JamiiForums
55.7K subscribers
33.2K photos
1.97K videos
30.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
#UWAJIBIKAJI: Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Tumaini Nagu, amepiga marufuku Watumishi wa Afya kutumia Simu na kufanya mazungumzo binafsi wakati wakiwa kazini

Mganga Mkuu amechukua hatua hiyo wakati kukiwa na ongezeko la malalamiko ya Wananchi juu ya kusuasua kwa huduma katika Vituo vya Afya ikielezwa Watoa Huduma wanatumia muda mwingi kuchezea Simu na kupuuza Majukumu yao

Profesa Nagu amewataka Watumishi wa Afya kuzingatia majukumu yao ya Kitaalamu wakati wote wa kazi ili kuhakikisha wanatoa huduma bora na zenye ufanisi kwa wananchi.

Soma https://jamii.app/SimuKazini

#JamiiForums #Governance #JFHuduma #PublicHealth #Accountability #ServiceDelivery
Siku chache baada ya Mdau wa JamiiForums.com kulalamikia hali mbaya ya Soko la Mahakama ya Ndizi maarufu kama Soko la Mabibo, Halmashauri ya Ubungo imetangaza kuanza ukarabati ikiwa ni pamoja na kujenga Vizimba vya Wauzaji Bidhaa

Akitoa taarifa hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Hashim Komba amesema jumla ya Tsh. Milioni 600 zimetengwa kwaajili ya ukarabati utakaohusisha Barabara za kuingia Sokoni na Vyoo vya Soko

Soko hilo ambalo huuza Bidhaa za Vyakula limekuwa na changamoto kubwa ya kujaa Maji ya Mvua ambayo hukusanyika na kuunda Tope na hivyo kuwalazimu Wafanyabiashara na Wanunuzi kukodi Buti ili kuingia ndani ya Soko

Soma https://jamii.app/MabiboMdau

#JamiiForums #Governance #Accountability #PublicHealth #JFSC
Vipi Mdau ni Chakula gani ukitengewa Ugenini unaweza kulala njaa?

Mjadala zaidi https://jamii.app/VyakulaVyaUgenini

#JamiiForums #Maisha #JFChitChats #Vyakula #Asili
#ZANZIBAR: Mwanachama wa zamani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mohamed Shamte amedai suala la kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale, Simai Mohamed Said lina kitu ambacho hakiwekwi wazi juu ya uamuzi huo

Shamte ambaye alifukuzwa uanachama wa #CCM Mwaka 2022 kwa kilichoelezwa kuwa ni kutomheshimu Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi, amesema kama kitu hicho kitaendelea kufichwa, kuna Mawaziri wengine watajiuzulu

Ikumbukwe, Januari 24, 2024 Simai aliilalamikia Bodi ya Vileo kubadilisha Mawakala wa kuingiza Vinywaji Zanzibar. Januari 26, 2024, Simai aliamua kuachia nafasi yake akidai Mazingira ya kazi si rafiki kwake.

Soma https://jamii.app/ShamteSimai

#JamiiForums #Governance #JFDemokrasia #Siasa #Accountability
MAREKANI: Mahakama imeagiza Rais wa zamani, #DonaldTrump kumlipa fidia ya zaidi ya Tsh. Bilioni 211, Mwanamke aliyetambulika kama E Jean Carroll ambaye alimshtaki Trump kwa madai ya kumnyanyasa Kingono Mwaka 1990

Kwa mujibu wa uamuzi wa Mahakama, Mgombea Urais huyo wa #Republican atalazimika kulipa Tsh. Bilioni 18.5 kama fidia ya udhalilishaji na Tsh. Bilioni 27.9 kama fidia ya kuharibu Heshima ya Mtu mwingine na Tsh. Bilioni 165.4 kama adhabu

Hata hivyo, #Trump amesema hajaridhishwa na uamuzi wa Mahakama na atakaka rufaa huku akimtuhumu Rais #JoeBiden kutoa maelekezo kwa Mahakama ili kumharibia sifa kuelekea Uchaguzi Mkuu utakafanyika mwishoni mwa Mwaka 2024

Soma https://jamii.app/TrumpEJ

#JamiiForums #Governance #WomenRights #SocialJustice #JFMatukio
KENYA: Mahakama ya Juu imezuia Serikali kupeleka Askari Polisi Nchini #Haiti, ikieleza Baraza la Usalama la Kitaifa halina Mamlaka ya Kisheria ya kutuma Polisi nje ya #Kenya bali linaweza kupeleka Wanajeshi kulinda Amani

Serikali ya Kenya imesema itakata rufaa dhidi ya uamuzi huo

Mwaka 2023, Waziri Mkuu wa Haiti, Ariel Henry aliomba Umoja wa Mataifa (#UN) kupeleka kikosi cha Kimataifa akidai Serikali yake imezidiwa nguvu na magenge yanayodhibiti 80% ya Mji Mkuu wa Port-au-Prince

Soma https://jamii.app/KenyaHaiti

#Diplomacy #Governance #JamiiForums
#ZANZIBAR: Rais Hussein A. Mwinyi amefanya Mabadiliko ya Baraza la Mapinduzi na kumteua Mudrick R. Soraga kuwa Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale akichukua nafasi ya Simai Mohamed Said aliyejiuzulu

Waliohamishwa Wizara ni Ali S. Ameir aliyeteuliwa kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - Ikulu na Shaaban A. Othman anayekuwa Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi

Mwingine ni Juma M. Juma anayekuwa Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - Fedha na Mipango akitoka Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi

Wateule wapya ni Salha M. Mwinjuma aliyeteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi pamoja na Zawadi A. Nassor anayekuwa Naibu Waziri wa Maji, Nishati na Madini

Soma https://jamii.app/ZNZCabinet

#JamiiForums #Governance #Accountability
Umewahi kukutana na changamoto ya kunyanyasika kwasababu ulitafutiwa Kazi na Mtu, uliwezaje kukabiliana na hali hiyo?

Shiriki mjadala zaidi https://jamii.app/MdauKazi

#JamiiForums #Maisha #JFStories
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Fahamu kuhusu Kidaka Tonge pamoja na umuhimu wake katika Afya ya Mwili

#Afya #JamiiForums #PublicHealth
#TaarifaPotofu zinazohusu #Afya huwafanya Watu wachukue hatua zisizo Sahihi kama vile kutokutii Miongozo ya kuzuia Magonjwa, kukataa Chanjo au hata kutumia Tiba zisizo sahihi

Mathalani, Kwa mujibu wa taasisi ya Global Polio Eradication Initiative, #Pakistan na #Afghanistan ni Nchi mbili pekee Duniani zinazosalia kuwa na Ugonjwa wa #Polio kutokana na uwepo wa Upotoshaji Mkubwa wa Taarifa za Chanjo zake hivyo kukwamisha Juhudi za Dunia katika kuutokomeza Ugonjwa huu

Taarifa Potofu huongeza Mzigo wa Magonjwa kwenye Jamii, ni Muhimu kuhakikisha Unapata taarifa Sahihi kutoka Vyanzo vya Kuaminika kabla ya Kuziamini au Kusambaza

Soma https://shorturl.at/dhwMX

#JamiiForums #JamiiCheck #Disinformation #Misinformation #VisitJamiiCheck #FactsChecking
Mdau anaeleza Miaka ya nyuma Wadau wa Filamu walilalamika kukosekana kwa Wawekezaji katika Tasnia yao, na kusababisha Kazi zao kutokuwa na ubora lakini licha ya kuanza kupatikana kwa Uwekezaji mzuri bado ubora wa Maudhui ni wa viwango vya chini

Anadai uigizaji wa Wasanii wa Tanzania hasa katika Tamthilia zinazorushwa kwenye Runinga hauna tofauti na uigizaji wa ngazi ya Sekondari na hata Maadili ya Ujumbe mwingi wa kazi hizo ni ngumu kuangalia na Watoto

Je, una Mtazamo gani kuhusu Ujumbe wa kwenye Tamthilia za Kitanzania?

Soma https://jamii.app/MaoniTamthilia

#Maadili #Maisha #Malezi #LifeStyle #JamiiForums
KENYA: Idadi kubwa ya Wanawake wameandamana katika Miji 11 wakipinga kuongezeka kwa Vitendo vya Ukatili Dhidi yao yakiwemo Mauaji mfululizo yaliyoripotiwa kati ya Desemba 2023 hadi Januari 2024

Maandamano yalitawaliwa na Mabango yenye jumbe mbalimbali za kukemea Ukatili kama "Sisi ni Watu si Wanyama" na mengine yakiwataja baadhi ya Wanawake waliouawa

Kwa mujibu wa Ripoti ya Shirika la Amnesty International inakadiriwa zaidi ya Wanawake 500 waliuawa kati ya Mwaka 2016 hadi 2023. Aidha utafiti wa Serikali wa Mwaka 2022 ulibaini Mwanamke mmoja katika kila Watatu amepitia Ukatili wa Kijinsia katika Maisha yake.

Soma https://jamii.app/MauajiKE

#JamiiForums #SocialJustice #HumanRights #WomenRights #EndGBV
Mchezaji huyu amefanikiwa kufunga Magoli katika Mechi zinazohusisha upinzani wa jadi wa Timu za Mji mmoja ‘Dabi’ na katika ushindani wa Timu kubwa zenye upinzani kutoka Miji tofauti Nchini #England na Hispania

Amefunga katika Mechi ya #Liverpool vs Everton, #Barcelona vs Real Madrid na Manchester City vs Manchester United

Je, Mchezaji huyu ni nani?

Soma https://jamii.app/SokaSwali

#JFSports #JFChemshaBongo #JFBrainTeaser #JamiiForums
JIUNGE NA 'CHANNEL' YA TELEGRAM YA JAMIICHECK UWE WA KWANZA KUPATA TAARIFA ZILIZOHAKIKIWA

JamiiForums kupitia Jukwaa lake la #JamiiCheck inaendelea kukupa nafasi ya Kuhabarika, Kuelimika na Kushiriki mchakato wa Kuhakiki Taarifa kila wakati na kwa haraka zaidi, ambapo hivi sasa imekuongezea sehemu nyingine ya kupata taarifa hizo kupitia Mtandao wa #Telegram

Jiunge sasa na 'Channel' yetu ya Telegram kwa kubofya hapa https://t.me/JamiiCheck

#JamiiForums #HakikiTaarifa #Misinformation #Disinformation #FactsChecking #VisitJamiiCheck
Kocha wa FC Barcelona, Xavi Hernández amesema ataondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu kutokana na matokeo mabaya ya timu hiyo aliyoanza kuinoa Novemba 2021

Ametangaza uamuzi huo baada ya Barcelona kupigika magoli 5-3 kutoka kwa Villarreal, hivyo kuzidiwa pointi 10 na vinara wa Ligi Kuu ya Uhispania (LaLiga), #RealMadrid

Xavi ,44, ambaye alishinda mataji 25 akiwa mchezaji wa Barcelona atajiuzulu rasmi Juni 30, 2024 licha ya kuwa amesaliwa na mwaka mmoja zaidi katika mkataba wake, ameweka wazi kuwa anaamini klabu hiyo inahitaji mbadiliko, akidai kwa sasa wamekuwa wakicheza wakiwa na presha kubwa

Soma https://jamii.app/Xavi

#JFSports #JamiiForums