JamiiForums
βœ”
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
TABORA: AMUUA BABA YAKE KWA SHOKA AKIMSHUTUMU KWA USHIRIKINA

Maiko Jacobo (25) mkazi wa Kijiji cha Upungu, Nzega anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kumuua baba yake mzazi, Jacobo Lubela (88) kwa kumkata kichwani, shingoni na mikono yote miwili

Soma - https://jamii.app/TaboraMauaji
MDAU: WATOTO WA NJE YA NDOA HUATHIRIKA KISAIKOLOJIA KWA KUKATALIWA

Anasema Watoto wa nje wanapata shida sana na kuathirika Kisakolojia hasa pale wanapohisi kukataliwa au kutokutambulika. Wengi huonekana kama Maadui na wezi wa Mali zilizotafutwa ndani ya Ndoa

Ameongeza, zipo sababu nyingi zinazopelekea kupatikana kwa Watoto wa nje ya Ndoa, ila Hisia zisitumike sana kwani huweza kuzalisha Uadui baina ya Watoto

Msome zaidi - https://jamii.app/WattNjeNdoa
#JamiiForums #Malezi
UKRAINE: KITUO CHA MITAMBO YA NYUKLIA CHASHAMBULIWA NA URUSI

Kituo cha Mtambo mkubwa wa Nishati ya Nyuklia Barani Ulaya, #Zaporizhia kimeshambuliwa usiku wa kuamkia leo

Ukraine yataka kusitishwa kwa mapigano ktk eneo hilo ili kuepusha Maafa

Soma - https://jamii.app/ZaporizhiaAttack

#JFLeo
UPDATES: Ukraine na #Russia zimekubaliana kutengeneza na kuweka maeneo salama ya kibinadamu ili kuruhusu Raia kuondolewa

Pande zote zimethibitisha Makubaliano hayo, lakini #Ukraine imesema bado haijapata matokeo inayohitaji

Soma - https://jamii.app/RussUkrAgree

#RussiaUkraineCrisis
Katika Ukaguzi wa Mapato ya Ndani ya Mamlaka za Serikali za Mitaa (MSM) 43 kwa kipindi cha 2017/18 - 2019/20, CAG alibaini kutokusanywa kwa Tsh. Bilioni 60.81 ambazo ni Mapato ya Ndani

Ukaguzi wa 2019/20 umeonesha kuongezeka kwa kutokusanywa kwa Mapato ya Ndani kwa kipindi cha 2016/17 - 2019/20.

#JamiiForums #JFUwajibikaji #Accountability #WAJIBU
#BURKINAFASO: JESHI LATEUA WAZIRI MKUU WA MPITO

Albert Ouedraogo ambaye ni Raia wa kawaida anatarajiwa kuunda Serikali Mpya ambayo jukumu lake kubwa litakuwa kudhibiti ghasia ambazo zimegharimu maisha ya maelfu, huku Mamilioni wakikimbia makazi

Soma - https://jamii.app/BurkinaPM
#UKRAINE: Wanajeshi wa #Russia wameukamata Mji Muhimu wa Bandari na kuuzingira mwingine kama sehemu ya juhudi za kuitenganisha nchi hiyo na Pwani yake

> Pia, umeme na mawasiliano ya simu vimekatwa huku chakula na maji vikikosekana

Soma - https://jamii.app/Urusi

#RussiaUkraineCrisis
KESI YA MBOWE: JAMHURI YAWASILISHA HATI YA KUFUTA KESI

Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) leo, Machi 4, 2022 amewasilisha hati ya kutokuwa na nia ya kuendelea na kesi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na wenzake 3 ktk Mahakama Kuu

Soma - https://jamii.app/KufutaKesiMbowe
FREEMAN MBOWE NA WENZAKE WAACHIWA HURU

Mahakama Kuu imemwachia huru M/Kiti wa CHADEMA Taifa pamoja na wenzake 3 waliokuwa wakikabiliwa na Mashtaka ya Ugaidi

Pia, Jaji kaagiza vielelezo vilivyowasilishwa Mahakamani wakati wa Kesi navyo kuachiwa

Soma - https://jamii.app/KufutaKesiMbowe
MSUMBIJI: Rais Filipe Nyusi amemfukuza kazi aliyekuwa Waziri Mkuu, Carlos Agostinho do RosΓ‘rio na kumteua Adriano Afonso Maleiane ktk nafasi hiyo

> Ernesto Max Tonela anakuwa Waziri wa Fedha na Uchumi, Carlos Zacarias kuwa Waziri wa Nishati na Madini

Soma: https://jamii.app/Msumbiji
MDAU: TUMJALI MTU ZAIDI PALE ANAPOKUWA MGONJWA KULIKO AKIWA MAREHEMU

Anasema Mtu akifariki kunakuwepo na michango na misaada mingi kwa ajili ya Msiba lakini Marehemu alipokuwa anaumwa huenda Ndugu na Marafiki hawakutoa msaada wowote

Aidha, baadhi ya wachangiaji wanasema kama Mtu huna ushirikiano mzuri na Watu hata unapopata matatizo pia utakosa wa kukupa msaada.

Una maoni gani?

Mjadala - https://jamii.app/KujaliWatu
#Maisha
URUSI: Bunge limepitisha Sheria inayoruhusu Mamlaka kuwafunga hadi miaka 15 watu walioshtakiwa kwa kusambaza makusudi taarifa zisizo na ukweli kuhusu Jeshi la Nchi hiyo. Sheria hiyo pia inafanya wito wa vikwazo dhidi ya Urusi kuwa Kosa la Jinai

Soma - https://jamii.app/JeshiUrusi
SHINYANGA: Madirisha Kanyalu (60) amejiua kwa kujitumbukiza kisimani baada ya kumuua mtoto wake, Meshack Madirisha (miezi 11) na mkewe Evodia Nyerere (27), akimtuhumu mkewe kwa usaliti

> Tukio hilo limetokea Februari 2, 2022 ktk Kijiji cha Bulambila

Soma - https://jamii.app/Ajiua
Balozi wa Marekani Nchini Tanzania, Donald J. Wright amesema kuachiwa kwa Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe ni nafasi nzuri kwa Tanzania kubadili ukurasa na kutazama maisha yajayo

Soma - https://jamii.app/USAMbowe

#JamiiForums
SIKU YA KIMATAIFA YA UFAHAMU WA VIRUSI VYA PAPILLOMA - HPV

'Human Papilloma Virus' au #HPV ni kirusi ambacho husambaa kwa njia ya kujamiiana. Asilimia kubwa ya Watu wenye maambukizi ya HPV hupata vipele au #GenitalWarts, maumivu au Damu wakati wa Tendo, kuwashwa n.k

HPV huweza kusababisha aina mbalimbali za Saratani kwenye Mwili wa Binadamu ikiwemo Saratani ya Shingo ya Kizazi, Saratani Njia ya Haja kubwa n.k. Takriban Saratani zote za Shingo ya Kizazi hutokana na HPV za aina mbili, HPV16 na HPV18.

Soma - https://jamii.app/HPVDay2022
#Afya #Cancer
UKRAINE: WANAFUNZI WA KITANZANIA KUONDOLEWA KUPITIA URUSI

Ubalozi wa Tanzania Sweden na Ubalozi wa Tanzania #Moscow unawaondoa Wanafunzi waliopo Chuo cha Sumy kupitia mpaka wa Urusi

Zoezi hilo linaratibiwa na Serikali ya Urusi

Soma https://jamii.app/WatzSumy
#RussianUkrainianWar
Rais Samia Suluhu Hassan leo Machi 4, 2022 amekutana na kuzungumza na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe

Soma zaidi > https://jamii.app/MboweSamia
URUSI: Sheria inayoruhusu Mamlaka kuwafunga hadi miaka 15 wanaoshtakiwa kusambaza makusudi taarifa feki imepelekea BBC, CNN, Bloomberg, CBC na Redio Canada kusema zitaacha kurusha Matangazo kwa muda Nchini humo ili kulinda Wanahabari

Soma - https://jamii.app/NewsRussia

#PressFreedom
URUSI: MEJA JENERALI AMSHAURI PUTIN WAPIGE MAPIGO MABAYA ILI UKRAINE IJISALIMISHE

Kiongozi wa #Chechnya, Ramzan Kadyrov amemshauri Rais Putin asikubali mazungumzo

> Ameshauri kuipiga #Ukraine haraka sana kwani kuchelewa kunafanya waongezewe vikwazo

Soma https://jamii.app/ChechnyaUrusi
AFRIKA KUSINI KUHARIBU DOZI 100,000 ZA CHANJO YA PFIZER

Afrika Kusini imerekodi idadi kubwa ya Maambukizi na vifo vya #CoronaVirus katika Bara la Afrika, hata hivyo utoaji Chanjo umepungua huku Nchi ikiwa na akiba ya kutosha ya dozi milioni 25

Soma - https://jamii.app/ExpireVaccineSA
MABEYO AWASAMEHE WALIOFUKUZWA JKT, WARUDISHWA JESHINI

Mkuu wa Majeshi, Jenerali Venance Mabeyo ametoa msamaha kwa Vijana 853 waliofukuzwa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Aprili Mwaka 2021

Wanatakiwa kupokelewa kambini Machi 12, 2022

Soma - https://jamii.app/JKTMabeyo

#JFLeo