JamiiForums
33.9K subscribers
37.3K photos
2.98K videos
32.8K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Mwanafunzi wa Sheria katika Law Development Centre (LDC), Gloria Grace Laker amekana mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mirriam Amoro, lakini jitihada zake za kupata dhamana hazikufanikiwa, na Mahakama imeamuru abaki mahabusu hadi Machi 17, 2026 kesi yake itakaposikilizwa tena

Kwa taarifa zaidi tembelea https://jamii.app/KesiBobiWine

#JamiiForums #Utawala #AfricanPolitics
DAR: Mdau wa JamiiForums.com ametoa wito kwa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo na Mamlaka nyingine zinazohusika kutatua kero ya foleni katika Barabara ya Mabibo Sokoni akidai imekuwa na usumbufu kwa watumiaji wa barabara hiyo kutokana na upangiliaji mbovu wa maegesho.

Fuatilia zaidi https://jamii.app/BarabaraMabibo

#JamiiForums #JFMdau2026 #JFHuduma
1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Wakili wa kujitegemea, Peter Madeleka ameyasema hayo Machi 13, 2026 kwenye kipindi cha Jambo Asubuhi cha Jambo TV.

Kwa taarifa zaidi https://jamii.app/MadelekaKatiba

#JamiiForums #Siasa #Utawala #KatibaMpya
Ikumbukwe kuwa Mwaka 2025 Umoja wa Mataifa uliitaka Serikali ya Eritrea kuwaachia huru takriban Watu 10,000 wanaodaiwa kushikiliwa bila kufikishwa Mahakamani, na kuachiliwa kwa Biniam kunakuja katika kipindi ambacho Serikali hiyo imeripotiwa kuanza kuwaachilia huru baadhi ya wafungwa waliokuwa wamekamatwa kwa muda mrefu.

Fuatilia zaidi: https://jamii.app/MchoraKatuniEritrea

#JamiiForums #HakiZaBinadamu #HumanRights
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
ARUSHA: Kutokana na Mvua kubwa kunyesha, mechi iliyokuwa ichezwe leo Machi 14, 2026 kati ya TRA United dhidi ya Simba SC kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid imeahirishwa baada ya uwanja kujaa maji na mpira kushindwa kudunda.

Kamishna wa mchezo huo, Mussa Nyamandege ametangaza maamuzi hayo baada ya kufanya kikao na wawakilishi wa timu zote mbili.

Ikumbukwe, Msimamo wa Ligi Kuu Bara unaonesha Simba SC ina alama 27 ikiwa nafasi ya nne, TRA United ina alama 19 ipo nafasi ya 9.

Zaidi https://jamii.app/MechiKuahirishwa

#JamiiForums #JFSports #JFMatukio #JFLigiKuu2026

Video: Bonga Pluss
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Mdau, ni somo gani ulikuwa unajiuliza kwanini unasoma, ukihisi labda halitakuja kukusaidia baadaye maishani? Kwa nini uliona halina umuhimu?

Tembelea Jukwaa la Elimu ndani ya JamiiForums.com kushiriki mijadala mingine.

Kuona maoni ya Wadau JF tembelea https://jamii.app/JukwaaElimu

#JamiiForums #JFChitChat #JFElimu
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR ES SALAAM: Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Paul Makonda amezitaka timu kuwekeza nguvu kwenye mazoezi na kutafuta wachezaji wazuri ili kuacha kutegemea vitendo vya kishirikina katika kutafuta ushindi.

Fuatilia zaidi https://jamii.app/UshirikinaUwanjani

#JamiiForums #JFSports
Mdau wa JamiiForums.com ametoa wito kwa Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kutoa orodha ya majina ya Watumishi ambao majibu ya uhamisho yametumwa kwa waajiri wao, akidai kumekuwepo na changamoto katika ufuatiliaji wa vibali tangu tangazo kutolewa.

Fuatilia zaidi https://jamii.app/OrodhaVibaliWatumishi

#JamiiForums #JFMdau2026 #JFHuduma #Accountability

Nawe pia unaweza kuwasilisha KERO yako kupitia FichuaUovu ndani ya JamiiForums.com📌📌
Mdau, wewe ulikutana na kitu gani ukajisemea kutoboa hapo ni ndoto?😃

Fuatilia zaidi https://jamii.app/SokoLaAjira

#JamiiForums #JFMdau2026 #Maisha