JamiiForums
33.9K subscribers
37.3K photos
2.98K videos
32.8K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Mdau, unakumbuka nini kuhusu matukio ya aina hii?

Zaidi tembelea https://jamii.app/NidhamuKipaYanga

#JamiiForums #JFMdau2026 #Uwajibikaji #JFSports
DAR: Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (#CHADEMA), Tundu Lissu ambaye amekaa gerezani kwa zaidi ya miezi 11 tangu alipokamatwa Aprili 9, 2025 Mbinga Mkoani Ruvuma amewasilisha maombi Mahakama ya Rufaa akiomba kesi yake ya uhaini isikilizwe kwa dharura kutokana na afya yake kuzorota.

Zaidi bofya https://jamii.app/LissuBaruala

#JamiiForums #JFSheria #JFMatukio
Timu ya #Simba imeichapa #TRAUnited magoli 3-0 katika mchezo wa Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo na hivyo kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kukimbizana na #Yanga (inaongoza ligi, pointi 38 michezo 16) katika kuwania ubingwa.

Matokeo hayo yanaifanya Simba ambayo imefikisha michezo 14 kushika nafasi ya pili kwa kuwa na alama 31 wakati TRA United ambayo inamilikiwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imebaki nafasi ya 10 kati ya timu 16 ikiwa na pointi 20 katika mechi 16.

Zaidi https://jamii.app/SimbaTRA

#JamiiForums #JFSports #JFLigiKuu2026
ENGLAND: Ndoto za #Arsenal kubeba mataji manne msimu huu wa 2025/26 zimeyeyuka baada ya kupoteza Kombe la EFL (Carabao Cup) kwa kufungwa Magoli 2-0 na #ManchesterCity inayonolewa na Kocha Pep Guardiola katika Fainali iliyopigwa kwenye Uwanja wa Wembley, Machi 22, 2026.

Magoli yote yameweka wavuni na Nico O'Reilly dakika ya 60 na 64, hivyo kuifanya Arsenal inayonolewa na Mikel Arteta kubaki kwenye mataji matatu msimu huu ambayo ni Premier League, Ligi ya Mabingwa Ulaya na Kombe la FA.

Timu zilizotwaa Carabao Cup mara nyingi:
1. Liverpool - 10
2. Man City - 9
3. Man United - 5
4. Aston Villa - 5
5. Tottenham  - 4
6. Nottingham  - 4
7. Leicester City - 3
8. Arsenal - 2
9. Norwich City - 2
10. Birmingham – 2

Zaidi https://jamii.app/EFLCupFinal

#JamiiForums #JFSports #EFL2026
2
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Padre Prosper Kessy aliyasema hayo wakati akitoa semina katika Mafungo ya WAWATA yaliyofanyika katika Kanisa Kuu la Moyo Safi wa Bikira Maria, Jimbo Katoliki la Bagamoyo, Machi 14, 2026.

Zaidi: https://jamii.app/PadreKessySiri

#JamiiForums #Uwajibikaji #UtawalaBora
DAR ES SALAAM: Mdau wa JamiiForums.com anadai Bodaboda wanaofika maeneo ya Kariakoo wanakumbana na kero ya Pikipiki zao kukamatwa na Maafisa ambao wanawadai fedha taslim, anazitaka mamlaka husika zifuatilie na kuchukua hatua kwani ni uonevu mkubwa.

Zaidi https://jamii.app/KukamataWrongParking"

#JamiiForums #JFMdau2026 #Uwajibikaji
UGANDA: Mashtaka hayo yaliwasilishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkuu ya Kasangati ikitaka amri ya kudumu itakayozuia Serikali au Mawakala wake kuingilia uhuru wa familia ya #BobiWine na kuwajibishwa kwa yeyote aliyehusika na ukiukwaji wa Haki za Binadamu.

Zaidi https://jamii.app/WanasheriaUganda

#JamiiForums #HumanRights #Democracy #AfricanPolitics