JamiiForums
35.5K subscribers
37.1K photos
2.92K videos
32.7K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
DAR: Mkurugenzi wa Gazeti la Pambazuko, Simon Mkina amesema; "Tumeripoti Polisi, wamekuja na kumchukua Mlinzi mmoja, wamemuhoji kisha wakamuachia. Mlinzi mwingine bado hajapatikana, pia kuna Kamera za CCTV nazo tumekabidhi kwa Jeshi la Polisi.”

Ameongeza; "Waliovunja hapa wanaonekana ni ‘professional’ kwa kuwa hata aina ya uvunjaji wao sio wa kuvunja kama wezi, bali wanajua walichokuwa wanafanya kwa kuwa ofisini hatuweki fedha, walivyoiba labda ndiyo vitu walivyokuwa wanataka."

Kupata taarifa zaidi tembelea https://jamii.app/UvamiziOfisiPambazuko

#JamiiForums #JFMatukio
KILIO CHA WATUMISHI WA UMMA: NDOA NA AFYA YA AKILI HATARINI!

Agizo la Dkt. Festo Dugange (TAMISEMI) kuwataka Watumishi kufanya kazi Miaka 3 bila uhamisho limeibua mjadala ndani ya JamiiForums.com. Wakati Serikali ikilenga kuboresha huduma mikoani, Watumishi wana kilio wakidai kuna urasimu na kuzuiliwa uhamisho (hasa wa kumfuata mwenza) kunavunja ndoa zao na kuwasababishia msongo mkubwa wa mawazo (depression).

Wadau wengine wanajiuliza, Mtumishi anayewaza kuvunjika kwa ndoa yake anawezaje kutoa huduma bora?

Mjadala umepamba moto ndani ya JamiiForums.com, wewe una maoni gani? Suluhisho ni nini?

Bofya hapa kusoma taarifa na kuishauri Serikali 👉🏾https://jamii.app/UhamishoWaWatumishi
1
Utafiti wa Cloudwards wa Mwaka 2026 unaeleza kwamba athari za kuvunja Sheria za Serikali kuhusu udhibiti wa maudhui hutofautiana kulingana na nchi, unajumuisha faini, au kukamatwa na kufungwa jela hasa katika maeneo yenye vizuizi vikali.

Aidha, Aprili 10, 2026, Rais Samia akiwa katika katika hafla ya uzinduzi wa minara 758 pamoja na uunganishaji wa Mkongo wa Mawasiliano katika wilaya 85 alisema kuwa Mawasiliano sio huduma ya Anasa bali ni Uti wa Mgongo wa Uchumi wa Kisasa

Una maoni gani? Bofya hapa kushiriki https://jamii.app/TanzaniaUhuruMtandao

#JamiiForums #HakiZaKidijitali #DigitalWorld
1
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Sekou Toure imesema Aprili 8, 2026 kulitokea hitilafu ya muda mfupi ya umeme (low voltage) kutoka kwenye chanzo kikuu cha umeme, Mkoa wa Mwanza hali iliyosababisha kushuka kwa uwezo wa kuendesha baadhi ya mashine na huduma muhimu za hospitali kuanzia Saa 6:00 Mchana hadi 8:00 Mchana.

Taarifa ya hospitali hiyo imeeleza baada ya tukio hilo jenereta tatu ziliwashwa kurudisha huduma zote kuendelea bila athari kwa wagonjwa na kwamba waliwasiliana na uongozi wa TANESCO ambao ulikiri kutokea kwa changamoto hiyo na kuwajulisha wanaifanyia kazi kwa haraka.

Ufafanuzi huo umetolewa baada ya Mdau wa JamiiForums.com kudai kumekuwa na changamoto ya umeme kukatika mara kwa mara siku tofauti na kusababisha baadhi ya huduma kusimama hospitalini hapo, akahoji hawana jenereta au miundombinu ni mibovu?

Zaidi https://jamii.app/UmemeHospitaliaMza

#JamiiForums #JFAfya #Uwajibikaji #PublicHealth
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
BEI ZA MAFUTA vs NAULI KUPANDA vs HALI YA UCHUMI YA WANANCHI...

Katibu Mkuu wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (#TABOA), Priscus John, ametoa kauli hiyo Aprili 10, 2026 Dar es Salaam, baada ya kukutana na Waziri wa Uchukuzi, Makame Mbarawa, na viongozi wa chama hicho.

Ikumbukwe April 8, 2026, Priscus alitoa taarifa kwa wananchi ambao hawajafanya 'booking' mpaka April 12 wasifanye, kwani hawawezi kuendelea kutoa huduma baada ya bei za mafuta kupanda mpaka pale serikali itakapokuja na suluhu, badala yake mabasi yangepelekwa kufanyiwa 'service'.

Una maoni gani juu ya hili Mdau?

Shiriki kwenye mjadala huu kupitia https://jamii.app/HatutagomaMadereva
PEMBA: Mdau wa JamiiForums.com anahoji mamlaka zinazohusika na ujenzi wa uwanja uliopo Mkoa wa Kaskazini, Wilaya ya wete, Shehia ya Pandani kwanini zielekeze kupekwa kwa nyasi kongwe sehemu ya kuchezea badala ya kuweka mpya? Kwamba hakuna bajeti ya kutosha au kuna mazingira ya upigaji?

Toa maoni yako kupitia https://jamii.app/UwanjaPemba

#JamiiForums #JFMdau2026 #Uwajibikaji #JFSports
Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (#TLS), Boniface Mwabukusi amevitaka vyombo vya dola na taasisi za usimamizi wa uchaguzi kutoa majibu ya haraka kuhusu kile alichokiita “mauaji ya halaiki” na miili ya raia iliyopotezwa Oktoba 29, 2025, akisisitiza kuwa taifa haliwezi kupona bila ukweli na uwajibikaji.

Fuatilia mjadala huu kupitia https://jamii.app/MauajiYaHalaiki

#JamiiForums #Uwajibikaji