JamiiForums
55.4K subscribers
33.4K photos
2.03K videos
30.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imesema imebaini uwepo wa vitendo vya Ukiukwaji wa Sheria ya Vyama vya Siasa Sura 258 katika Mikutano ya Siasa, kwa baadhi ya Vyama kuruhusu Wanachama na mashabiki wake kutumia maneno ya Uongo, kashfa na uchochezi dhidi ya Chama kingine, Mtu binafsi, Taasisi au Serikali

Msajili amekiasa kila Chama cha Siasa chenye Usajili kamili, kuwaelimisha na kuwadhibiti Wanachama na Mashabiki wake, kuhakikisha hawakiuki Sheria za Nchi, hususani Sheria ya Vyama vya Siasa na Kanuni zake na inafuatilia mienendo ya Viongozi, Wanachama na Mashabiki wa Vyama vya Siasa

Soma https://jamii.app/MsajiliMaelekezo

#JamiiForums #Kuelekea2025 #UchaguziMkuu2025 #Siasa
DAR: Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limesema linaidai Klabu ya Yanga (kiasi cha Fedha hakijawekwa wazi) na si kweli kuwa Klabu hiyo inadai Fedha za ubingwa wa Kombe la Shirikisho la TFF ilizostahili kupata msimu uliopita

TFF imesema Yanga iliomba kwa barua Fedha zao za zawadi katika mashindano mbalimbali zikatwe kulipia malipo wanayotakiwa kulipa kwa TFF ikiwemo ada za wachezaji wa kigeni

TFF imesema imeandika barua kwenda #Yanga ikiitaka Klabu hiyo kumtuma Mtaalamu wao wa Fedha Juni 11, 2025 kuhakiki deni la Klabu hiyo akiwa na vielelezo vyote katika Ofisi za TFF

Wakati Yanga ikisema haitacheza fainali ya Michuano hiyo hadi ilipwe, TFF imeeleza Mdhamini Mkuu wa mashindano hayo, Benki ya CRDB ililipa Fedha zote za Kimkataba Tsh. 255,000,000

Soma https://jamii.app/TFFVsYanga

#JamiiForums #JamiiAfrica #JFSports #Michezo
Yanga imesema haijawahi kulipwa fedha yoyote ya Ubingwa wa Kombe la Shirikisho la TFF kwa Misimu mitatu mfululizo (2021/2022, 2022/2023 na 2023/24) na kwamba TFF imekuwa ikishikilia fedha hizo kwenye akaunti zao huku wakifahamu ni makosa na ni kinyume cha utaratibu

Yanga imeeleza “Hakuna uthibitisho wowote wa kimaandishi kuonyesha TFF wamewahi kulipa fedha hizo. Ni aibu, fedheha na kumtia dosari mdhamini kuendesha mashindano bila kumlipa Bingwa. Tunaelekeza, dawa ya deni ni kulipa kwa wakati ikiwa ni haki ya mshindi na inampa heshima mdhamini wa mashindano.”

Taarifa “leleweke, ada za malipo ya Wachezaji wa kigeni walizozisema kwenye taarifa yao hulipwa mwanzo wa msimu mpya na hela hizi za Ubingwa hutolewa Mwisho wa msimu. Yanga haijawahi kupokea taarifa yoyote rasmi kutoka TFF kuhusu Klabu yetu kuwa na deni kwao.”

Soma https://jamii.app/YangaMajibuJuni10

#JamiiForums #JFSports #JamiiAfrica
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Kada wa Chama cha ACT Wazalendo, Selemani Said Bungara (Bwege) amesema Chama cha Demokrasia na Maendeleo (#CHADEMA) kiko sahihi kudai Mabadiliko ya Mfumo wa Uchaguzi lakini ameonesha wasiwasi kama wataweza kushikilia msimamo wao huo kwa bila ruzuku kwa Miaka mitano ijayo

Akihojiwa na EATV, Bwege aliyewahi kuwa Mbunge wa Kilwa Kusini kwa Miaka 10 (2010- 2020) kupitia Chama cha Wananchi (CUF) kabla ya kuhamia #ACTWazalendo ameongoza kuwa #CHADEMA wakishikilia msimamo huo hadi Mwaka 2030 watakuwa Chama imara zaidi huku akidai ACT inasubiri huruma ya #CCM katika Uchaguzi

Soma https://jamii.app/BwegeKuhusuUchaguzi

#JamiiForums #Kuelekea2025 #Democracy #UchaguziMkuu2025
KENYA: Matokeo ya Uchunguzi wa Daktari yanapingana na ripoti ya Polisi iliyosema kuwa Mwanaharakati na Mwanamitandao, Albert Ojwang' alifariki kwa kujigonga Kichwa kwenye ukuta wa chumba cha Mahabusu katika Kituo Kikuu cha Polisi, alipokuwa akishikiliwa kwa tuhuma za kuchapisha maandiko yaliyolenga kumchafua Naibu Mkuu wa Polisi

Daktari wa Serikali, Bernard Midia, amesema kama Ojwang’ angejigonga ukutani, Damu ingetoka mbele ya Kichwa, lakini walikuta michubuko mbalimbali Kichwani, Usoni, pembeni na nyuma ya Kichwa, ikionesha kuwa majeraha hayo hakuweza kujisababishia mwenyewe

Midia, ambaye alifanya uchunguzi huo pamoja na mwakilishi wa Familia, Mutuma Zambezi, alikanusha uwezekano wa Ojwang' kujijeruhi. Alisema, "Tunapojumuisha pamoja na majeraha mengine yaliyosambaa sehemu mbalimbali za Mwili, ikiwemo Mikononi na Kiwiliwili, basi hii haiwezekani kuwa ni jeraha alilojifanyia mwenyewe

Soma https://jamii.app/PostmortemResults

#JamiiAfrica #JamiiForums #Accountability #HakiZaBinadamu
Nidhamu ni Msingi wa Mafanikio, kipaji pekee hakitoshi.

Ili kufikia ndoto zako, unahitaji nidhamu isiyoyumba. Nidhamu ndiyo inageuza uwezo wako kuwa matendo na hatimaye, mafanikio unayoyatamani

#JamiiForums #JamiiAfrica #AmkaNaJamiiAfrica #GoodMorning #Maisha
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (#CHADEMA) kimetoa tamko kuwa kuna hali ya hatari inayojitokeza kwa kasi dhidi ya Vyama vya Siasa vinavyopigania mabadiliko ya kweli nchini

Chama hicho kimedai kuna juhudi za kurejea kwa enzi za Utawala wa Kiimla unaotumia Vyombo vya Dola na Mahakama kama zana za kukandamiza sauti mbadala, badala ya kulinda haki za Wananchi na Utawala wa Sheria

CHADEMA imetoa wito kwa Viongozi, Wanachama, Wafuasi wake na wote wanaoamini katika misingi ya uhuru, haki, na demokrasia, kuwa tayari kupokea maelekezo kutoka kwa Viongozi Wakuu wa Chama na kuwa hawatarudi nyuma katika kudai Tanzania yenye Mfumo wa Haki, Uhuru na Utawala wa Sheria.

Soma https://jamii.app/TamkoLaCHADEMA

#JamiiForums #Siasa #Democracy
Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma imeendelea kusikiliza hoja za rufaa kupinga kifungo cha Maisha jela walichohukumiwa aliyekuwa askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Clinton Damas, maarufu Nyundo na wenzake Amin Lema, Nickson Jackson na aliyekuwa Askari Magereza, Praygod Mushi, huku upande wa Jamhuri ukiomba kuzijibu Juni 12, 2025

Akiwasilisha hoja Mahakamani, Juni 10, 2025, Wakili wa Warufani hao, Godfrey Wasonga amedai kulikuwa na dosari za Kisheria katika kesi hiyo kuanzia hati ya mashtaka hadi hukumu. Amedai Mahakama ilioneshwa vipande Vinne vya Video ambavyo ni 6, 7, 8 na 9 lakini kwenye hukumu, vipande vya Video vilivyowatia hatiani ni namba 1, 2, 3 na 4 ambavyo havikuoneshwa Mahakamani hapo

Aidha, kwa mujibu wa Wakili huyo, vipande vya Video vilivyooneshwa viliwaonesha washtakiwa wakijirekodi wakiwa wanacheza Muziki, huku wakiwa na chupa za Vinywaji lakini hazikuonesha wakiwa wanatenda kosa la kubaka kwa kikundi wala kulawiti

Soma https://jamii.app/UpdatesKesiYaNyundo
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Musukuma, ameibua hoja #Bungeni leo Juni 11, 2025 akidai kuwepo kwa Mazingira yasiyo rafiki kwa Viongozi na Familia zao wanapopita maeneo ya VIP katika Viwanja vya Ndege

Soma https://jamii.app/MusukumaJuni11

#JamiiAfrica #Siasa #Govevernance #JamiiForums
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
#BUNGENI: Leo Juni 11, 2025, Mbunge wa Kinondoni Abbas Tarimba amependekeza wabunge wapewe 'plate number' maalumu zitakazowatambulisha Barabarani kwenye misafara au kwenye shughuli zao za kila siku

Zaidi https://jamii.app/WabungeSpecialPlateNumbers

#JamiiForums #JamiiAfrica #Accountability #Uwajibikaji #Kuelekea2025 #Governance
Aliyekuwa Jaji Mkuu wa Kenya, Dkt. Willy Mutunga, Wakili Mwandamizi Martha Karua, pamoja na watu wengine wanne wamefungua kesi katika Mahakama ya Haki ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EACJ) dhidi ya Serikali ya Tanzania, wakidai kuwekwa kizuizini kinyume cha Sheria, kunyimwa kuingia nchini na kufukuzwa kati ya Mei 18 hadi 19, 2025, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam

Kundi hilo ambalo pia linajumuisha Wanaharakati na Watetezi wa Haki za Binadamu wanne ambao ni Gloria Kimani, Lynn Ngugi, Hussein Khalid na Hanifa Adan wamedai kuwa haki zao kama raia wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zilikiukwa waziwazi walipozuiwa kuingia Tanzania kushuhudia kesi ya uhaini dhidi ya Kiongozi wa Upinzani, Tundu Lissu

Aidha, Kesi hiyo inatarajiwa kuhamishiwa Makao Makuu ya EAC - Arusha ambako tarehe ya kusikilizwa itapangwa na Mahakama hivi karibuni

Soma https://jamii.app/KenyaKuiburuzaTZ

#JamiiForums #JamiiAfrica #Diplomasia