JamiiForums
52.9K subscribers
34.3K photos
2.42K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
UGANDA: MLINZI AMPIGA RISASI MWANAFUNZI WA CHUO CHA KAMPALA

> Polisi nchini Uganda wanachunguza tukio la Mlinzi wa Usalama kumpiga Risasi Isaac Katagwa (mwaka 3) kutoka Chuo Kikuu cha Kampala, Tawi la Jinja

> Isaac alipigwa risasi mgongoni na kupoteza maisha papo hapo usiku wa Jumatano

Soma - https://jamii.app/MlinziAuaRisasiMwnfz
MVUA, MAFURIKO NA MAPOROMOKO ZAATHIRI WATU MILIONI 3 AFRIKA MASHARIKI

> Watu milioni 3 Afrika Mashariki wameathiriwa na mvua, mafuriko na maporomoko ya matope huku zaidi ya 200 wakifariki tangu kuanza kwa msimu wa mvua hizo

> Mvua hizo zinasababishwa na viwango vya juu vya joto katika Bahari ya Hindi na kupanda kwa digrii 2 Celsius

Soma - https://jamii.app/FloodsDisasterEAC
HUKUMU YA JAMAL MALINZI KUTOLEWA LEO

> Mahakama ya Kisutu inatarajia kutoa Hukumu ktk kesi inayomkabili aliyekuwa Rais wa TFF, Jamal Malinzi na wenzake 4

> Wanakabiliwa na mashtaka ya kula njama, kughushi, kujipatia fedha kidanganyifu na utakatishaji fedha

Soma - https://jamii.app/HukumuMalinziKisutuDec5
NAFASI ZA KUJIUNGA KIDATO CHA 1 ZATOKA, MIKOA 13 YAFAULISHA WANAFUNZI WOTE

> Wanafunzi 701,038 (92.27%) waliofaulu Mtihani wa Darasa la Saba mwaka 2019 wamechaguliwa kuendelea na Kidato cha 1

> Wanafunzi 58,699 wamekosa nafasi kutokana na uhaba wa madarasa

Soma - https://jamii.app/MajinaUfauluKidato1
USHAURI: MISAFARA YA VIONGOZI INACHOSHA, INATESA. IGP PELEKA WATU SWEDEN WAKAJIFUNZE

- Mdau wa JamiiForums anasema akiwa njia ya Bagamoyo eneo la Mbezi Tangi Bovu, walisimamishwa karibu dakika 30 kupisha msafara wa Kiongozi fulani

Zaidi, soma > https://jamii.app/MisafaraViongozi
USHAURI WA KANUNI BORA ZA KILIMO CHA MIGOMBA

> Kiasi cha chini cha mvua kifaacho ni 100mm kwa mwezi au 1200mm kwa mwaka. Mwinuko ni kutoka usawa wa bahari hadi mita 1800 juu ya usawa wa bahari. Kiasi cha joto ni nyuzi joto za 25'C hadi 30'C

> Machipukizi mazuri yanayofaa kwa mbegu ni yale yenye majani membamba, Mgomba (shina) wenye afya nzuri na Mgomba wenye sifa ya kuzaa mikungu mikubwa
-
Wakati unaofaa kupanda machipukizi ni mwanzoni mwa msimu wa mvua

Fahamu zaidi - https://jamii.app/KilimoMigombaNdizi
#JFKilimo
MABORESHO YA BIMA YA AFYA KUJUMUISHA MAGONJWA YENYE GHARAMA KUBWA

> Wizara ya Afya kwa kushirikiana na NHIF inaendelea kuboresha vifurushi vya bima kwa kuweka magonjwa yenye gharama kubwa kama Moyo, Figo, Saratani, Kisukari na mengineyo

> Aidha, huduma ya uzazi itaendelea kuboreshwa kwa kupunguzwa muda wa kusubiri matumizi

Soma - https://jamii.app/MaboreshoMagonjwaBima
UPDATE: HUKUMU YA KESI DHIDI YA JAMAL MALINZI NA WENZAKE WA 4 YAAHIRISHWA HADI DESEMBA 11, 2019

> Kesi hiyo inayosimamiwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Janeth Mtega imeahirishwa baada ya Hakimu kuomba muda wa kupitia jalada la hukumu

Zaidi soma > https://jamii.app/HukumuMalinziKisutuDec5
DOVUTWA APINGA KUVULIWA UENYEKITI UPDP, AWATAKA WANACHAMA KUJIANDAA NA UCHAGUZI

> Fahmi Dovutwa amepinga kuvuliwa Uenyekiti kwa madai ya kutangaza kuwa UPDP haitashiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika Novemba 24

> Asema, wanaotangaza hivyo wana hofu ya uchaguzi wa Chama hicho utakaofanyika mwishoni mwa Desemba, 2019

Soma - https://jamii.app/DovutwaApingaKuvuliwaMKiti
FAHAMU NGUVU YA UTULIVU NA KUWEZA KUKAA PEKE YAKO ILI KUFIKIRI

> Jijengee tabia ya kuwa na muda wa utulivu kila siku, muda ambao unakaa wewe peke yako na mawazo yako, na hakuna usumbufu wowote unaokuwa karibu na wewe katika wakati huu

> Utaanza kuona jinsi ambavyo maisha yako yatabadilika, Msongo utapungua, wasiwasi na mashaka ya kupoteza vitu yataondoka kabisa na utajiona unayaendesha maisha badala ya maisha kukuendesha wewe

Tembelea - https://jamii.app/NguvuUtulivuKufikiri
#JFMaisha
TANZIA: KIUNGO MAHIRI WA ZAMANI WA KLABU ZA YANGA NA SIMBA, ALLY YUSUF MAARUFU TIGANA AFARIKI DUNIA

- Amefariki dunia leo katika hospitali ya Amana, Jijini Dar baada ya kuugua ghafla na kukimbizwa hospitali hapo

> Alianza kuhara na kutapika ghafla

Soma > https://jamii.app/RIPTigana
#JFLeo
KENYA: CHUO CHA EGERTON CHAFUNGWA KUTOKANA NA MGOMO WA WANAFUNZI

> Chuo Kikuu cha Egerton kimefungwa kwa muda usiojulikana kutokana na wanafunzi kufanya mgomo wakishinikiza kuruhusiwa kufanya mitihani ya muhula pasipo kukamilisha ada

> Aidha, Chuo kimetishia kuwasimamisha masomo wanafunzi kwa mwaka 1 ikiwa hawatokamilisha ada

Soma - https://jamii.app/EgertonUnvClosedFees
HUKUMU YA KESI ILIYOFUNGULIWA NA JAMHURI DHIDI YA JAMIIFORUMS KUTOLEWA KESHO

- Shauri hilo ni moja kati ya kesi zilizofunguliwa na Jamhuri dhidi ya Mkurugenzi wa Jamii Media Co. Ltd na mmoja wa wanahisa wake

- Hukumu hiyo ni ya shauri namba 456

Soma > https://jamii.app/JamhuriVsJamiiForums

#JFLeo
IJUE SHERIA INAYOPIGA MARUFUKU KUPIGA KELELE MAENEO YA MAKAZI

> Marufuku hii ni kwa mujibu wa Kanuni zilizozinduliwa mwaka 2015 kulingana na Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya mwaka 2014.

> Kelele za Baa, muziki, matangazo na shughuli nyingine za kijamii zinatozwa faini ya milioni 50

Zaidi, soma > https://jamii.app/UchafuziMazingiraKelele
WHO: VISA VYA UGONJWA WA SURUA DUNIANI VYAONGEZEKA

> Takriban watu 140,000 hufariki duniani kutokana na ugonjwa wa Surua na Bara la Afrika linasadikiwa kuwa na idadi kubwa zaidi ya vifo vinavyotokana na ugonjwa huo kwa takriban vifo 52,600

> Barani Afrika, nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Liberia, Madagascar na Somalia zimeathirika zaidi huku DRC ikiripoti visa 250,000 vya ugonjwa huo kufikia Novemba mwaka huu

Soma - https://jamii.app/OngezekoMaambukiziSurua
UTAFITI: KUKU WA KIENYEJI WANAOUZWA MITAANI WABAINIKA SIO WA KIENYEJI

> Utafiti uliyofanywa na Shirika la World Animal Protection umebaini kuku hao ni wa kisasa (kizungu) wanaofugwa majumbani kwa kupewa majani pamoja na dawa mbalimbali za kuwakuza na kuwafanya kuwa wagumu

Soma - https://jamii.app/KukuKienyejiFeki
KENYA: JENGO LA GHOROFA 6 LAANGUKA, WATU WAHOFIWA KUNASA KWENYE KIFUSI

- Jengo hilo la ghorofa sita limeanguka asubuhi ya leo katika eneo la Embakasi Jijini Nairobi

- Hadi sasa juhudi za uokoaji zinaendelea kufanyika

Zaidi, sma => https://jamii.app/JengoLaporomokaKenya
MICHEZO: CHELSEA FC YAPUNGUZIWA ADHABU. SASA ITARUHUSIWA KUFANYA USAJILI DIRISHA LA JANUARI 2020

- Chelsea ilifungiwa kufanya usajili kwa madirisha 2 ya usajili baada ya kukutwa na hatia ya kuwasajili wachezaji vijana kinyume na utaratibu

Soma > https://jamii.app/ChelseaFcHuru

#JFSports
KENYA: GAVANA WA JIJI LA NAIROBI, MIKE SONKO AKAMATWA NA TAASISI YA KUPAMBANA NA RUSHWA

- Imeelezwa kuwa Sonko amekamatwa akituhumiwa kwa kujipatia kiasi cha zaidi ya Shilingi za Kitanzania bilioni 8 kinyume cha sheria ya manunuzi

Zaidi, soma > https://jamii.app/SonkoMbaroni
MANYARA: RC MNYETI AFUTA KIKUNDI CHA WATU WA KILIMANJARO

> Ni kikundi cha watu wa Kilimanjaro waishio Manyara

> Asema ataendelea kuvifuta vikundi vyote vya watu kutoka mikoa mingine waishio Manyara kwani havina faida mkoani humo na vinaendekeza ukabila

Soma http://jamii.app/RCMnyetiTena