JamiiForums
35K subscribers
37.2K photos
2.94K videos
32.8K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
DAR: Mdau wa JamiiForums.com anasema Barabara inayopita Kimara, Mavurunza, Bonyokwa mpaka Kinyerezi wakati wa awamu ya nne chini ya Rais Jakaya Kikwete liliwekwa jiwe la msingi na barabara hiyo kuitwa Kikwete Road, lakini hadi sasa ujenzi wake haujatekelezwa.

Mdau, barabara ya mtaani kwako inapitika vizuri kipindi hiki cha mvua?

Shiriki mjadala https://jamii.app/MkandarasiHayupoSite

#JamiiForums #JFMdau2026 #Uwajibikaji
DAR: Mdau wa JamiiForums.com aliyejitambulisha kuwa ni Mfanyakazi katika Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka ameomba Uongozi uboreshe maslahi yao katika mikataba na kuwalipa malipo ya muda wa ziada (overtime) waliyostahili kulipwa Mei hadi Oktoba 2025.

Jitihada za kutafuta Mamlaka inayosimamia mradi huo upande wa mabasi zinaendelea.

Fuatilia zaidi mjadala huu https://jamii.app/MwendikasiMaslahi

#JamiiForums #Uwajibikaji #JFMdau2026
MALAWI: Jeshi la Polisi limemkamata aliyekuwa Waziri wa Fedha, Simplex Chithyola kwa tuhuma za utakatishaji fedha na matumizi mabaya ya ofisi. Chithyola, ambaye kwa sasa ni Kiongozi wa Upinzani bungeni, alijikabidhi mwenyewe Polisi Aprili 12, 2026 baada ya kuwekwa kwenye orodha ya wanaosakwa na wachunguzi wa makosa ya jinai.

Fuatilia mjadala huu https://jamii.app/ChithyolaMalawi

#JamiiForums #Uwajibikaj #Accountability
DAR ES SALAAM: Mdau wa JamiiForums.com anatoa wito kwa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) kufanya matengenezo ya 'lifti' tatu zilizoharibika ambazo hazitumiki katika jengo la RITA Tower akidai imekuwa kero kwa Watu wengi na kwamba Mtu anaweza kusubiri kwa nusu saa au zaidi kusubiria zamu ya kupanda.

Nini maoni yako Mdau?

Shiriki kwenye mjadala https://jamii.app/RitaLift

#JamiiForums #JFMdau2026 #Uwajibikaji #JFHuduma
1
Je, unakubaliana na hoja kuwa wazazi wanapaswa kujipanga wenyewe kwa Maisha ya uzeeni badala ya kutegemea Watoto?

Toa maoni yako 👇 na washirikishe wazazi wako kupata mitazamo yao https://jamii.app/WatotoMsaadaWazazi

#JamiiForums #JFMaisha #JFUwajibikaji
Akizungumzia kuhusu mfumo huo, Mkurugenzi wa Muungano wa Kupambana na Rushwa Uganda (ACCU), Marlon Agaba amesema kuwa mkataba wa Mwaka 1 utamaliza "kubweteka" kwa Watumishi wanaojiona wana usalama wa ajira hata wasipofanya kazi na kuongeza kuwa mapendekezo hayo yanaakisi mapendekezo ya muda mrefu ya wanaharakati wa kupambana na Rushwa.

Mdau, unaonaje pendekezo hili likifanyika nchini?

Toa maoni yako kupitia https://jamii.app/UgandaWatumishi

#JamiiForums #Governance #Utawala #Accountability
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR ES SALAAM: Mdau wa JamiiForums.com anatoa wito kwa Mkandarasi anayejenga barabara ya Mwenge - Tegeta kumwaga maji kwani vumbi limekuwa kero kwa watumiaji wa barabara na wenye makazi maeneo ya jirani.

Fuatilia zaidi mjadala https://jamii.app/BarabaraMwengeTegeta

#JamiiForums #JFMdau2026 #Uwajibikaji