JamiiForums
54K subscribers
34.1K photos
2.26K videos
31K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
UPINZANI VENEZUELA WAKAMATA KITUO CHA MAFUTA

> Upinzani unaolidhibiti Bunge la Venezuela umeteuwa bodi ya mpito ya kampuni ya mafuta ya Serikali (PDVSA), ikiwa ni jitihada za kiongozi, Juan Guaido kuidhibiti sekta ya uchimbaji wa mafuta

Soma - https://jamii.app/GuaidoSeizeOilProduction
NIGERIA: WATU 7 WAFARIKI DUNIA KWENYE KAMPENI ZA RAIS BUHARI

> Wengine 12 wamejeruhiwa baada ya umati wa Watu kukanyagana wakati wakitoka kwenye uwanja uliofanyika kampeni za Rais Muhammadu Buhari

> 8 bado wamelazwa Hospitali

Zaidi, soma => https://jamii.app/VifoMkutanoBuhari
AFYA: SIDIRIA INAYOWEZA KUGUNDUA SARATANI YA MATITI YAVUMBULIWA

> Sidiria hiyo inaweza kupima viwango vya joto, kuviweka katika programu na kisha kutoa taarifa

> Wanawake wanaohitaji watalazimika kuivaa kwa dakika 60 hadi 90 kwa wiki

Soma > https://jamii.app/SidiriaSaratani
BUSEGA, SIMIYU: WANANCHI WAPIGA KURA YA SIRI ILI KUWATAJA WAUAJI WA WATOTO

> Zoezi hilo limeendeshwa leo kwenye Kata ya Lamadi ambapo kura hiyo imelenga kuwataja watuhumiwa wa mauaji ya Watoto wilayani humo

Zaidi, soma => https://jamii.app/KuraWauajiSimiyu
MFANYAKAZI WA TAZARA AKAMATWA NA TAKUKURU KWA TUHUMA ZA RUSHWA

> Bahati Selemani amekamatwa na TAKUKURU, Mbeya kwa tuhuma za kupokea rushwa ya Shilingi laki 2 kutoka kwa Mfugaji aliyemkamata akilisha mifugo kwenye hifadhi ya reli

Soma > https://jamii.app/TAKUKURUVsAfisaTAZARA
CHINA YAIPATIA BURUNDI IKULU MPYA

> Balozi wa China nchini Burundi, na Waziri wa mambo ya nje wa Burundi, wamesaini hati ya makabidhiano ya jengo la Ikulu ya Burundi lililojengwa kwa msaada wa China

> Ipo eneo la Mutimbuzi, Bujumbura

Soma - https://jamii.app/BurundiNewWhiteHouse
TRUMP KUSAINI MUSWADA WA KUGHARAMIA MATUMIZI YA SERIKALI

> Muswada huo utazuia kufungwa tena kwa Serikali Kuu na kuwapa ahueni wafanyakazi takribani 800,000 waliopata kadhia ya kutolipwa mishahara mwezi Desemba

> Aahidi kutangaza hali ya dharura ili kupata pesa za kujenga ukuta

Zaidi, soma https://jamii.app/USFundingBill
KUELEKEA UCHAGUZI MKUU NIGERIA: MAGUNIA 17 YA KURA ZILIZOPIGWA YAKAMATWA

> Magunia hayo yamekamatwa kwenye Jimbo la Kano na inadaiwa kura zake zimepigwa ili kukipa ushindi chama tawala cha All Progressive Party (APC)

Zaidi, soma => https://jamii.app/NigeriaBallotsScandal
WANASAYANSI ITALIA WATENGENEZA CHANJO YA UKIMWI

> Wanasayansi kutoka nchini Italia wamegundua chanjo dhidi ya ugonjwa wa UKIMWI ambayo imefanikiwa kupunguza idadi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa huo mwilini kwa asilimia 90

Fahamu zaidi, soma - https://jamii.app/UtafitiChanjoUKIMWI
ZANZIBAR: MWANAUME AMJERUHI MKE WAKE USONI, BAADA YA KUKATAA KUTOA PENZI KINYUME NA MAUMBILE

> Amesema Mume wake alianza kumuomba penzi kinyume na maumbile miezi 3 baada ya ndoa

> Baada ya kukataa Mume wake alianza kumwambia hajui mapenzi

Soma > https://jamii.app/AjeruhiwaMapenziZNZ
AIRBUS KUSITISHA UZALISHAJI WA NDEGE AINA YA A380

> Shirika la Airbus limetangaza kusitisha uzalishaji wa ndege zake aina ya A380 Superjumbo ifikapo 2021 kutokana na kukosekana kwa soko

> Mteja mkuu alikuwa ni Shirika la ndege la Emirates

Soma - https://jamii.app/AirbusSeizeA380
TRUMP KUSAINI MUSWADA WA KUGHARAMIA MATUMIZI YA SERIKALI

> Muswada huo utazuia kufungwa tena kwa Serikali Kuu na kuwapa ahueni wafanyakazi takribani 800,000 waliopata kadhia ya kutolipwa mishahara mwezi Desemba

> Aahidi kutangaza hali ya dharura ili kupata pesa za kujenga ukuta

Soma - https://jamii.app/USFundingBill
KENYA: AFISA WA POLISI AHUKUMIWA KIFO KWA KUMUUA MAHABUSU

> Mahakama Kuu imempa adhabu ya kifo Afisa Mwandamizi wa Jeshi la Polisi, Nahashon Mutua kwa kosa la kumuua Mahabusu

> Mutua alimpiga na nondo Martin Koome hadi kufa mwaka 2013

Soma - https://jamii.app/AfisaPolisiAhukumiwaKifoKE
RAIA 13 WA ETHIOPIA WAKAMATWA MWANZA

> Jeshi la Polisi mkoani Mwanza linawashikilia raia 13 wa Ethiopia baada ya kukutwa wakiwa wamejificha kwenye shamba la mkazi mmoja wa mtaa wa Nyaburogoya Kata ya Nyegezi

> Walikamatwa Februari 13

Soma - https://jamii.app/WahamiajiEthiopiaWakamatwa
KENYA: MAAFISA WATANO WA POLISI WAKUTWA NA HATIA YA KUMUUA MTOTO

> Maafisa 5 wa Jeshi la Polisi, wamekutwa na hatia ktk kesi ya kumpiga na kitu kizito kichwani mtoto mwenye umri wa miezi 6, Samantha Pendo mwaka 2017 na kumsababishia kifo

Soma - https://jamii.app/Maafisa5HatianiMauajiMtoto
KAMPALA, UGANDA: WANAWAKE WAWILI WAFANYAKAZI WA BENKI WABAKWA NA MAJAMBAZI

> Wanawake hao ni wafanyakazi wa Benki ya Development Finance Company of Uganda(DFCU). Wamebakwa na majambazi waliojaribu kupora fedha katika benki hiyo

Soma > https://jamii.app/KampalaBankRobbery
SHINYANGA: WATU 2 WAFARIKI DUNIA BAADA YA KUANGUKIA KWENYE SHIMO LA MACHIMBO YA KOKOTO

> Shimo hilo limejaa maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha kwenye kijiji cha Kadoto huko Mwalukwa

Zaidi, soma => https://jamii.app/WafarikiShimoKokoto
SLOVENIA: MBUNGE AJIUZULU BAADA YA KUIBA MKATE

> Mbunge Krajcic wa Slovenia amejiuzulu baada ya kuiba mkate maarufu ''sandwich'' katika duka moja kwa madai kuwa wahudumu wa sehemu hiyo walimpuuzia

> Ameomba msamaha na kujutia kufanya hivyo

Soma - https://jamii.app/PmResignsStealingSandwich
AFARIKI KWA KUCHOMWA KISU NA MKEWE

> Mkazi wa Kijiji cha Lugalawa, Wilaya ya Ludewa-Njombe, Osmund Joseph Mwinuka(37) amefariki baada ya kuchomwa Kisu tumboni na mke wake kwa wivu wa Mapenzi

> Kamanda wa Polisi amethibitisha taarifa hiyo

Soma - https://jamii.app/MkeAuaMumeLudewa
KONDOMU ZADAIWA KUADIMIKA WILAYANI MAFINGA

> Kondomu za kike na kiume zimeonekana kupungua mjini hapo huku zilizopo zikielezwa kupanda bei na kuuzwa ghali kuanzia shilingi 1,000 mpaka 3,000

Soma - https://jamii.app/UhabaKondomuMafinga
SERIKALI KURUDISHA KODI KWENYE TAULO ZA KIKE KAMA HAZITASHUKA BEI

> Hii ni kutokana na wauzaji na wasambazaji wa taulo hizo kushindwa kupunguza bei licha ya kodi kuondolewa

> Waziri wa Fedha na wa Viwanda watakiwa kuanza kusimamia

Soma > https://jamii.app/BeiTauloKike