JamiiForums
34K subscribers
37.3K photos
2.97K videos
32.8K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
PWANI: Baada ya Mdau wa JamiiForums.com kutoa Kero ya Maji wanayopitia Wakazi wa Mtaa wa Muheza, MailiMoja - Kibaha, ufafanuzi umetolewa.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa #DAWASA, Everlasting Lyaro amesema, “Ni kweli Mtaa wa Muheza bado kuna changamoto ya huduma ya maji, eneo hilo ni miongoni mwa maeneo yanayosubiri Mradi wa PANGANI.”

Ameongeza, “DAWASA inafikiria mpango wa kuchimba kisima kirefu ili kianze kuhudumia Wananchi wa maeneo hayo, tunaomba Wananchi wawe na uvumilivu wakati tunaendelea na mipango ya uboreshaji huduma.

Zaidi tembelea https://jamii.app/DAWASAKibaha

#JamiiForums #Uwajibikaji #JFMdau2026 #JFHuduma
1
Mdau wa JamiiForums.com ametoa ushauri kuhusu changamoto ya foleni katika Jiji la Dar es Salaam, je, yapi maoni yako?

Zaidi tembelea https://jamii.app/FoleniDar

#JamiiForums #JFMdau2026 #Uwajibikaji
Machi 7, 2026: Moja kati ya mijadala inayoendelea ndani ya JamiiForums (Jukwaa la MMU).

Nini maoni yako?😊

#JamiiForums #JFChitChat #JFMaisha
Je, unakubaliana na Mdau?😃

Zaidi tembelea https://jamii.app/PesaMkopo

#JamiiForums #JFChitChat
1
Tag Wanawake 3 unaowakubali uwape Maua yao leo katika Siku ya Wanawake Duniani

Zaidi tembelea https://jamii.app/IntWomensDay

#JamiiForums #JFWomen #InternationalWomensDay
1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
MARA: Jeshi la Polisi Musoma limetumia mabomu ya machozi kuwatawanya Baraza la Wanawake la Chadema (#BAWACHA) waliokusanyika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani, leo Machi 8, 2026.

Tukio hilo limetokea wakati Wanachama hao walipokuwa katika kongamano la Siku ya Wanawake, ambapo Polisi walizunguka eneo hilo na kuingilia kati kwa kutumia mabomu hayo.

Taarifa iliyotolewa kwenye kurasa rasmi za #CHADEMA imesema hatua ya Polisi ilikuwa ya ghafla. Aidha, Katibu Mkuu wa BAWACHA Pamela Maassay na baadhi ya viongozi na Wanachama wamekamatwa na Jeshi la Polisi.

Zaidi https://jamii.app/BawachaPolisi

#JamiiForums #Demokrasia #InternationalWomensDay
👎2
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
SIMIYU: Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (#CCM), Kenani Kihongosi, ameyasema hayo Machi 7, 2026  katika mkutano wa hadhara uliofanyika Wilayani Maswa.

Shiriki https://jamii.app/KihongosiWanagombana

#JamiiForums #Siasa
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
TABORA: Jeshi la Polisi linawashikilia Wanafunzi 17 wa Chuo cha Ardhi kwa tuhuma za kumshambulia na kumjeruhi mlinzi wa chuo hicho, pamoja na kuwatishia Wanafunzi wenzao kwa kutumia silaha za ncha kali (visu).

Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paulo Chacha Machi 7, 2026 ameagiza uongozi wa chuo hicho kuwasimamisha masomo mara moja Wanafunzi hao wakati mchakato wa kuwafikisha Mahakamani ukiendelea, baada ya kubainika kuwa wanajihusisha na vitendo vya uvunjifu wa amani vinavyohatarisha usalama wa chuo.

Soma https://jamii.app/WanafunziMlinzi

#JamiiForums #Uwajibikaji #JFMatukio
1
DAR: Mdau wa JamiiForums.com ametoa wito kwa uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kusimamia matengenezo ya magari mabovu ili kurahisisha huduma kwa wateja na kuboresha utendaji kazi wa wafanyakazi.

Zaidi https://jamii.app/KeroMuhimbili

#JamiiForums #Accountability #JFMdau2026
Mdau anatoa wito kwa mamlaka za juu kuboresha miundombinu ya Zahanati ya Mbuchi Wilayani Kibiti kwa kuwa mazingira yake siyo rafiki kwa Watumiaji wote.

Soma https://jamii.app/KituoChaAfyaMbuchi

#JamiiForums #JFMdau2026 #Uwajibikaji #JFHuduma

Nawe pia unaweza kuwasilisha Kero yako kupitia FichuaUovu ndani ya JamiiForums.com📌📌