JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
JE, ILANI YA CHAUMMA INASEMA NINI KUHUSU ELIMU NA MALEZI YA TAIFA?

- Itabadili mitaala kuanzia Elimu ya Msingi hadi Vyuo Vikuu ili kuipa ubora wa hali ya juu

- Itahakikisha mitaala yote nchini ni ile tu yenye manufaa na maana

Soma > https://jamii.app/IlaniCHAUMMA

#Uchaguzi2020 #Siasa
DKT. MAGUFULI: MAENDELEO HAYANA CHAMA LAKINI UNACHAGUA CHAMA NA KIONGOZI KWA MAENDELEO

> Ameyasema hayo alipokuwa Kasulu na ameahidi kujenga lami ili Kigoma iwe kama Ulaya

> Ameongeza kuwa, ametenga Tsh. bilioni 402 za kuiendeleza Kigoma

Soma https://jamii.app/MaendeleoChama
#JFSiasa
JE, ILANI YA CUF INASEMA NINI KUHUSU ELIMU?

- CUF itatumia si chini ya asilimia 25 ya bajeti yake kila mwaka kuboresha Sekta ya Elimu kwa ujumla

- Lishe kwa wanafunzi: Utafiti unaonyesha kuwa watoto wenye njaa hawafundishiki

Soma > https://jamii.app/IlaniCUF
#Uchaguzi2020 #TZ2020
NJOMBE: TAKUKURU YAMSHTAKI RAIA ALIYETOA USHAHIDI WA UONGO

> Inadaiwa, awali Eliezer Lutumo aliieleza TAKUKURU kuwa alitoa Tsh. 10,000 na kumpa Bryson Lupenza

> Alipoitwa Mahakamani mbele ya Hakimu Mkazi, Lutumo alikana maelezo hayo

Soma https://jamii.app/KizimbaniUshahidi
#JFLeo
KILIMANJARO: TAKUKURU YAREJESHA TSH. MILIONI 2.6 ZA SHULE

> Aliyekuwa Mkuu wa Shule na Mhasibu walizitumia kwa matumizi yao

> Fedha hizo zilitolewa na wafadhili kwa ajili ya chakula cha mchana kwa watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu

Soma https://jamii.app/PCCBtsh2b
#JFLeo
NI KOSA KUBANDIKA PICHA YA MGOMBEA JUU YA PICHA YA MGOMBEA MWINGINE

> Hayo yameainishwa kwenye Maadili ya Uchaguzi ya mwaka 2020

> Pia, kuzidisha muda, kukiuka ratiba ya kampeni na kutoa Lugha ya matusi na kashfa vimezuiwa

Soma https://jamii.app/MaadiliUchaguzi

#TZ2020
DAR: 5 WAHUKUMIWA KUNYONGWA KWA MAUAJI YA DKT. SENGONDO MVUNGI, 1 AACHIWA HURU

> Dkt. Mvungi alivamiwa nyumbani kwake Novemba 3, 2013

> Aliwahi kugombea Urais wa JMT 2005 kupitia NCCR-Mageuzi na alikuwa Mjumbe wa Tume ya Katiba ya Jaji Warioba

Soma https://jamii.app/HukumuWauajiDrMvungi
SINGIDA: MIAKA 30 JELA KWA KUMBAKA MTOTO WAKE

> Hamisi Mtanda (37) amekutwa na hatia ya kumbaka mwanaye wa kike wa kumzaa wa miaka 11

> Katika kujitetea, mshtakiwa alisema mtoto huyo alifanya ngono na mwalimu bila kutaja ni mwalimu yupi

Soma https://jamii.app/BabaAmbakaMwanaye
#JFLeo
DIAMOND PLATNUMZ ASHIRIKISHWA KWENYE ALBUM YA ALICIA KEYS

> Alicia Keys ametoa Album mpya inayoitwa 'Alicia' ambapo Msanii kutoka Tanzania, Naseeb Abdul amepata nafasi ya kushirikishwa kwenye wimbo wenye jina Wasted Energy

Soma https://jamii.app/DiamondAliciaKeys
#JFBurudani #Entertainment
1
DKT. MAGUFULI ATOA WITO KWA WASIOAMINI MUNGU WAJE KUJIONEA TANZANIA

> Dkt. John Magufuli ametoa wito kwa wasioamini Mungu waje wajionee Mungu alivyoifukuza #CoronaVirus Tanzania

> Pia amesema, hata wale waliobeza awali na kusema watu milioni 4 wangekufa kwa #COVID19, hawana la kusema sasa

Soma https://jamii.app/WitoKuaminiMungu
#TZ2020
IGP SIRRO AONGEZEWA MWAKA 1 ZAIDI KUIONGOZA EAPCCO

> Shirikisho la Wakuu wa Polisi Mashariki mwa Afrika wamemtaka IGP Simon Sirro kuendelea kuwa Mwenyekiti wao

> IGP Sirro amesema watahakikisha wanabadilishana uzoefu na kufanya mafunzo ya pamoja

Soma https://jamii.app/IGPSirroEAPCCO
#JFLeo
JE, ILANI YA NCCR-MAGEUZI IMEZUNGUMZA NINI KUHUSU AFYA NA USTAWI WA JAMII?

> Itaimarisha afya ya Mama na Mtoto kwa kusogeza Huduma za Afya karibu na makazi ya watu

- Itaongeza mishahara na marupurupu kwa watumishi wa Sekta ya Afya

Soma https://jamii.app/IlaniNCCR
#Uchaguzi2020
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DKT. MAGUFULI ATAJA MPANGO WA KUPANUA UWANJA WA NDEGE WA KIGOMA

> Mgombea Urais (CCM) amesema wanataka Airbus ziwe zinatua ktk Uwanja wa Ndege wa Kigoma ili kukuza utalii

> Asema, Sekta ya Utalii imeajiri watu milioni 4 kwa miaka 5 iliyopita

Soma https://jamii.app/WitoKuaminiMungu
#TZ2020
KAGERA: SERIKALI YATOA 250,000 KWA FAMILIA ZILIZOFIWA KATIKA AJALI YA MOTO

> Ni rambirambi kwa kila familia iliyofiwa na mtoto ktk ajali ya moto, Shule ya Msingi Islamic Byamungu

> Pia, Serikali inawagharamia wanafunzi 6 wanaopatiwa matibabu

Soma https://jamii.app/AjaliKageraSerikali
#JFLeo
JE, WAJUA UMUHIMU WA JESHI LA POLISI TANZANIA?

> Jeshi la Polisi lipo kuhakikisha usalama wa raia na mali zao

> Pia, kubaini na kupambana na uhalifu na kuhakikisha kila mtu anafuata Sheria

Soma https://jamii.app/UmuhimuWaPolisi
#JFMaarifa
MPANDA: JELA MIAKA 60 KWA KUMTOROSHA NA KUMBAKA MWANAFUNZI

> Said Selemani(20), amekutwa na hatia ya kumbaka Mwanafunzi wa Kidato cha Pili

> Katika utetezi mshtakiwa alidai alikuwa naye ili amsaidie kumrejesha kwao kwani alikuwa amefukuzwa

Soma https://jamii.app/Jela60Kubaka
#JFLeo
ZANZIBAR: TAMWA YALAANI WATOTO KUCHOMWA SINDANO BILA SABABU

> Septemba 15, 2020 iliripotiwa tukio la watoto 3 kuchomwa sindano na mtu asiyejulikana

> Tukio kama hilo si la kwanza, TAMWA wanaona huo ni udhalilishaji unaopaswa kukemewa

Soma https://jamii.app/WatotoZnz
#JFLeo
YAJUE MAMLAKA YA POLISI

> Polisi ana mamlaka kukamata, kufanya upekuzi, kushikilia, kumpeleleza mtuhumiwa, kumhoji shahidi na kufanya mahojiano na mtuhumiwa

> Kutawanya waandamanaji wenye nia ovu na kuhakikisha usalama katika jamii

Soma https://jamii.app/UmuhimuWaPolisi
#JFMaarifa
ILANI YA UCHAGUZI YA CHADEMA INAAHIDI NINI KUHUSU SEKTA YA AFYA?

> CHADEMA itatoa motisha kwa watendaji wa Sekta ya Afya kulingana na nafasi zao

> Itaboresha mifumo ya huduma za dharura ktk maeneo yote ya utoaji huduma za afya

Soma https://jamii.app/IlaniCDM

#Uchaguzi2020
DAR: AFISA MAUDHUI WA CHADEMA KIZIMBANI

> Dominic Mgaya amepandishwa kizimbani kwa kosa la kuchapisha maudhui bila kuwa na leseni ya TCRA

> Alifanya hivyo kupitia channel ya CHADEMA MEDIA TV kati ya Oktoba 14, 2017 na Septemba 1, 2020

Soma https://jamii.app/MakosaYaMtandaoCHADEMA
#JFLeo