JamiiForums
βœ”
35.6K subscribers
37.1K photos
2.92K videos
32.7K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (#CHADEMA), leo Aprili 9, 2026 kinafanya kongamano la Mtandaoni kuadhimisha Mwaka mmoja tangu kukamatwa kwa kiongozi wake, Tundu Lissu ambapo Katibu Mkuu wa Chama cha Orange Democratic Movement (#ODM) cha Kenya, Edwin Sifuna atakuwa mgeni rasmi.

Soma https://jamii.app/LissuUhainiKesi

#JamiiForums #HumanRights #Democracy
❀1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
ARUSHA: Watu wanaodhaniwa kuwa ni 'Makomandoo' wa Simba SC na Walinzi wa Uwanja wa Amri Abeid wamerushiana ngumi wakati msafara wa Simba SC ulipokuwa unaingia Uwanjani Saa 8:30 Mchana, leo Aprili 9, 2026 kabla ya kuanza kwa mchezo wa Ligi Kuu Bara timu hiyo inayovaana na TRA United. Chanzo cha tukio hilo hakijajuliana.

Zaidi https://jamii.app/MakomandooSimba

Video: Olakajr Sports

#JamiiForums #JFSports #LigiKuuBara
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Mbunge wa Jimbo la Gairo, Ahmed Shabiby, ameyasema hayo leo Aprili 9, 2026, wakati akichangia hoja Bungeni.

Zaidi https://jamii.app/BandariKwala

#JamiiForums #Uwajibikaji #Governance #JFUchumi
ARUSHA: Mambo yanaendelea kuwa magumu kwa Timu ya Simba katika mbio za kuwania Ubingwa wa Ligi Kuu Bara, hiyo ni baada ya kulazimishwa matokeo ya 0-0 dhidi ya TRA United kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Mchezo mwingine wa Ligi, Mbeya City na #AzamFC zimepata matokeo ya 0-0 kwenye Uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Manyara.

Matokeo hayo yanaifanya Simba kubaki nafasi ya pili ikiwa na pointi 36 katika michezo 17, ipo mbele ya Azam FC yenye alama 34 kwenye michezo 18, huku #Yanga ikiongoza kwa kuwa na alama 44 katika michezo 18. Upande wa TRA ipo nafasi ya 7 kwa alama 25 michezo 18.

Soma https://jamii.app/TRASimbaAprili

#JamiiForums #JFSports #JFLigiKuu2026
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Akichangia hoja Bungeni Aprili 9,2026, Mbunge wa Jimbo la Kisarawe, Suleiman Jafo amewasilisha pendekezo lenye lengo la kutatua changamoto ya ajira kwa Vijana nchini akisisitiza bado kuna haja ya mpango mahususi wa muda mrefu wa kuwaingiza wengi zaidi katika mfumo wa kazi.

Zaidi https://jamii.app/JafoAjiraVijana

#JamiiForums #Uwajibikaji #Governance
πŸ‘3
NJOMBE: Mdau wa JamiiForums.com anatoa wito kwa mamlaka husika kufanya usafi kuzunguka Kituo cha Afya cha Manda Wilayani Ludewa kwa kuwa hali ilivyo sasa siyo salama kiafya.

Zaidi tembelea https://jamii.app/UchafuKituoChaAfya

#JamiiForums #JFMdau2026 #Uwajibikaji #PublicHealth
❀1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR ES SALAAM: Mtandao wa Asasi za Kiraia nchini (CSOs) kupitia Kikundi Elekezi cha Wadau wa Utawala Tanzania (TG-MSG) umeitaka Tume ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani Wakati na Baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 inayoongozwa na Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Othman Chande kuacha kuchelewesha mchakato huo na badala yake kutoa ripoti kamili kwa umma.

Ikumbukwe, Tume hiyo ilisema Mamlaka ya Uteuzi imeridhia maombi yao ya muda wa ziada wa siku 21 ili kukamilisha kazi kabla au ifikapo Aprili 24, 2026, baadhi ya sababu zikitajwa kuwa ni kukamilisha uchambuzi wa ushahidi, kutoa fursa kwa Wataalamu wa uchunguzi wa Kisayansi kufanyia kazi baadhi ya vielelezo vipya vilivyowasilishwa.

Kupata taarifa zaidi tembelea https://jamii.app/LHRCTume

#JamiiForums #Uwajibikaji #HumanRights
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Mbunge wa Jimbo la Mchinga, Salma Kikwete, ameyasema hayo Aprili 9, 2026, wakati akiuliza swali Bungeni.

Kwa taarifa zaidi na kushiriki kwenye mjadala huu tembelea https://jamii.app/SalmaKikweteBarabara

#JamiiForums #Uwajibikaji #Governance
πŸ‘Ž2
Taarifa ya Gerson Msigwa, Msemaji Mkuu wa Serikali imetolewa kufuatia Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kueleza uteuzi wa Angela Kizigha uliofanywa na Rais, Aprili 2, 2026 una mgongano na Masharti ya Ibara ya 50 ya Mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Wakati huohuo, James Milya (Simanjiro) na Dkt. Ng’waru Magembe (Mwanga) walichaguliwa kuwa Wabunge katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 wakiwa bado ni Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki.

Soma zaidi https://jamii.app/UfafanuziUteuziKizigha

#JamiiAfrica #Utawala #EAC #Governance
πŸ‘Ž2
MWANZA: Mdau kutoka Jukwaa la Michezo ndani ya JamiiForums.com anatoa wito kwa mamlaka husika kufanya uchunguzi kwenye Klabu ya Pamba Jiji inayoshiri Ligi Kuu Bara kwani anahisi kuna ubadhirifu wa fedha klabuni hapo.

Una maoni gani kuhusu suala hili?

Shiriki mjadala kupitia https://jamii.app/UpigajiPambaJiji

#JamiiForums #JFSports #Uwajibikaji
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Rais Samia ameyasema hayo Aprili 10, 2026, alipokuwa akitoa maelekezo kwa Serikali katika hafla ya uzinduzi wa minara 758 pamoja na uunganishaji wa Mkongo wa Mawasiliano katika wilaya 85.

Fuatilia zaidi mjadala huu https://jamii.app/SamiaUrasimuHalmashauri

#JamiiForums #Uwajibikaji #JFHuduma #DigitalRights
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mohammed Khamis Abdulla, amesema hayo leo Aprili 10, 2026, katika hafla ya uzinduzi wa minara 758 pamoja na uunganishaji wa Mkongo wa Mawasiliano katika wilaya 85.

Una maoni gani juu ya hili Mdau?

Fuatilia zaidi mjadala huu https://jamii.app/Mawasiliano2030

#JamiiForums #Uwajibikaji #JFHuduma #DigitalRights