JamiiForums
32.8K subscribers
37.6K photos
3.02K videos
33K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mbunge wa Tunduru Kaskazini na Katibu Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Ado Shaibu ameyasema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari, Aprili 30, 2026.

Soma zaidi https://jamii.app/AdoShaibuSiasaAfrika

#JamiiForums #Siasa #Demokrasia #Governance
3
DAR: Mdau wa JamiiForums.com anatoa wito kwa mamlaka husika kutatua kero ya takataka kutelekezwa kwa muda mrefu bila kuzolewa mitaa ya Bunju.

Zaidi https://jamii.app/TakaKurundikwa

#JamiiForums #Uwajibikaji #JFMdau2026 #PublicHealth #JFAfya
1
ENGLAND: Timu ya #ManchesterUnited imetandika #Liverpool magoli 3-2 katika mchezo wa Premier League, leo Mei 3, 2026 ushindi ambao unaifanya Uniyed kujihakikishia nafasi ya kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao wa 2026/27.

Man United imefikisha pointi 64 ikiendelea kubaki nafasi ya tatu, Liverpool imesalia nafasi ya nne ikiwa na alama 58,  huku kila upande ukiwa umesaliwa na michezo mitatu.

Zaidi https://jamii.app/ManUtdVsLiverpool

#JamiiForums #JFSports #JFEPL2026
1
DAR: Aprili 30, 2026 mwili huo ulionekana ukielea katika Mto Msimbazi eneo la Kipawa wilaya ya Ilala huku ukiwa hauna kichwa.

Zaidi soma https://jamii.app/PolisiKifoMsimbazi

#JamiiForums #Uwajibikaji #HumanRights
DAR: Baada ya tambo kwa siku kadhaa, hatimaye wababe wa mitaa ya Kariakoo, Simba na Yanga wamekipiga uwanjani na kutoshana nguvu ya magoli 2-2 katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, leo Mei 3, 2026.

Simba ilitangulia kufunga kupitia kwa Libasse Gueye na Clatous Chama, Yanga ikasawazisha kwa magoli ya Prince Dube na Bakari Mwamnyeyo.

Kutokana na matokeo hayo, Yanga imeendelea kuongoza msimamo wa Ligi ikiwa na alama 48, Simba ni ya pili ikiwa na pointi 43, timu zote zikiwa zimecheza michezo 20.

Zaidi https://jamii.app/SimbaYangaMei3

#JamiiForums #JFSports #JFLigiKuu2026
👍2
Mdau, ni kitu gani ulishawahi kukisikia na hukuamini, lakini baadaye ukagundua ni kweli?

Zaidi https://jamii.app/UkweliKuamini

#JamiiForums #JFMaisha
1
Mdau wa JamiiForums.com amehoji kuhusiana na ukimya wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (#LATRA) wa kutotoa tamko rasmi au ufafanuzi kuhusu suala la nauli kupanda tangu taarifa hizo zilipoanza kusambaa Mtandaoni na nauli kupanda rasmi kuanzia Mei Mosi, 2026.

Zaidi https://jamii.app/UkimyaLatraNauli

#JamiiForums #JFMdau2026 #JFHuduma #Uwajibikaji
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, leo Mei 4, 2026, amewasilisha hotuba ya Bajeti ya Wizara kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027, akiomba Bunge kuidhinisha Tsh. Bilioni 525.3.

Kati ya hizo, kiasi cha Tsh. Bilioni 39.07 kwa ajili ya mishahara, Tsh. Bilioni 28.06 ni matumizi mengineyo, huku Tsh. Bilioni 458.19 zikitengwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

Kwani nyie Wadau wa Michezo, Habari, Sanaa na Utamaduni mnasemaje?

Soma https://jamii.app/BajetiWizaraHabari

#JamiiForums #Utawala #Governance
1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Makamu Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo Bara, Isihaka Mchinjita amesema hayo Mei 4, 2026 wakati akizungumza na Waandishi wa Habari.

Fuatilia zaidi https://jamii.app/MchinjitaTumeRisasi

#JamiiForums #Uwajibikaji #HumanRights