JamiiForums
55.4K subscribers
33.4K photos
2.03K videos
30.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
#BUNGENI: Leo Juni 11, 2025, Mbunge wa Kinondoni Abbas Tarimba amependekeza wabunge wapewe 'plate number' maalumu zitakazowatambulisha Barabarani kwenye misafara au kwenye shughuli zao za kila siku

Zaidi https://jamii.app/WabungeSpecialPlateNumbers

#JamiiForums #JamiiAfrica #Accountability #Uwajibikaji #Kuelekea2025 #Governance
Aliyekuwa Jaji Mkuu wa Kenya, Dkt. Willy Mutunga, Wakili Mwandamizi Martha Karua, pamoja na watu wengine wanne wamefungua kesi katika Mahakama ya Haki ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EACJ) dhidi ya Serikali ya Tanzania, wakidai kuwekwa kizuizini kinyume cha Sheria, kunyimwa kuingia nchini na kufukuzwa kati ya Mei 18 hadi 19, 2025, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam

Kundi hilo ambalo pia linajumuisha Wanaharakati na Watetezi wa Haki za Binadamu wanne ambao ni Gloria Kimani, Lynn Ngugi, Hussein Khalid na Hanifa Adan wamedai kuwa haki zao kama raia wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zilikiukwa waziwazi walipozuiwa kuingia Tanzania kushuhudia kesi ya uhaini dhidi ya Kiongozi wa Upinzani, Tundu Lissu

Aidha, Kesi hiyo inatarajiwa kuhamishiwa Makao Makuu ya EAC - Arusha ambako tarehe ya kusikilizwa itapangwa na Mahakama hivi karibuni

Soma https://jamii.app/KenyaKuiburuzaTZ

#JamiiForums #JamiiAfrica #Diplomasia
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Akizungumza #Bungeni, leo Juni 11, 2025, Naibu Spika wa Bunge, Mussa Azzan Zungu amesema Jengo la Bunge ni la Wananchi na hakuna Mwananchi anayekatazwa kutembelea hivyo ni lazima kuwe na Utaratibu wa Kiusalama kwa Wabunge wenyewe na Wageni, akisisitiza suala la Wabunge kukaguliwa ni la muhimu na lazima

Soma https://jamii.app/ZunguUsalamaBungeni

#JamiiForums #Governance #JamiiAfrica
KENYA: Bunge la Seneti limesitisha shughuli zake za kawaida ili kujadili na kujibu maswali kuhusu uchunguzi wa kifo cha Albert Ojwang, ambapo Waziri wa Mambo ya Ndani, Kipchumba Murkomen, Mkuu wa Polisi Douglas Kanja, na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Jinai (DCI) Amin Mohammed walikuwepo Bungeni kujibu maswali kuhusu kesi hiyo

Katika kikao hicho kilichorushwa moja kwa moja kwenye Vyombo vya Habari, Makamu Mwenyekiti wa IPOA, Anne Wanjiku, ameliambia Bunge kuwa Mifumo ya CCTV katika ofisi ya Mkuu wa Kituo Kikuu cha Polisi alipokuwa akishikiliwa Albert ilichezewa, huku akiongeza kuwa uchunguzi wa awali kuhusu kifo hicho unatupilia nadharia kuwa Albert alijiua

Soma https://jamii.app/KikaoBungeKE

#JamiiAfrica #JamiiForums #Accountability #Uwajibikaji #Governance #HumanRights
Mdau wa Jukwaa la 'JF Chit chats and Jokes' ndani ya JamiiForums.com ameanzisha Mjadala akihoji ni nani akija nyumbani kwako bila kukupa taarifa hutakuwa na tatizo naye?

Mjadala https://jamii.app/Kutembeleana

#JamiiForums #JamiiAfrica #Maisha #LifeStyle
SINGIDA: Baada ya Mdau wa JamiiForums.com kudai baadhi ya Maafisa Utumishi na Ofisi ya Mkurugenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama wanachelewa kupitisha barua za uhamisho wa Watumishi na kutoa wito kwa UTUMISHI au TAMISEMI kufuatilia na kuchukua hatua, ufafanuzi umetolewa

Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama imesema inatekeleza mchakato wa uhamisho wa Watumishi kwa mujibu wa taratibu na Kanuni za Utumishi wa umma kupitia Mfumo rasmi wa maombi ya Uhamisho (Employee Self Service ESS)

Kuhusu Watumishi wanaohama kufuata wenza wao, Halmashauri hiiyo imeeleza mara ya mwisho walipokea barua Mei 2025 na zile zilizokidhi vigezo zimepitishwa na wahusika wamekabidhiwa kwa ajili ya Utekelezaji

Soma https://jamii.app/MkalamaDC

#JamiiForums #Accountability #Governance #JamiiAfrica #Uwajibikaji
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Akizungumza na Wanahabari, leo Juni 11, 2025, Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema "Wakati mwingine unaona vikampeni havina mbele wala nyuma. Vijana tutumie mitandao kwa njia za kimanufaa, ukifanya makosa tutakupata tu, jinai haifi."

Ameongeza “Tunaelekea katika Uchaguzi, mihemko imekuwa mingi, uhamasishaji wa Kijingajinga umekuwa mwingi, Vijana ‘watch out’, ukikamatwa utakuwa peke yako.”

Soma https://jamii.app/MsigwaKuhusuMitandao

#JamiiForums #DigitalRights #Governance #Kuelekea2025
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
TABORA: Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora limekanusha kuwa mtu aliyetambulika kuwa Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Igunga aliyeonekana akimuomba msamaha Makamu Mwenyekiti wa #CHADEMA, John Heche, si mtumishi wa Jeshi hilo

Kamanda wa Polisi Mkoa, Richard Abwao, amesema baada ya msako wamemkamata mtu huyo aliyetambulika kwa jina la Daud Paul Delim (49), Mkazi wa Mbagala A Wilayani Igunga aliyejifanya ni Mkuu wa Kituo cha Polisi

Ameongeza kuwa anaendelea kuhojiwa ili kujua alioshirikiana nao kuandaa picha mjongeo hiyo hasi na potofu na kuisambaza ili hatua stahiki za kisheria dhidi yao zichukuliwe

Soma https://jamii.app/RPCTabora

#JamiiAfrica #JFMatukio #JamiiForums
KENYA: Katika Kikao maalum cha Bunge cha kujadili suala hilo, IGP Douglas Kanja aliomba radhi kwa niaba ya Jeshi la Polisi na aliahidi kuwachukulia hatua maafisa waliompatia ripoti hiyo baada ya Uchunguzi wa Wasimamizi wa Utendaji wa Polisi (IPOA), akisema kuwa taratibu za kinidhamu zitafuata Miongozo ya Utendaji Kazi

Aidha, Wabunge walimhoji ni nani aliyechezea Mfumo wa CCTV Kituoni hapo siku hiyo ya tukio na kwa nini Ojwang alihamishwa kutoka Homa Bay hadi Nairobi, ambapo alisema
IPOA bado inachunguza eneo lote la uhalifu na itatoa ripoti kamili ya kilichoukumba Mfumo wa CCTV

Soma https://jamii.app/IGPAombaRadhi

#JamiiAfrica #JamiiForums #Accountability #Uwajibikaji #HumanRights
Leo Juni 12, 2025 #BajetiKuu ya Serikali kwa Mwaka 2025/26 inatarajiwa kusomwa Bungeni

Mdau, unadhani Serikali itawekeza zaidi kwenye Sekta gani muhimu?

Unadhani bajeti itagusa maisha yako kwa unafuu wa kodi, fursa mpya za ajira au maboresho katika huduma za kijamii?

Mjadala https://jamii.app/BajetiKuu26

#JamiiAfrica #JamiiForums #BajetiKuu26 #Governance
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Msemaji Mkuu wa Serikali na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa, amesema mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025 utafadhiliwa kwa Fedha za ndani

Amesema hayo Juni 11, 2025

Soma https://jamii.app/MsigwaUchaguzi2025

#JamiiForums #Democracy #Kuelekea2025 #JamiiAfrica #UchaguziMkuu2025
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mchambuzi na Mtangazaji, Edo Kumwembe kupitia Kipindi cha Jana na Leo cha Wasafi FM ameeleza hoja ya Mbunge wa Kinondoni, Abbas Tarimba kuwa Wabunge wapewe 'plate number' maalumu sio kipaumbele cha Watanzania huku akitoa mfano kuwa Viongozi wengi wa Nchi masikini wanapenda maisha ya kifahari

Tarimba akiwa Bungeni, jana Juni 11, 2025 alisema namba hizo zitawatambulisha barabarani kwenye misafara au kwenye shughuli zao za kila siku, ili wapishwe na wafike haraka katika misafara yao

Soma https://jamii.app/UchambuziWaEdo

Video credits: Wasafi FM

#Democracy #JamiiForums #Kuelekea2025
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Rais #WilliamRuto amesema Usalama wa Kenya ni Haki ya Wananchi, hivyo Wahalifu wote wawe Raia au Maafisa wa Usalama wa Taifa lazima wawajibishwe Kisheria

Kauli hiyo ni baada ya uchunguzi wa Mwili wa Mwanaharakati na Mwanamitandao Albert Ojwang' aliyedaiwa kufariki kwa kujigonga ukutani, kubaini kuwa aliteswa na kupigwa vibaya akiwa chini ya ulinzi wa Polisi

Aidha, Bunge liliahirisha shughuli zake kujadili suala hilo ambapo Waziri wa Mambo ya Ndani, IGP, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Jinai (DCI) waliitwa kujibu maswali kuhusu kesi hiyo, ambapo Taasisi ya Kusimamia Utendaji wa Polisi (IPOA) ilieleza Mifumo ya CCTV katika ofisi ya Mkuu wa Kituo Kikuu cha Polisi alipokuwa akishikiliwa Albert ilichezewa

Zaidi https://jamii.app/RutoUhalifu

Video Credits: BBC Swahili

#JamiiForums #JamiiAfrica #Accountability #HumanRights #Governance
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA-Bara, John Heche amesema Mtu aliyemuomba radhi katika ‘clip’ inayosambaa ni raia ambaye alifanya hivyo kwa niaba ya Mtoto wa dada yake ambaye alifanya vurugu wakati wa Mkutano wa chama hicho

Heche amesema “Huyu bwana alionesha ustaarabu wa hali ya juu kwa kukiri kosa la mtoto wa dada yake, anachofanya RPC ni kuficha madhaifu yao na kubadili ukweli wa mambo, hakuna sehemu yoyote katika mazungumzo hayo mtu huyo amejitambulisha kuwa ni Askari.”

Ikumbukwe, Kamanda wa Polisi Mkoa, Richard Abwao aliwaambia Wanahabari kuwa wamemkamata mtu huyo Daud Paul Delim (49), Mkazi wa Mbagala A, Wilayani Igunga ikielezwa alijifanya ni Mkuu wa Kituo cha Polisi

Soma https://jamii.app/HecheMkoaniTabora

#JamiiForums #Siasa #Kuelekea2025
Mdau wa JamiiForums.com kwenye Jukwaa la Habari na Hoja Mchanganyiko anasema tangazo la Serikali kuwa uchaguzi Mkuu utafadhiliwa kikamilifu kwa fedha za ndani ni habari njema kwa uhuru wetu wa kisiasa lakini je, hii inaweza kuathiri ugawaji wa rasilimali kwenye miradi ya maendeleo au huduma za kijamii?

Anaongeza kuelekea kusomwa kwa Bajeti Kuu kwa mwaka wa fedha 2025/26, tujiulize; Je, tumetenga fedha za kutosha kwa uchaguzi bila kukwamisha miradi mingine muhimu kama afya, elimu na miundombinu?

Mdau anaendelea kwa kuhoji ni mikakati gani mipya ya mapato inakuja kusaidia kuhakikisha tunafikia malengo yote bila kumuumiza Mwananchi wa kawaida?

Mjadala https://jamii.app/BajetiKuu26

#JamiiForums #BajetiKuu26 #Uchumi #JamiiAfrica #Uwajibikaji #Accountability #Demokrasia
Mshiriki wa Stories of Change 2022 alisema Viongozi wateule waache kuwapotezea muda Wananchi wanapotafuta Haki kwenye Migogoro ya Ardhi sababu wapo wanaohangaika Miaka miwili bila kupata Haki na endapo RC au DC akibadilishwa Mtu anaanza kuteseka upya badala ya kueleweshwa tangu mwanzo ili aende kwenye Mabaraza ya Ardhi

Soma zaidi https://jamii.app/WateuleMigogoroArdhi

#JamiiForums #JamiiAfrica #Accountability #Uwajibikaji #SOC2022