bila kusumbuliwa

Angalia https://youtu.be/IQ1YPihUZc0
#Uchaguzi2020
KUKWAMA KWA SHERIA YA JINSIA: RAIS WA KENYA ASHAURIWA KUVUNJA BUNGE

> #Katiba ya #Kenya inataka Sheria hiyo kuwepo ili kudhibiti jinsia kutotawala ktk nyadhifa za uteuzi na kwa miaka 10 sasa Wabunge ambao wengi ni wanaume, wameshindwa kuipitisha

Soma - https://jamii.app/JinsiaBungeniKE
FAHAMU BAADHI YA MAKOSA YA UCHAGUZI

> Kifungu cha 92 cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi Sura ya 343: Ni kosa kutoa ushahidi/maelezo ya uongo

> Kifungu cha 93: Ni kosa kutoa siri inayohusu Mgombea/mchakato unaoendelea ktk Kituo cha Kupigia Kura

Soma https://jamii.app/MakosaUchaguzi
MALI: WAZIRI WA ZAMANI ATEULIWA KUWA RAIS WA MPITO

> Bah Ndaw atangazwa kama Rais wa Mpito, naye Kanali Goita aliyeongoza mapinduzi ya kijeshi atakuwa Makamu wa Rais

> ECOWAS imekuwa ikiwashinikiza Wanajeshi kurudisha madaraka kwa raia

Soma - https://jamii.app/NdawRaisMali
FACEBOOK YATUHUMIWA KUINGILIA FARAGHA ZA WATUMIAJI WA INSTAGRAM KUPITIA KAMERA ZA SIMU

> Mlalamikaji Brittany Conditi amesema Facebook inatumia kamera za iPhone ili kukusanya taarifa za watumiaji ambazo hawawezi kuzikusanya kwa njia nyingine

Soma - https://jamii.app/FBSpyIstagram