JamiiForums
35.5K subscribers
37.1K photos
2.92K videos
32.7K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Mbunge wa Jimbo la Mchinga, Salma Kikwete, ameyasema hayo Aprili 9, 2026, wakati akiuliza swali Bungeni.

Kwa taarifa zaidi na kushiriki kwenye mjadala huu tembelea https://jamii.app/SalmaKikweteBarabara

#JamiiForums #Uwajibikaji #Governance
👎2
Taarifa ya Gerson Msigwa, Msemaji Mkuu wa Serikali imetolewa kufuatia Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kueleza uteuzi wa Angela Kizigha uliofanywa na Rais, Aprili 2, 2026 una mgongano na Masharti ya Ibara ya 50 ya Mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Wakati huohuo, James Milya (Simanjiro) na Dkt. Ng’waru Magembe (Mwanga) walichaguliwa kuwa Wabunge katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 wakiwa bado ni Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki.

Soma zaidi https://jamii.app/UfafanuziUteuziKizigha

#JamiiAfrica #Utawala #EAC #Governance
👎2
MWANZA: Mdau kutoka Jukwaa la Michezo ndani ya JamiiForums.com anatoa wito kwa mamlaka husika kufanya uchunguzi kwenye Klabu ya Pamba Jiji inayoshiri Ligi Kuu Bara kwani anahisi kuna ubadhirifu wa fedha klabuni hapo.

Una maoni gani kuhusu suala hili?

Shiriki mjadala kupitia https://jamii.app/UpigajiPambaJiji

#JamiiForums #JFSports #Uwajibikaji
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Rais Samia ameyasema hayo Aprili 10, 2026, alipokuwa akitoa maelekezo kwa Serikali katika hafla ya uzinduzi wa minara 758 pamoja na uunganishaji wa Mkongo wa Mawasiliano katika wilaya 85.

Fuatilia zaidi mjadala huu https://jamii.app/SamiaUrasimuHalmashauri

#JamiiForums #Uwajibikaji #JFHuduma #DigitalRights
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mohammed Khamis Abdulla, amesema hayo leo Aprili 10, 2026, katika hafla ya uzinduzi wa minara 758 pamoja na uunganishaji wa Mkongo wa Mawasiliano katika wilaya 85.

Una maoni gani juu ya hili Mdau?

Fuatilia zaidi mjadala huu https://jamii.app/Mawasiliano2030

#JamiiForums #Uwajibikaji #JFHuduma #DigitalRights
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mkurugenzi wa Udhibiti Uchumi wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (#LATRA), Abdallah Mhagama ametoa kauli hiyo Aprili 9, 2026 wakati wa mahojiano na Kituo cha Redio cha #RadioOne.

Yapi maoni yako Mdau?

Shiriki mjadala huu kupitia https://jamii.app/KufutiwaLeseni

#JamiiForums #Uwajibikaji #JFHuduma
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
PWANI: Jeshi la Polisi limesema taarifa inayosambaa kuwa Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Nassoro Mana aliyetoa taarifa mbele ya Waziri Mkuu, Mwigulu Nchemba (Februari 15, 2026 wakati wa ziara yake Wilayani Mkinga) ametoweka na hajulikani halipo, si taarifa ya kweli kwa kuwa yupo kituoni kwake Mkoa wa Pwani anaendela na majukumu.

Taarifa ya Polisi inaeleza Askari huyu alikuwa Tanga akihudhuria mashtaka ya Kijeshi kuanzia Februari 15, 2026 mpaka yalipokamilika na kutumwa kwenye mamlaka yenye maamuzi juu yake, na kwamba mkewe, Hawa Msuya anafahamu na alifika Tanga kuonana naye.

Polisi imeeleza kuwa Aprili 8, 2026 Askari huyo alipewa kibali cha safari kutoka Tanga kwenda kuripoti kituo chake cha kazi Pwani, na leo Aprili 10, 2026 ameripoti Ofisi ya Kamanda wa Polisi Pwani na kuelekezwa kurejea Polisi Wilaya ya Chalinze kuendelea na majukumu yake ya kazi.

Kwa taarifa zaidi tembelea https://jamii.app/KanushoAskariKutekwa

#JamiiForums #JFMatukio #Governance
DAR: Mkurugenzi wa Gazeti la Pambazuko, Simon Mkina amesema; "Tumeripoti Polisi, wamekuja na kumchukua Mlinzi mmoja, wamemuhoji kisha wakamuachia. Mlinzi mwingine bado hajapatikana, pia kuna Kamera za CCTV nazo tumekabidhi kwa Jeshi la Polisi.”

Ameongeza; "Waliovunja hapa wanaonekana ni ‘professional’ kwa kuwa hata aina ya uvunjaji wao sio wa kuvunja kama wezi, bali wanajua walichokuwa wanafanya kwa kuwa ofisini hatuweki fedha, walivyoiba labda ndiyo vitu walivyokuwa wanataka."

Kupata taarifa zaidi tembelea https://jamii.app/UvamiziOfisiPambazuko

#JamiiForums #JFMatukio
KILIO CHA WATUMISHI WA UMMA: NDOA NA AFYA YA AKILI HATARINI!

Agizo la Dkt. Festo Dugange (TAMISEMI) kuwataka Watumishi kufanya kazi Miaka 3 bila uhamisho limeibua mjadala ndani ya JamiiForums.com. Wakati Serikali ikilenga kuboresha huduma mikoani, Watumishi wana kilio wakidai kuna urasimu na kuzuiliwa uhamisho (hasa wa kumfuata mwenza) kunavunja ndoa zao na kuwasababishia msongo mkubwa wa mawazo (depression).

Wadau wengine wanajiuliza, Mtumishi anayewaza kuvunjika kwa ndoa yake anawezaje kutoa huduma bora?

Mjadala umepamba moto ndani ya JamiiForums.com, wewe una maoni gani? Suluhisho ni nini?

Bofya hapa kusoma taarifa na kuishauri Serikali 👉🏾https://jamii.app/UhamishoWaWatumishi
1
Utafiti wa Cloudwards wa Mwaka 2026 unaeleza kwamba athari za kuvunja Sheria za Serikali kuhusu udhibiti wa maudhui hutofautiana kulingana na nchi, unajumuisha faini, au kukamatwa na kufungwa jela hasa katika maeneo yenye vizuizi vikali.

Aidha, Aprili 10, 2026, Rais Samia akiwa katika katika hafla ya uzinduzi wa minara 758 pamoja na uunganishaji wa Mkongo wa Mawasiliano katika wilaya 85 alisema kuwa Mawasiliano sio huduma ya Anasa bali ni Uti wa Mgongo wa Uchumi wa Kisasa

Una maoni gani? Bofya hapa kushiriki https://jamii.app/TanzaniaUhuruMtandao

#JamiiForums #HakiZaKidijitali #DigitalWorld
1