JamiiForums
34.7K subscribers
37.3K photos
2.95K videos
32.8K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Je, unakubaliana na hoja ya mdau kuwa mafanikio siku hizi ni bahati tu? Au nguvu ya kupambana bado ina nafasi yake?

Ungana na wadau wengine https://jamii.app/MaishaBoraSiBidii

#JamiiForums #Lifestyle #MorningPost #AmkaNaJF
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Usikose kujiunga nasi Machi 30, 2026, kuanzia Saa 12:00 Jioni hadi Saa 2:00 Usiku kupitia Instagram Live ya JamiiForums katika mjadala wa “Mchakato wa Uhakiki wa Taarifa kwenye Vyombo vya Habari unaendana na kasi ya kuenea kwa Taarifa Potofu?”

#MisinformationAndDisinformation #HakikiTaarifa #FactsChecking #JamiiCheck
Chama cha Wanahabari nchini Uganda (UJA) kimelaani vikali kitendo hicho, kikidokeza kuwa kutekwa kwa Arnold Mukose ni shambulio dhidi ya uhuru wa habari na usalama wa Wanahabari wanapotekeleza majukumu yao.

Zaidi: https://jamii.app/MwandishiUganda

#JamiiForums #Democracy #PressFreedom #Accountability
ZANZIBAR: Mdau wa JamiiForums.com ametoa wito kwa mamlaka za Shehia ya Jang'ombe na Kidongo Chekundu pamoja na Baraza la Manispaa Mjini kushughulikia kero ya takataka zilizotelekezwa katika jalala la Jang'ombe na Kidongo Chekundu kabla hazijaleta madhara makubwa ya Afya kwa wakazi wa eneo hilo

Bofya https://jamii.app/UchafuZanzibar

#JamiiForums #JFMdau2026 #Uwajibikaji
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (#TAKUKURU), Crispin Chalamila akisoma Taarifa ya Utendaji wa taasisi hiyo Mwaka 2024/2025, leo Machi 30, 2026 katika Ikulu Dar es Salaam.

Zaidi https://jamii.app/RipotiTAKUKURU2026

#JamiiForums #Uwajibikaji #TAKUKURUReport2026
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (#TAKUKURU), Crispin Chalamila akitaja idadi ya kesi zinazohusu rushwa zilizofikishwa Mahakamani wakati akisoma Taarifa ya Utendaji wa TAKUKURU ya Mwaka 2024/2025, leo Machi 30, 2026 katika Ikulu Dar es Salaam.

Zaidi https://jamii.app/RipotiTAKUKURU2026

#JamiiForums #Uwajibikaji #TAKUKURUReport2026
TANZIA: Aliyewahi kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jimbo la Kilwa Kusini kupitia Chama cha CUF, Seleman Said Bungara maarufu kwa jina la Bwege, amefariki Dunia, Machi 30, 2026 akiwa hospitali ambako alikuwa akipatiwa matibabu.

Enzi za uhai wake Bwege amewahi kutumikia vyama vya Siasa vya CUF, ACT Wazalendo na hivi karibuni ilidaiwa alikuwa mbioni kujiunga na CHADEMA, ingawa mchakato rasmi wa kukabidhiwa kadi ya chama hicho ulikuwa haujakamilika.

Zaidi https://jamii.app/RIPBwege

#JamiiForums #RIPBwege
2
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), CPA Charles E. Kichere akisoma Ripoti ya ofisi yake ya Mwaka 2024/2025, leo Machi 30, 2026, Ikulu Dar es Salaam ametaja taasisi zenye Hati Mbaya, Hati Zenye Mashaka na ambazo ameshindwa kutoa maoni.

Zaidi https://jamii.app/CAGHatiMbaya

#JamiiForums #Uwajibikaji #TAKUKURUReport2026
1
Kujua hili na mengine mengi, usiache kujiunga nasi katika Mjadala wa “Mchakato wa Uhakiki wa Taarifa kwenye Vyombo vya Habari unaendana na kasi ya kuenea kwa taarifa potofu?” Jumatatu ya Machi 30, 2026, kuanzia Saa 12:00 Jioni hadi Saa 2:00 Usiku kupitia Instagram Live ya JamiiForums.

#MisinformationAndDisinformation #HakikiTaarifa #FactsChecking #JamiiCheck
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere akisoma ripoti ya ofisi yake ya Mwaka 2024/2025, Machi 30, 2026 amesema alibaini upungufu katika mradi wa ujenzi wa Uwanja wa Mpira wa Arusha, ambapo ulikadiriwa kugharimu Tsh. Bilioni 187 lakini mkataba ukasainiwa kwa Tsh. Bilioni 338.

Soma https://jamii.app/CagUwanjaArusha

#JamiiForums #Uwajibikaji #RipotiCAG #JFSports
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), CPA Charles E. Kichere amegusia changamoto za Mradi wa Kufua Umeme wa Bwawa la Mwalimu Nyerere na kueleza kuwa umesababisha hasara ya Tsh. Trilioni 1.48 kutokana na kushindwa katika Baraza la Usuluhishi.

Ameeleza hayo katika Ripoti ya ofisi yake ya Mwaka 2024/2025, leo Machi 30, 2026, Ikulu Dar es Salaam.

Zaidi https://jamii.app/BwawaHasaraTANESCO

#JamiiForums #Uwajibikaji #RipotiCAG
1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), CPA Charles Kichere ya Mwaka 2024/2025 iliyosomwa leo Machi 30, 2026, Ikulu Dar es Salaam imeonesha Deni la Serikali hadi Juni 30, 2025 lilikuwa ni Tsh. Trilioni 110.05 ambapo ndani ya Mwaka mmoja limeongezeka kwa Tsh. Trilioni 12.7 sawa na Asilimia 13.04.

Zaidi https://jamii.app/DeniLaSerikali2025

#JamiiForums #Uwajibikaji #TAKUKURUReport2026
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Akizungumza Machi 30, 2026, wakati anapokea Taarifa ya Mwaka ya Tathmini ya Utendaji Kazi wa Ununuzi wa Umma, Rais Samia ameiagiza Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) kuanza utaratibu wa kuanika hadharani taasisi za umma zinazofanya vibaya katika usimamizi wa fedha na ununuzi, akisema hatua hiyo itaongeza uwajibikaji.

Zaidi: https://jamii.app/SamiaRipoti

#JamiiForums #Uwajibikaji #PPRAReport2026
Jiunge nasi leo Machi 30, 2026 kupitia Instagram Live ya JamiiForums kuanzia saa 12 jioni hadi saa 2 usiku katika mjadala wa “Mchakato wa Uhakiki wa Taarifa kwenye Vyombo vya Habari unaendana na kasi ya kuenea kwa Taarifa Potofu?” ambapo tutajadili nafasi ya teknolojia, changamoto pamoja na mbinu zinazotumiwa na vyombo vya habari katika kupambana na taarifa potoshi.

#JamiiForums #MisinformationAndDisinformation #HakikiTaarifa #HakikiKablaYaKupost
#FactsChecking #JamiiCheck
TUPO LIVE KUPITIA JAMIICHECK!!! 🔥📌🔨

Jiunge nasi leo Machi 30, 2026 kupitia Instagram Live ya JamiiCheck kuanzia saa 12 jioni hadi saa 2 usiku katika mjadala wa “Mchakato wa Uhakiki wa Taarifa kwenye Vyombo vya Habari unaendana na kasi ya kuenea kwa Taarifa Potofu?” ambapo tutajadili nafasi ya teknolojia, changamoto pamoja na mbinu zinazotumiwa na vyombo vya habari katika kupambana na taarifa potoshi.

Kushiriki Bofya instagram.com/JamiiCheck

#JamiiForums #MisinformationAndDisinformation #HakikiTaarifa #HakikiKablaYaKupost
#FactsChecking #JamiiCheck
2