JamiiForums
35.6K subscribers
37.1K photos
2.92K videos
32.7K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
DAR: Ombi hilo limetolewa leo Aprili 8, 2026 katika Mkutano wa Wadau wa Usafirishaji ulioandaliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Ardhini (#LATRA), muda mchache baada ya Mamlaka hiyo kutangaza kuongeza muda wa wiki mbili zaidi wa kupokea maoni kuhusu mapitio ya nauli.

Soma zaidi https://jamii.app/DaladalaKusitishaUsafiri

#JamiiForums #Uwajibikaji #JFUchumi
1
MICHEZO: Licha ya kupewa nafasi kubwa ya kushinda kabla ya mchezo, timu ya #FCBarcelona imekutana na kipigo cha magoli 2-0 kwenye Uwanja wa Camp Nou kutoka kwa Atletico Madrid, ikiwa ni mchezo wa kwanza wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Mchezo mwingine wa hatua hiyo, PSG ikiwa nyumbani imeshinda 2-0 dhidi ya Liverpool ambayo haijapiga shuti hata moja langoni kwa wapinzani ambao wao walipiga mashuti 6. Timu hizo zinatarajiwa kurudiana wiki ijayo Aprili 14, 2026.

Zaidi https://jamii.app/UEFARoboFainali

#JFSports #JamiiForums #JFUEFA2026
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Janeth Magomi amesema wanachunguza tuhuma za baadhi ya Watu kudai wamejaziwa maji kwenye magari yao badala ya mafuta walipoenda kupata huduma katika Kituo cha Mafuta, Aprili 7, 2026.

Je, Mdau umewahi kukutana na kadhia hiyo? Unadhani nini kifanyike?

Fuatilia zaidi https://jamii.app/MagariKuwekwaMaji

#JamiiForums #Uwajibikaji #JFHuduma
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mwenyekiti wa Umoja wa Wasafirishaji Mkoa wa Mwanza, Yusuph Lupilya ameyasema hayo katika mkutano wa wadau wa usafirishaji uliondaliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Ardhini (#LATRA), jana Aprili 8, 2026.

Fuatilia mjadala https://jamii.app/UpigajiBeiMafuta

#JamiiForums #Uwajibikaji #Utawala #JFUchumi
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba ameyasema hayo Bungeni, Aprili 9, 2026 wakati akijibu swali la Mbunge wa Segerea, Agnesta Kaiza kuhusu utitiri wa michango kwenye Shule za Umma.

Ikumbukwe, Wadau mbalimbali wa JamiiForums.com kwa nyakati tofauti wamekuwa wakidai baadhi ya Shule za Umma na Walimu kadhaa wamekuwa wakilalamikia wingi wa michango, wakieleza inaongeza mzigo wa gharama kwa Wazazi na kuondoa dhana ya elimu bure.

Soma https://jamii.app/WarakaMichangoShuleni

#JamiiForums #Uwajibikaji #JFHuduma
2
MWANZA: Mdau wa JamiiForums.com anatoa wito kwa mamlaka husika kuchukua hatua dhidi ya kukatika mara kwa mara kwa umeme katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Sekou-Toure, kuangalia namna ya kuzuia kero hiyo ya kukatika-katika na pia kuboresha miundombinu ya kuwa na mbadala wa nishati hiyo inapokatika.

Zaidi https://jamii.app/UmemeSekouToure

#JamiiForums #JFMdau2026 #Uwajibikaji
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (#CHADEMA), leo Aprili 9, 2026 kinafanya kongamano la Mtandaoni kuadhimisha Mwaka mmoja tangu kukamatwa kwa kiongozi wake, Tundu Lissu ambapo Katibu Mkuu wa Chama cha Orange Democratic Movement (#ODM) cha Kenya, Edwin Sifuna atakuwa mgeni rasmi.

Soma https://jamii.app/LissuUhainiKesi

#JamiiForums #HumanRights #Democracy
1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
ARUSHA: Watu wanaodhaniwa kuwa ni 'Makomandoo' wa Simba SC na Walinzi wa Uwanja wa Amri Abeid wamerushiana ngumi wakati msafara wa Simba SC ulipokuwa unaingia Uwanjani Saa 8:30 Mchana, leo Aprili 9, 2026 kabla ya kuanza kwa mchezo wa Ligi Kuu Bara timu hiyo inayovaana na TRA United. Chanzo cha tukio hilo hakijajuliana.

Zaidi https://jamii.app/MakomandooSimba

Video: Olakajr Sports

#JamiiForums #JFSports #LigiKuuBara
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Mbunge wa Jimbo la Gairo, Ahmed Shabiby, ameyasema hayo leo Aprili 9, 2026, wakati akichangia hoja Bungeni.

Zaidi https://jamii.app/BandariKwala

#JamiiForums #Uwajibikaji #Governance #JFUchumi
ARUSHA: Mambo yanaendelea kuwa magumu kwa Timu ya Simba katika mbio za kuwania Ubingwa wa Ligi Kuu Bara, hiyo ni baada ya kulazimishwa matokeo ya 0-0 dhidi ya TRA United kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Mchezo mwingine wa Ligi, Mbeya City na #AzamFC zimepata matokeo ya 0-0 kwenye Uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Manyara.

Matokeo hayo yanaifanya Simba kubaki nafasi ya pili ikiwa na pointi 36 katika michezo 17, ipo mbele ya Azam FC yenye alama 34 kwenye michezo 18, huku #Yanga ikiongoza kwa kuwa na alama 44 katika michezo 18. Upande wa TRA ipo nafasi ya 7 kwa alama 25 michezo 18.

Soma https://jamii.app/TRASimbaAprili

#JamiiForums #JFSports #JFLigiKuu2026
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Akichangia hoja Bungeni Aprili 9,2026, Mbunge wa Jimbo la Kisarawe, Suleiman Jafo amewasilisha pendekezo lenye lengo la kutatua changamoto ya ajira kwa Vijana nchini akisisitiza bado kuna haja ya mpango mahususi wa muda mrefu wa kuwaingiza wengi zaidi katika mfumo wa kazi.

Zaidi https://jamii.app/JafoAjiraVijana

#JamiiForums #Uwajibikaji #Governance
👍3
NJOMBE: Mdau wa JamiiForums.com anatoa wito kwa mamlaka husika kufanya usafi kuzunguka Kituo cha Afya cha Manda Wilayani Ludewa kwa kuwa hali ilivyo sasa siyo salama kiafya.

Zaidi tembelea https://jamii.app/UchafuKituoChaAfya

#JamiiForums #JFMdau2026 #Uwajibikaji #PublicHealth
1