JamiiForums
35.2K subscribers
37.2K photos
2.94K videos
32.7K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
PWANI: Mdau wa JamiiForums.com ametoa wito kwa Jeshi la Polisi kuchukua hatua dhidi ya kundi la Vijana linalojihusisha na matukio ya uhalifu katika eneo la Misugusugu Wilaya ya Kibaha, akidai Wananchi wanateseka kwa kuporwa mali zao na kutishiwa maisha.

Fuatilia mjadala https://jamii.app/VibakaMisugusugu

#JamiiForums #JFMdau2026 #JFHuduma #CivilRights
Kauli ya Rais #DonaldTrump inakuja siku moja baada ya Papa Leo XIV wakati wa ibada Aprili 11, 2026 katika Kanisa la Mtakatifu Petro mjini Vatican, kukosoa vita inayoendelea kati ya Marekani, Israel na Iran, akisema Viongozi wanaolewa sifa za madaraka na nguvu za kijeshi ndiyo wanaochochea vita hiyo.

Shiriki mjadala https://jamii.app/TrumpPapaMarekani

#JamiiForums #JFDiplomacy #Governance
Mdau wa JamiiForums.com anashauri Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) ifanye maboresho kwenye Kitengo cha Huduma kwa Wateja, hasa eneo la mawasiliano ya njia ya simu.

Mdau, umewahi kukumbana na changamoto hii?

Shiriki mjadala https://jamii.app/TRAHuduma

#JamiiForums #JFMdau2026 #Uwajibikaji #JFHuduma
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR ES SALAAM: Mdau wa JamiiForums.com anatoa wito kwa Viongozi wanaohusika kukarabati barabara iliyopo Darajani Kimara Mwisho, ameonesha hali ilivyo, leo Aprili 13, 2026 ikiwa haipitiki kiurahisi na kuwa adha kwa Watumiaji.

Mdau, hali ya barabara eneo lako ikoje kipindi hiki cha mvua?

Shiriki kwenye mjadala https://jamii.app/KimaraBarabara

#JamiiForums #JFMdau2026 #Uwajibikaji
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Mbunge wa Jimbo la Bariadi, Masanja Kadogosa ameyasema hayo leo Aprili 13, 2026 alipokuwa akichangia hoja Bungeni.

Yapi maoni yako

Shiriki mjadala https://jamii.app/GesiMafuta

#JamiiForums #Governance
Ikumbukwe mapema Aprili 13, 2026, Rais Donald Trump kupitia ukurasa wake wa Truth Social, alimtaja Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Leo XIV kuwa ni Papa dhaifu katika kukemea masuala ya uhalifu na kudai kuwa alichaguliwa na Kanisa Katoliki kwa makusudi ili apambane na utawala wake.

Fuatilia mjadala https://jamii.app/PapaLeoTrump

#JamiiForums #Utawala #Governance #JFDiplomacy
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Bonnah Ladislaus Kamoli ameyasema hayo leo Aprili 13, 2026 wakati akichangia Hotuba ya Waziri Mkuu Bungeni ambapo amegusia hali ya miundombinu kuelekea michuano ya #AFCON2027 ambapo Tanzania itakuwa mwenyeji kwa kushirikia na Kenya na Uganda.

Nini maoni yako Mdau?

Fuatilia mjadala https://jamii.app/BarabaraDarAFCON

#JamiiForums #Governance #Uwajibikaji
2
Historia inasema mwanzoni mwa miaka ya 60, nchi nyingi za Afrika na Asia zilikuwa kwenye "level" moja ya kiuchumi na maisha. Lakini baada ya hapo, nchi kama Singapore zilichomoka na kuwaacha mbali wengine, wakibaki kwenye mstari uleule wa mwaka 1960!

Leo hii Singapore ni nchi ya 13 kwa uchumi mkubwa duniani. Je, unadhani hawa waliofanikiwa kusonga mbele walifanya nini cha tofauti?

Bofya, kushiriki kwenye mjadala huu https://jamii.app/PichaSingapore

#JamiiForums #Utawala #Uchumi
ZANZIBAR: Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Unguja Kaskazini, Benedict Mapujira amesema Mwanamtandao Ashly Robinson (#AshleeJenae), Raia wa Marekani alifia Hospitali alikowaishwa baada ya kukutwa na Mhudumu wa Hoteli akiwa amejinyonga katika chumba chake cha hoteli.

Nini maoni yako?

Fuatilia mjadala huu https://jamii.app/AshleeAlifiaHospitali

#JamiiForums #JFMatukio
1
Wadau mbalimbali wa JamiiForums.com kutoka Halmashauri tofauti nchini wanatoa wito kwa mamlaka husika kuwapatia barua za kuwathibitisha kazini, wakidai kuwa wanakosa baadhi ya stahiki za kiutumishi kwa wao kukosa barua za uthibitisho kazini.

Fuatilia mjadala https://jamii.app/UthibitishoWaajiriwaWapya

#JamiiForums #JFMdau2026 #Uwajibikaji

Nawe pia unaweza kuwasilisha Kero yako kupitia FichuaUovu ndani ya JamiiForums.com 📌