JamiiForums
33.2K subscribers
37.5K photos
3K videos
32.9K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
RUVUMA: Machi 28, 2025, Mdau wa JamiiForums.com alilalamikia kuhusu Soko la Bombambili kuwa na miundombinu mibovu na hali kuwa mbaya zaidi wakati wa mvua, Juni 15, 2025, Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea akakabidhi mradi kwa Mkandarasi ili kujenga Soko la Kisasa ili kukidhi mahitaji, lakini hadi Desemba 2025 mradi huo haujaanza rasmi.

Zaidi soma https://jamii.app/SokoLaBombambili

#JamiiForums #JFUwajibikaji #Governance #HudumaZaJamii
2
Desemba 27, 2025: Mojawapo kati ya mijadala mingi inayoendelea ndani ya JamiiForums.com muda huu 📌

Zaidi bofya https://jamii.app/ChandeUshahidi

#JamiiForums #Uwajibikaji
AFCON 2025: Mchezo wa Kundi C kati ya Timu ya Taifa ya #Uganda dhidi ya #Tanzania matokeo bado ni 0-0 hadi mapumziko.

Tembelea JamiiForums.com kwa mjadala zaidi.

#JamiiForums #JFSports #JFAFCON2025
MOROCCO: Timu ya Taifa ya #Tanzania “Taifa Stars” imeendeleza rekodi yake ya kutoshinda mchezo wa Michuano ya AFCON kwa kupata sare ya Goli 1-1 dhidi ya Uganda katika mchezo wa Kundi C.

Mchezo ujao wa Kundi, Tanzania itaivaa Tunisia wakati Uganda itacheza dhidi ya Nigeria, michezo yote ikichezwa Desemba 30, 2025.

Tanzania ilishiriki kwa mara ya kwanza michuano hiyo Mwaka 1980, kisha 2019 na 2024 ambapo haijawahi kushinda mchezo hata mmoja, ikifungwa mechi 7 na sare 3, mchezo wa Uganda unakuwa sare ya nne kwa jumla.

Zaidi https://jamii.app/Uganda1Tanzania1

#JamiiForums #JFSports #JFAFCON2025
2
Disemba 28, 2025: Moja kati ya mijadala mingi inayoendelea ndani ya JamiiForums.com wakati huu📌

Zaidi tembelea https://jamii.app/Rweyongeza

#JamiiForums #Accountability #Governance #UtawalaBora
1
Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (#TAZARA) imetangaza mpango wake wa muda mrefu wa kuifufua reli hiyo umeingia hatua ya utekelezaji kwa Mkataba wa thamani ya Dola Bilioni 1.4 (Takriban Tsh. Trilioni 3.7) na Kampuni ya China Civil Engineering Construction Corporation (CCECC), kwaajili ya kusimamia na kuendesha reli hiyo kwa Kipindi cha Miaka 30.

Zaidi https://jamii.app/ChinaTazaraMiaka30

#JamiiForums #ServiceDelivery
👏2
Mshambuliaji wa Timu ya #Tanzania “Taifa Stars”, Simon Happygod Msuva ameifikia rekodi ya #Mrisho Ngassa ya kufunga Magoli 25 katika timu hiyo na hivyo kuwa wachezaji waliofunga Magoli mengi ngazi ya timu ya Taifa.

Msuva amefikia rekodi hiyo kwa kufunga kwa njia ya penati katika mchezo dhidi ya Uganda wa Kundi C katika Michuano ya #AFCON2025, Desemba 28, 2025 Nchini Morocco.

Pia, Msuva ambaye amewahi kupita katika Klabu kadhaa zikiwemo Azam FC, Yanga, Wydad C kwa sasa anaitumikia Al-Talaba SC na amefunga Magoli matatu katika Michuano tofauti ya AFCON tangu alipoanza kucheza Mwaka 2019 na 2024.

Zaidi https://jamii.app/MsuvaNaNgassa

#JamiiForums #JFSports #JFAFCON2025
4👍1
PWANI: Mdau wa JamiiForums.com ameelezea kero ya ubovu wa barabara ya Kibaha Mailimoja maeneo ya Mang’umbi hadi Tankini akidai kumekuwa na ahadi za viongozi zisizotekelezwa licha ya usumbufu mkubwa hasa wakati wa mvua.

Zaidi: https://jamii.app/KibahaMitaa

#JamiiForums #JFHuduma #Accountability #JFMdau2025