JamiiForums
βœ”
52.9K subscribers
34.3K photos
2.43K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
AFRIKA KUSINI KUHARIBU DOZI 100,000 ZA CHANJO YA PFIZER

Afrika Kusini imerekodi idadi kubwa ya Maambukizi na vifo vya #CoronaVirus katika Bara la Afrika, hata hivyo utoaji Chanjo umepungua huku Nchi ikiwa na akiba ya kutosha ya dozi milioni 25

Soma - https://jamii.app/ExpireVaccineSA
MABEYO AWASAMEHE WALIOFUKUZWA JKT, WARUDISHWA JESHINI

Mkuu wa Majeshi, Jenerali Venance Mabeyo ametoa msamaha kwa Vijana 853 waliofukuzwa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Aprili Mwaka 2021

Wanatakiwa kupokelewa kambini Machi 12, 2022

Soma - https://jamii.app/JKTMabeyo

#JFLeo
JESHI LA URUSI KUWAPOKEA WANAFUNZI WA KITANZANIA WALIO UKRAINE

Wanafunzi hao wanatakiwa kuelekea eneo la Sudja, watapokelewa na kusafirishwa hadi Belgorod, hapo watakabidhiwa kwa Maafisa wa Ubalozi wa Tanzania Nchini Urusi kwa taratibu za kurejeshwa

Soma https://jamii.app/RussiaTZ
CANADA YAWATAKA RAIA WAKE KUONDOKA URUSI

Serikali ya #Canada imesema hali ya Usalama haitabiriki na inaweza kuwa mbaya ghafla

IMF imeonya kuwa athari za kiuchumi za vita kati ya #Ukraine na Urusi zitakuwa mbaya zaidi ikiwa mzozo huo utaendelea

Soma - https://jamii.app/RaiaCanada
SERIKALI MPYA YAPITISHWA NCHINI BURKINA FASO

Rais wa Mpito ameidhinisha Serikali mpya yenye Mawaziri 25. Miongoni mwao ni Barthelemy Simpore aliyehudumu kama Waziri wa Ulinzi chini ya Rais Roch Kabore kabla ya Jeshi kufanya Mapinduzi

Soma - https://jamii.app/BFNewGovt

#JFLeo
#UKRAINE: RAIS VOLODYMYR ZELENSKY AHIMIZA VIKWAZO ZAIDI DHIDI YA URUSI

Asema ujasiri wa kutangaza wazi ukatili uliopangwa kufanyika ni ishara tosha kwa Nchi za Magharibi kwamba vikwazo vilivyowekwa dhidi ya #Russia havitoshi

Soma - https://jamii.app/UrusiVikwazo

#RussiaUkraineWar
URUSI: PADRI MBARONI KWA KUHUBIRI AMANI

Padri John Burdin amekosoa mapigano yanayoendelea kati ya Urusi na #Ukraine huku akichapisha picha za kupinga Vita

Kukosoa matumizi ya Jeshi ni jinai kwa Sheria iliyopitishwa na Bunge

Soma - https://jamii.app/PadriAmani
#RussiaUkraineConflict
Ripoti ya CAG 2019/20 ilibaini zaidi ya Miradi ya Maendeleo 68 yenye thamani ya Tsh. Bilioni 18.3 ilikuwa imekamilika lakini haitumiki

Baadhi ya Miradi hiyo ni Ujenzi wa Masoko, Miundombinu ya Shule, Hospitali za Wilaya, Vituo vya Afya na Zahanati

#JFUwajibikaji #WAJIBU #JamiiForums #Accountability
MDAU: TAKA NGUMU ZICHAKATWE KUWA MBOLEA ASILIA KUOKOA MAZINGIRA

Anasema tatizo la taka ngumu ni kubwa, na jitihada za Mamlaka pamoja na wadau mbalimbali bado hazijakidhi ukubwa wa tatizo lililopo

Anashauri maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya kutupa taka ngumu kuwekwa viwanda vya mbolea, malighafi ya chuma na plastiki badala ya kuchoma moto taka na kusababisha uchafuzi wa mazingira na athari za Kiafya

Soma - https://jamii.app/TakaNgumuSOC

#StoriesOfChange
Kuelekea Siku ya Wanawake Duniani (Machi 8, 2022), inaelezwa Wanawake na Wasichana wanakumbana na athari kubwa zaidi za Mabadiliko ya TabiaNchi, kwani yanazidisha ukosefu wa #UsawaWaKijinsia

Kukosekana Usawa wa Kijinsia ni miongoni mwa changamoto kubwa inayohitaji suluhisho la haraka, na ni wakati wa kuchukua hatua

Soma - https://jamii.app/UsawaWanawake

#IWD2022
NAMIBIA: Wanafunzi 23 wamefanikiwa kurejeshwa Nchini humo kutoka #Ukraine na Wizara ya Elimu imewataka kujiunga na Vyuo vya ndani ili kuendelea na Masomo

Wanafunzi takribani 13,000 wa #Ghana, Somalia na #Nigeria wamekwama Mjini Sumy

Soma - https://jamii.app/WanafunziNamibia

#RussiaUkraine
MTWARA: ATUHUMIWA KUUA MKE NA KISHA KUMZIKA KWENYE SHIMO

Shaibu Kauselela anatafutwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma ya kumuua Amina Mtausi (40) kwa kumpiga na kitu kizito, baadaye kumzika kwenye Shamba na kupanda Mpunga ili kupoteza ushahidi

Soma - https://jamii.app/Mtwara

#GBV
URUSI: Baadhi ya raia wameingia Mitaani kupinga hatua ya Nchi yao kuishambulia #Ukraine wakitoa maneno ya β€˜No to War’

Wizara ya Mambo ya Ndani imesema takriban Watu 3,500 wamekamatwa katika Miji 56 kwa kufanya maandamano

Soma - https://jamii.app/ProtestersRussia
#RussiaUkraineConflict
KUNYIMWA KUJIELEZA NI KUNYIMWA HAKI YA KUSHIRIKI KATIKA MAENDELEO

Ripoti iliyotolewa na Taasisi ya Article 19 Mwaka 2021 inaonesha hali ya #UhuruWaKujieleza/kutoa mawazo binafsi imekuwa ikidorora katika maeneo mengi duniani

Bila Uhuru wa Kuzungumza haiwezekani kamwe kutatua matatizo ambayo yanahitaji kutatuliwa

Soma - https://jamii.app/UhuruKujieleza
ETHIOPIA: Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Wakimbizi (UNHCR) limeripoti machafuko ya #Ethiopia kusababisha Watu milioni 2 kukimbia Makazi yao

> Mapigano ya #Tigray yamezibomoa hata kambi za Wakimbizi zilizokuwa Nchini #Eritrea

Soma https://jamii.app/EthiopiaMachafuko

#JFLeo
UPDATES: Serikali ya #Ukraine imependekeza vikwazo vya kibiashara vya kimataifa dhidi ya Urusi ikiwemo kuzuia mafuta ya Taifa hilo ikisema 'Vita viwalishe'

Vikosi vya Moscow vinaushambulia Mji wa #Mariupol na Raia 300,000 wanasubiri kuondolewa

Soma - https://jamii.app/MafutaUrusi
SIMIYU: WATENDAJI WA SERIKALI WAKAMATWA KWA WIZI WA CHUPA ZA DAWA

Watu 12 wakiwamo Watendaji wa Serikali za Mtaa wamekamatwa wakidaiwa kuiba Chupa 434 za Dawa za kuua wadudu wa Pamba zilizotolewa na Serikali kwa Wakulima Wilayani Bariadi

Soma - https://jamii.app/WiziSimiyu

#JFLeo
URUSI YATOA MASHARTI YA KUACHA KUISHAMBULIA UKRAINE

Imeitaka Ukraine kuitambua #Crimea kama sehemu ya #Russia, na Donetsk and Luhansk kama Mataifa huru

Aidha, #Ukraine imetakiwa kubadili Katiba na kukataa kuingia katika kambi yoyote kama NATO

Soma - https://jamii.app/UrusiMasharti
WANAFUNZI WA KITANZANIA WATOKA SALAMA UKRAINE

Waziri wa Mambo ya Nje, Balozi Liberata Mulamula amesema Wanafunzi wapatao 150 wamevuka salama na kukimbilia nchi za Poland, #Hungary, Romania na #Denmark. 23 wamefanikiwa kurejea Tanzania

Soma - https://jamii.app/WatanzaniaSalama

#JFLeo
#BURUDANI: Watu wengi hasa Vijana wanapenda kuangalia Filamu (#Movies). Filamu hizi huburudisha, huchangamsha na kutoa mafunzo kwa Jamii

Je, ni Filamu gani uliyowahi kuangalia zaidi ya mara moja na bado huichoki?

Mjadala - https://jamii.app/FilamuBurudani

#Entertainment #JamiiForums
SERIKALI: WATU 8 WAFARIKI DUNIA KWA #COVID19 NDANI YA MWEZI MMOJA

Visa vipya 290 viliripotiwa kuanzia Februari 5 - Machi 4, 2022. Wagonjwa 136 walilazwa na 128 kati yao hawakupata chanjo

Idadi ya waliopata dozi kamili ya chanjo Nchini ni 2,664,373

Soma https://jamii.app/8COVID19