JamiiForums
55.4K subscribers
33.4K photos
2.03K videos
30.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Unampa Ushauri gani Kijana aliyekuja Dar kutafuta Maisha?

Mjadala zaidi https://jamii.app/KijanaUkijaDar

#JamiiAfrica #JamiiForums #Maisha #JFStories #JFChitChats
Akizungumza na Mwananchi Communications Ltd kuhusu wimbi kubwa la watumiaji wa Mitandao ya Kijamii 'ku-comment' No reforms, No Election, Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, amesema "Watu wajiepushe na kampeni zisizokuwa na tija, watumie Mitandao kama fursa ya kujifunza Teknolojia mpya, wanapaswa kutambua na kujua kutumia Mitandao vibaya ni kupoteza Rasilimali Fedha kwa kuwa wanatumia bando"

Katika maelezo yake Msigwa amesema "Kinachoendelea kwenye Mitandao ni upuuzi. Huu ni upuuzi unaoendelea, Watanzania wajielekeze kujenga Nchi yao. Huwezi kuendesha Kampeni ya kuzuia Uchaguzi wakati Nchi imejiwekea kalenda yake."

Soma https://jamii.app/MsigwaUpuuziNRNE

#JamiiAfrica #JamiiForums #HumanRights #HakiZaKidijitali #DigitalRights
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Sheikh wa Mkoa wa Simiyu, Issa Kwezi amesema “Watanzania mara zote tumesimama katika maadili ya kuheshimiana, mdogo anamuheshimu mkubwa na yule asiyekuwa na cheo ambapo yeye anaongozwa anamuheshimu yule ambaye anamuongoza, na hizo ndio tamaduni zetu, lakini leo tunaona mpaka watu wazima wamepoteza maadili kwa kisingizio tu cha demokrasia"

Ameyasema hayo Juni 7, 2025 wakati akitoa Mawaidha kwenye Swala ya Eid Adh-ha Mkoani humo

Soma https://jamii.app/TusiwakosoeViongoziHadharani

#JamiiForums #JamiiAfrica #Governance
Kwenye maisha, kuna wakati utajisikia kuchoka iwe ni kutokana na kazi, ndoto zako au changamoto unazopitia. Kuchoka hakumaanishi kwamba umefeli au unapaswa kuacha

Badala ya kurudi nyuma au kuachana na safari yako, jipe muda wa kupumzika, kutulia, kujikusanya tena na kuendelea mbele ukiwa na nguvu mpya

#JamiiForums #JamiiAfrica #GoodMorning #AmkaNaJF #Weekend
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Mhashamu Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Mwanza, Renatus Nkwande amesimulia tukio la gari lake kufuatiliwa na 'Watu ambao hakuwatambua', na kuongeza hali hiyo inatia hofu kwa kuwa wakati huu kuna taarifa zinazoripotiwa kuhusu matukio ya utekaji

Ameyasema hayo Juni 3, 2025 katika Msiba wa Mzee Mongela, mbele ya Viongozi mbalimbali wa Nchi akiwemo Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa na Spika wa Bunge

Soma https://jamii.app/AskofuAnusurikaKutekwa

#JamiiForums #JamiiAfrica #HumanRights #Governance
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Baadhi Waumini wa Kanisa la Glory of Christ Tanzania (Kanisa la Ufufuo na Uzima) linaloongozwa na Askofu Josephat Gwajima ambalo Juni 2, 2025 lilifungiwa na Serikali, wamejitokeza eneo la pembezoni mwa Kanisa hilo lililopo Ubungo wakisali na kuimba nyimbo mbalimbali za Dini

Wakati hayo yakiendelea Kanisa limezungukwa na Askari Polisi ambao wapo tangu siku Serikali ilipotangaza kulifungia Kanisa hilo kwa kutoa huduma kwa kile kilichoelezwa kutoa matamshi ya Kisiasa yenye lengo la kuichonganisha Serikali na Wananchi

Awali, jana Juni 7, 2025, Katibu Mkuu wa Kanisa hilo, Dkt. Erick Shoo alitangaza kutokuwa na ibada katika matawi yao yote Nchini, badala yake ibada zifanyike nyumbani hadi watakapopewa taarifa zaidi

Soma https://jamii.app/WaumiziWaGwajima

#JamiiAfrica #JamiiForums #JFMatukio
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Mchungaji wa Kanisa la Waadventista wa Sabato Kinyerezi, Maotola John Lumbe amesema “Nitoe ushauri wa bure kwa Viongozi, Kiongozi yoyote usipopata mawazo kinzani, unaogopwa na haufanyi vizuri. Kiongozi ruhusu mawazo mbadala yaje, sasa hapa wale wanaojiita chawa hawatakuja kwako maana unaruhusu 'discussion'. Kiongozi lazima ukubali kukosolewa na uwe na uwezo mkubwa wa kuvumilia, kustahimili, kunyamaza kimya na kuongea kidogo"

Ameyasema hayo katika Ibada ya Sabato iliyofanyika Kanisa la Waadvintista Wasabato SDA Kinyerezi Juni 7, 2025

Soma https://jamii.app/KiongoziUweMvumilivu

#JamiiForums #JamiiAfrica #HumanRights #Governance
Kusoma kwa undani habari hizi na nyingine zilizojiri juma lililopita bofya https://jamii.app/YaliyojiriJumaLililopita

#JamiiForums #JamiiAfrica #YaliyojiriJumaLililopita #JFToons
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Askofu Mkuu, Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam, Yuda Thadeus Ruwaichi amesema kwa yanayoendelea Tanzania kwasasa hatupaswi kujiita Kisiwa cha Amani

Amesema “Tupende kushughulikia mambo yetu kwa msingi wa ukweli zaidi, msingi wa haki, msingi wa amani na msingi unaompendeza Mungu. Kusudi tuweze kweli kudai kwamba sisi ni kisiwa cha amani, katika yale yanayoendelea zama hizi katika nchi yetu, nashauri tusithubutu kujiita kuwa ni kisiwa cha amani. Tusithubutu kujitanabaisha kama kisiwa cha amani”

Zaidi https://jamii.app/KisiwaChaAmani

#JamiiForums #JamiiAfrica #SocialJustice #Governance #HumanRights #Accountability
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion, Alex Msama akizungumza na Wanahabari Juni 8, 2025 amesema wote wanaomsema vibaya Rais Samia Suluhu ni sawa na kuwa wanamsema Mungu ambaye ndiye aliyempa Mamlaka aliyonayo

Soma https://jamii.app/AlexMsamaSiasa

Video Credits: Torch Media

#JamiiForums #Siasa #Kuelekea2025 #Democracy #UchaguziMkuu
DAR: Wakati Uongozi wa #Yanga ukitarajiwa kufanya kikao na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania, leo Juni 9, 2025 kuhusu ajenda ya mchezo dhidi ya #Simba uliopangwa kuchezwa Juni 15, 2025, Klabu hiyo imesema matakwa yao yakisililizwa na kutekelezwa, timu itaingia uwanjani

Akijibu swali kupitia Wasafi FM, Afisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe amesema “Yanga ni Klabu ya Mpira wa Miguu, kazi kubwa ni kucheza Mpira wa Miguu, matakwa ya Kamati ya Utendaji ya Yanga yaliyowasilishwa kwa Bodi ya Ligi yakisikilizwa na yakafanyiwa kazi bila shaka yoyote mbungi itapigwa.”

Mchezo huo ulipangwa kuchezwa Machi 8, 2025 lakini uliahirishwa baada ya Simba kuzuiwa kufanya mazoezi kwenye Uwanja wa Mkapa siku moja kabla, Yanga ilipeleka timu uwanjani na kueleza haipo tayari kucheza mchezo huo Namba 184 wakati mwingine kwa madai maamuzi ya kutochezwa yalikuwa kinyume na utaratibu wa Kanuni za Ligi

Soma https://jamii.app/KamweYanga

#JFSports #JFLigiKuu25 #JamiiForums #KariakooDerby
Mdau wa JamiiForums.com ameshauri tuache kulalamika pale ambapo marafiki wakitutenga au wakibadilika kwani kuna sababu zinazofanya marafiki kuja na kuondoka katika maisha

Unakubaliana na hoja ya Mdau?

Mjadala zaidi https://jamii.app/UsiogopeKupotezaMarafiki

#JamiiForums #JamiiAfrica #Lifestyle #Lifelessons
SINGIDA: Mdau wa JamiiForums.com anadai Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama wanaoomba uhamisho wamekuwa wakikutana na usumbufu kutoka kwa Maafisa wanaohusika kupokea taarifa kutoka Makao Makuu ya UTUMISHI au TAMISEMI

Anadai hadi Mamlaka ya juu inakubali uhamisho ni kwamba umejiridhisha na sababu zilizotolewa lakini Maafisa wa Halmashauri hiyo wanawakwaza wengi kwa kukwamisha au kuchelewesha taratibu za uhamisho

Anaeleza kuwa Serikali ilipotambulisha uhamisho wa Kidigitali walitegemea utaboresha lakini hali imekuwa ngumu, hivyo anatoa wito kwa Katibu Mkuu UTUMISHI na Katibu Mkuu TAMISEMI na Waziri wa UTUMISHI kufuatilia kero hiyo ambayo imekuwa kikwazo kwa wengi na inashusha thamani ya Utumishi wa Umma

Soma https://jamii.app/SingidaUtumishi

#JamiiForums #Accountability #JFHuduma
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
RUVUMA: Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (#CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira amesema Chama chao hakina mpango wa kuahirisha Uchaguzi kama ambavyo “Wale wa Tonetone” wanavyopita na kutangaza kutoshiriki katika Uchaguzi Mkuu wa 2025

Amesema hayo alipokuwa katika Ofisi za CCM Mkoa, leo Juni 9, 2025 ikiwa ni Siku ya kwanza ya ziara yake Mkoani humo

Soma https://jamii.app/WasiraUchaguzi

#Siasa #JamiiForums #Kuelekea2025 #UchaguziMkuu2025 #Democracy
Wizara ya Mambo ya Nje ya Rwanda imelalamikia uamuzi wa kutokabidhiwa uenyekiti wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika ya Kati (ECCAS), ambapo katika tamko lake imesema haina sababu ya kuendelea kuwa Mwanachama wa Jumuiya ambayo haitii misingi, uamuzi ambao bado haujawa wazi utachukuliwa lini

Aidha, Ofisi ya Rais wa DRC, Félix Tshisekedi, ikiongelea Uamuzi wa Rwanda kutokabidhiwa uongozi wa Jumuiya hiyo imesema Wanachama wa ECCAS wametambua “uchokozi wa Rwanda dhidi ya Congo” na kuitaka Rwanda kuondoa Wanajeshi wake kutoka ardhi ya Congo mara moja

Mvutano kati ya Rwanda na DRC umechochewa na tuhuma za uhusiano wa karibu wa Rwanda na Waasi wa M23 wanaopigana Mashariki mwa Congo, uhusiano ambao mara kadhaa Rwanda imeukana

Zaidi https://jamii.app/RwandaKujitoa

#JamiiForums #JamiiAfrica #Diplomacy